Ha ha ha mkuu bhana☝
KAMA NAWAONA WALIMU WATAVYONYANYASWA NA MAKONDAKTA WA DALADALA,
TENA BORA HATA WANAFUNZI WATATHAMINIWA KWA KUWA WANALIPA 200/=
KULIKO WALIMU WATAKAOPANDA BURE.
______
NAUONA MTITI ZAIDI PALE KONDA ANAPOONDOA GARI PALE MAWASILIANO AU MAKUMBUSHO KUELEKEA MBEZI, TEGETA, GONGO LA MBOTO
NA
MBAGALA AKIAMINI AKIAMINI KABISA KUWA BASI LIMESHAJAZA ABIRIA ZAIDI YA 40,
KUMBE WOTE NI WAALIMU!
____________
TASWIRA MPYA NAIONA PALE 97.8% YA WABONGO TUTAVYOGEUKA WAALIMU KWA KUTEMBEA NA VITABU VYA KEMIA NA CIVICS WAKATI NI WAMACHINGA TU WA PALE mtoni KWA AZIZI ALLI,
NA
IKIZINGATIWA HATUONI KAZI KUFOJI VITAMBULISHO VYA KAZI YA UALIMU ILI TUPUNGUZE MAKALI YA NAULI.
_____
INGAWA SIJAJUA KAKA'ANGU @KAKA_MAKONDA AMEANDAA STRATEGIES ZIPI,
ILA
NASUBIRI KUSHUDIA VICHWA VYA UTOSI NA MAKONZI WATAYOPIGWA NDUGU WALIMU KWENYE DALADALA.
NIMEMALIZA!
Kama wamiliki wa magari wameridhia, Kondakta au dereva atakataa vipi?
Askari Si wanatumia ubabe na dezo ndio maana wakustaafu life inawashindaVipi kuhusu askari
Yaani wewe kila mwenye mawazo tofauti na yako ni bavicha! Sijawahi kuona mhaya hopeless kama weweRuttashobolwa said:Hivi we Bavicha madereva wana mamlaka kuzidi Maboss wao wamiliki wa hayo magari? Hivi Bavicha mnashida gani?
Yes, wakiongezewa maslahi watajisafirisha wenyewe kma wafanyakazi wengine na hii itaondoa msuguano na makondakta.Uzalilishaji kwa walimu waongezewe maslai wapewe ela za nauli waweze kusafiri kwa Uhuru huku ni kufanya walimu waonekane ni wafanyakazi Wa chini katika jamii yeye angesema wanafunzi wasafiri bure
Walimu msikubali kudhalilishwa namna hii! yaani muanze kuzuiwa mlangoni kama watoto wa shule?!
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kwa kushirikiana na wamiliki wa vyombo vya usafiri Dar es salaam wametangaza kuanzisha mpango wa kuwasaidia Walimu wa Shule za Serikali kwa kuwapatia huduma za usafiri bure katika daladala.
Akieleza mbele ya waandishi wa habari Makonda amesema ‘Nilianza kuongea na vyama vya usafirishaji kisha kujenga hoja dhidi ya changamoto za Walimu wetu, na nikawaomba viongozi hao tuonane kulijadili hili na kisha tukafika muafaka ’
‘Na muafaka huo ningependa kuwatangazia Walimu na Watanzania, yakwamba sasa kuanzia tarehe 7/3/2016 Walimu wa Shule za msingi na wasekondari watasafiri bure kwenye vyombo vyetu vya usafiri kwa Mkoa wa Dar es salaam’
‘Tumeweka utaratibu, Walimu watalazimika kutengenezewa vitambulisho maalum ambavyo kila Shule itatengeneza vitambulisho vyake, huku kukiwa na mambo manne ya kuzingatia ambayo ni 1. Picha ya Mwalimu husika, 2. Jina la shule 3.Namba ya Mkuu wake wa shule 4. Kuwe na sahihi ya Mkuu wa Wilaya Paul Makonda’
source:MILLARDAYO.COM