Walimu punguzeni mitihani mashuleni.

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
3,945
Reaction score
12,459
Walimu hasa wa kike mnafosi wazazi wawalipie vikoba vyenu kwa gia ya mitihani ya kila siku. Au hawa watoto wetu siku hizi wamekuwa vilaza? Tofauti na sisi wazazi wao?

Mbona technology imewarahidishia sana hawa watoto wa sasa, material wanapata kwa urahisi sana tofauti na sisi hapo nyuma.



Your browser is not able to display this video.
 
Kabisa kabisa
Wamezidi aisee, Yaaan Walimu wametufanya sisi wazazi ATM michango kila siku, hela za mitihani n.k Serikali iingilie hili swala yaani Ssasa hv shule za private zina afadhali kuliko za Serikal
Mfano mzuri kuna shule hapa Chanika zinaongoza kwa walimu kufosi king
Yaani wao wamenunua hadi magari kwa kutukamua
WIZARA YA ELIMU NA SERIKALI TAZAMENI HILI WAZAZI TUMECHOKA
 
Miaka yetu mihitani ilikuwa sana, hadi ya shule za ujirani kabla hata ya vikoba kuwepo wala mtandano wa Vodacom Tanzania kutokuwepo mitihani inaongeza ushindani na juhudi sana kwa wanafunzi.. Kama hela ipo wapeni watoto wakafanya jipime mbavu
Iwepo lakini sio kila siku, wanasoma saa ngapi, masahahisho wanafanyiwa saa ngapi na ingekuwa inawasaidia tungeona matokeo ya darasa la saba mambo yakibadilika lakini ni yale yale shule za private hazina hiyo mitihani ya kila siku imebaki ile mitihani ya likizo tuu, na kama mwalimu anataka kuwajaribu watoto wake anaandika mtihani kwenye karatasi inatolewa kopi kesi imeisha
 
Nimepigia gharama za mitihani yote

Hayaaaa hata kama ni sh 1000 ndo mje kulia huku kama ving'ora vya magari ya ndejembi..? πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Kopi ikiwa bei kuuubwaa ni sh.100.Okay,si mbaya lakini mitihani isizidi muda wa kujifunza na kufundishwa kwa wanafunzi.Kila siku!?
 
Mzee enzi zetu hiyo mitihani tulikuwa tunaitafuta, na tulikuwa tuna wish kila wiki tupige, shule vs shule, yaani mtu unakaa unajiuliza wiki hii wapi kuna paper . sema pia nje ya hilo ndio tulikuwa tunapatiaga na mademu 🀣🀣🀣
 
Mimi mawazo yangu, shule zianzishe kuwataka wazazi kupeleka walau karatasi za A4 bunda mbili kwa mwaka.
 
Mzee enzi zetu hiyo mitihani tulikuwa tunaitafuta, na tulikuwa tuna wish kila wiki tupige, shule vs shule, yaani mtu unakaa unajiuliza wiki hii wapi kuna paper . sema pia nje ya hilo ndio tulikuwa tunapatiaga na mademu 🀣🀣🀣
Siku hizi sio mtihani ya kuwapima watoto uwezo, nakumbuka ilikuwa ikiandaliwa mitihani ya kata wanachaguliwa wa kwenda kufanya sio wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…