Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

Kama kuchapia naona hapa Mkuu wa wilaya amechapia.Kesho manesi na madaktari watalalamika nao watapanda daladala bure.Nadhani wafanyakazi biashara na wafanyakazi wa mashirika na makampuni binafsi ndiyo yatalipia nauli.Mh!!!
 
Wazo la Makonda la kuwapandisha walimu daladala bure ni la fedheha na aibu sana kwa taaluma ya Mwalimu. ifike mahali umaarufu wa siasa ufike kikomo na mambo ya msingi yafanyike.

kama kweli unataka kuwapa motisha walimu, waboreshee maslahi yao, wape Vifaa bora vya kufundishia na uboreshe miundo mbinu ya maeneo ya kazi.

na kama unataka kuwapa unafuu wa usafiri, basi wape cash kama allawance kwenye mishahara au wape Mikopo nafuu ya Magari au nunua staff basi maalumu kwa ajili ya walimu.

hili ya kuwapandisha daladala bure kiukweli ni fedheha na uzalilishaji.

Yaani Mwanafunzi alipe 200 halafu Mwalimu apande buree. Haiingii akilini.

Ukweli ndo huo.
 
Najaribu kuliangalia hili swala na hali halis ya jiji la dsm ,naona kama itakuwa ngumu vile ,embu vuta picha asubuhi watu wanavyogombania daladala halafu ifike muda wa kutoa nauli mtu anakupa kitambulisho cha ualimu ,na jamaa zetu walivyoo na maneno mabaya hii si itakuwa kutiana aibu jamani..
 
huenda ni kwa magari ya mradi wa mabasi yaendayo kasi hili litatendeka, bali ikiwa ni hizi daladala hapo hamna tija ni fedheha na dharau kubwa kwa Mwalimu, na hili litawaumiza sana akina mama walimu.
 
kwahiyo walimu nao watakuwa wanachelewa shule kwa sababu usafiri ni mgumu

ni nani aliyeloga viongozi wetu kuwa na ufikiri mdogo sana

eeeh mungu angalia taifa lako tanzania
Nikiyafikiria mahubiri ya Leo kwba kuna viongozi ambao hawajui kuongoza na hawajui kwamba hawajui kuongoza,na kuna viongozi ambao wanajua kwamba hawajui kuongoza sasa huyu sijui atakuwa kundi lipi.
 
yaan akiwa na mtoto wake,mtoto analipa afu mzazi halipi,dah patamu hapo
 
Hicho ndo wanachotaka walimu jibu hapana kama wanawaonea huruma walimu wawape fedha ya nauli ya mwezi na sio hicho wanachokifanya.
 
huenda ni kwa magari ya mradi wa mabasi yaendayo kasi hili litatendeka, bali ikiwa ni hizi daladala hapo hamna tija ni fedheha na dharau kubwa kwa Mwalimu, na hili litawaumiza sana akina mama walimu.
Kama ni kuwajali walimu angepigania maslahi yao yanayokwamishwa na serikali na si kitu kidogo kama nauli
 
Huyu bwanamdogo ni jipu toka kitambo! Maamuzi mengine yafaa kuwa universal; k'ndoni siyo nchi, nawaunga baadh ya wadau hapo juu kwamba tatizo LA mwalimu ni zaid ya hiyo nauli!
Me ni mwalimu pia, nachoona hapo ni siasa kwenye mambo ya msingi! Maamuzu hayo hayajalenga kumsaidia mwlm was nchi hii Bali kumdhalilisha na kumfanya awe inferior. Yawezekanaje mwanafunzi anaelipa 200 akeshe kituoni na mwalm apande bure tukiamini atawahi kazini? Me naona anatutekenya walimu huku anacheka yeye!!!
Nasubir nione matokeo!
Kama wewe ni mwalimu basi kazi ipo!
Samahani kwa kuanza hivyo lakini naona tatizo ni kubwa zaidi kwa walengwa katika uelewa huu....
Mnataka DC awafanyie nini???
Yule amejitahidi kwa nafasi yake na anafanikisha usafiri kwenda na kutoka kazini bure na bado mnaona hakuna lolote!
DC sio waziri wa elimu, sio waziri wa fedha, sio mwajiri! Anafanya mahusiano kwa nia njema....
Kama unadhani utadhalilika, usipande basi na kujitambualisha kuwa wewe ni mwalimu ili ulipe nauli.
DC Hongera kwa u ubunifu wako huo...WANAKUONEA GERE! PIGA KAZI.
 
Uzalilishaji kwa walimu waongezewe maslai wapewe ela za nauli waweze kusafiri kwa Uhuru huku ni kufanya walimu waonekane ni wafanyakazi Wa chini katika jamii yeye angesema wanafunzi wasafiri bure
Fedha ni kichocheo cha kuhamasisha mtu kufanya mazuri kweli. Pia hali ya walimu kuhisi wanathaminiwa na kukubalika katika jamii yao nayo pia hutoa hamasa ya kufanya vizuri shuleni. Tumuunge mkono DC Makonda na tutowe mawazo chanya.
 

KAMA NAWAONA WALIMU WATAVYONYANYASWA NA MAKONDAKTA WA DALADALA,
TENA BORA HATA WANAFUNZI WATATHAMINIWA KWA KUWA WANALIPA 200/=
KULIKO WALIMU WATAKAOPANDA BURE.
______
NAUONA MTITI ZAIDI PALE KONDA ANAPOONDOA GARI PALE MAWASILIANO AU MAKUMBUSHO KUELEKEA MBEZI, TEGETA, GONGO LA MBOTO
NA
MBAGALA AKIAMINI AKIAMINI KABISA KUWA BASI LIMESHAJAZA ABIRIA ZAIDI YA 40,

KUMBE WOTE NI WAALIMU!
____________
TASWIRA MPYA NAIONA PALE 97.8% YA WABONGO TUTAVYOGEUKA WAALIMU KWA KUTEMBEA NA VITABU VYA KEMIA NA CIVICS WAKATI NI WAMACHINGA TU WA PALE mtoni KWA AZIZI ALLI,

NA
IKIZINGATIWA HATUONI KAZI KUFOJI VITAMBULISHO VYA KAZI YA UALIMU ILI TUPUNGUZE MAKALI YA NAULI.
_____

INGAWA SIJAJUA KAKA'ANGU @KAKA_MAKONDA AMEANDAA STRATEGIES ZIPI,
ILA
NASUBIRI KUSHUDIA VICHWA VYA UTOSI NA MAKONZI WATAYOPIGWA NDUGU WALIMU KWENYE DALADALA.

NIMEMALIZA!
Toa suluhu ya hayo uliyoyahisi kuwa yatatokea. Mbona tu mafundi wa kulalamika na kufikilia kushindwa tu?
 
Walimu wa shule za msingi na sekondari za umma mkoani Dar es Salaam wataanza kusafiri bure kwenye daladala kuanzia tarehe 7 Machi 2016.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paulo Makonda na viongozi wa vyama vya usafirishaji abiria jijini Dar wanazungumza na wanahabari hivi sasa.

Walimu wstatengenezewa vitambulisho maalum ili kuwaondolea usumbufu.

Huduma hiyo ni katika kuwapunguzia adha ya usafiri na ugumu wa maisha ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure.

Muda wa kuwasafirisha bure ni saa 11.30 hadi 2 asubuhi na saa 9 hadi 11 jioni.
Tunaomba maelezo zaidi!

A word of caution to mh. Magufuli there is more to this dc than meets the eye. Gut feeling.! Nothing makes sense.

Tujiulize,
Aliyegharamia service za magari zilizotolewa free ni nani?
Aliyegharamia check up ya moyo ni nani?
Uhusiano wa Dc na waliotoa huduma pamoja na misaada mbali mbali ni upi?
Anayelipia walimu dala dala bure ni nani?

Hamna cha bure dunia hii! Kama ulipii moja kwa moja, utalipia bila kujua au mtu mwingine analipia.

Au inawezekana kabisa huyu dc ana uwezo mkubwa wa kumsoma Rais aliye madarakani na ku act accordingly.
 
Kama watatengenzewa kitambulisho ambacho kinawekeka mfukoni au kwenye handbags sioni Kama kutakuwa na manyanyaso mana mwalim ataingia kwenye Gari bila hata kujulikana Kama ni mwalim ila wakat wa konda anadai chake ndo pale anaonyeshwa kitambulisho, pia nafkiri iwekwe sheria kali kwa konda yoyote atakae mnyanyasa mwalim.mbona hatujawah kuskia wanajeshi wananyanyasika kwenye madaladala? Hii nchi sheria zikisimamiwa vizuri kila mtu atakuwa na adabu na hata mwanafunzi anaweza kusafiri bure tuache ujinga ujinga
Ikatokea gari ya siti 20 ikajaa walimu siti 15 itakuwaje??? Kwamba nae akubali tu hasara sio
 
Duh walimu nataka niwasikie wenyewe je mmekubaliana na hilo au sio?
 
Back
Top Bottom