Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

Walimu Dar kusafiri bure kwenye daladala

Walimu bure, wanafunzi wao wanalipa nauli sh 200.

Angalia kitakachotokea:
1. Mwanzoni makonda (wa daladala, siyo Paulo) na madereva watakuwa wanawagundua walimu baada ya kuonyeshwa vitambulisho wakati walimu wameshapanda.

2. Baada ya muda makonda & madereva watawakariri walimu wa njia/route/vituo vyao na watakuwa wakiwakimbia na kupaki mbele zaidi au nyuma zaidi, na kuchukua abiria juu kwa juu ili mradi kuwakwepa walimu. Wenzangu tuliosomea Dar Form One to Six tunajua issue za daladala na madenti, sembuse walimu wasiolipa hata senti tano?
Kumbuka hesabu ya tajiri ipo palepale, haijalishi walimu wanalipa au hawalipi.

3. Matokeo ya walimu kukimbiwa na daladala (baada ya kukaririwa sura) ni kwamba ndio watachelewa zaidi kufika kazini/shuleni kuliko ilivyo sasa.
Na huo ndio ukweli. Hata asikari wanakimbiwa hivyo hivyo. Daladala wako radhi wapate hasara ya mafuta kwa kubadilisha njia ili kuwakwepa wapanda dezo. Kweli watu wadalala wanaonewa. Hawapewi ruzuku, mafuta yako palepale, vipuri viko pale pale, hesabu ya siku iko pale pale, kula yao iko pale pale, kodi iko pale pale na trafik wanawasubiri njiani wawapige bao halafu bado "wanaombwa" na serikali inayokusanya kodi zaidi ya trilioni 1 kwa mwezi nyingine ikitoka kwenye daladala hizo hizo watoe usafiri bure kwa baadhi ya makundi ya watu kama askari na walimu. Hiyo ofa bora wangepewa walemavu na vikongwe
 
Makonda anatapatapa tu.Hana jipya ni mpuuzi tu.
Kero ya walimu sio usafiri tu.Wanafunzi wanlipa shilingi mia mbili bado wananyanyaswa na wenye vyombo vya usafirishaji.
Makonda unakimbilia kutatua kero za walimu..wanafunzije?
 
Hili wazo la waalimu wa kinondoni kusafiri bure ni wazo la kijinga kabisa. Waalimu wengi wa wilaya ya kinondoni ni wanawake ambao wameolewa na maafisa wakubwa serikalini pamoja na wafanya biashara maarufu. Wengi wao wana usafiri binafsi. Halafu kwa nini waalimu wa kinondoni tu? wa vijijini ambao hawana hata baiskeli wakipimbilie kwa nani?
 
Vya bure vinaua, hapo hawajafikri kwa mapana naona kwa mbili mwalimu akiambiwa wewe subiri kwanza, halfu baadaye anaambiwa panda na kaa hapo, ile sehemu iliyo nyuma ya kiti cha dereva kwenye injini. Sasa hapo si kumdhalilisha mwalimu, yaani kama ni kumsaidia mwalimu wangetoa pesa ya nauli au mazngira magumu kwenye mshahara wao, zeni mwlimu alipe nauli na kueshimiwa ndani ya daladala, vingnevyo ni kutafuta kiki uku Ukidhalilisha wengine
 
Hivi Makonda ndio msemaji wa mkoa?
Basi Sadick Meck Sadick afutwe tu kazi Makonda apewe u-RC.
 
Very good for Dar.Vipi kuhusu mikoani na vijijini...?????Huu utakuwa muendelezo wa matabaka.....tuwe waangalifu kweli kweli.Sasa migomo itahamia kwa waalimu...watafudisha below standard.
 

KAMA NAWAONA WALIMU WATAVYONYANYASWA NA MAKONDAKTA WA DALADALA,
TENA BORA HATA WANAFUNZI WATATHAMINIWA KWA KUWA WANALIPA 200/=
KULIKO WALIMU WATAKAOPANDA BURE.
______
NAUONA MTITI ZAIDI PALE KONDA ANAPOONDOA GARI PALE MAWASILIANO AU MAKUMBUSHO KUELEKEA MBEZI, TEGETA, GONGO LA MBOTO
NA
MBAGALA AKIAMINI AKIAMINI KABISA KUWA BASI LIMESHAJAZA ABIRIA ZAIDI YA 40,

KUMBE WOTE NI WAALIMU!
____________
TASWIRA MPYA NAIONA PALE 97.8% YA WABONGO TUTAVYOGEUKA WAALIMU KWA KUTEMBEA NA VITABU VYA KEMIA NA CIVICS WAKATI NI WAMACHINGA TU WA PALE mtoni KWA AZIZI ALLI,

NA
IKIZINGATIWA HATUONI KAZI KUFOJI VITAMBULISHO VYA KAZI YA UALIMU ILI TUPUNGUZE MAKALI YA NAULI.
_____

INGAWA SIJAJUA KAKA'ANGU @KAKA_MAKONDA AMEANDAA STRATEGIES ZIPI,
ILA
NASUBIRI KUSHUDIA VICHWA VYA UTOSI NA MAKONZI WATAYOPIGWA NDUGU WALIMU KWENYE DALADALA.

NIMEMALIZA!
Hapa ni kuwatengenezea chance ya kughalilika dhidi ya makondakta tu, cha msingi ni kuwaongezea mishahara tu hawa walimu kama kweli mkuu wa wilaya ya kinondoni na serikali kwa ujumla wameamua kuwajali hawa watu tafadhari.
 
Nani alimshauri huyu Makonda?, kama ni wazo toka kichwami kwake basi uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana,tena Sana, anachotaka kusema ni kuwa walimu wapewe "special privilege", ila kwa hili na hakika CWT watoa tamko la kukataa ofa hii. Sulihisho ni kuongeza mishahara ya Walimu kama hadi wanaamini wanapaswa wasilipe nauli basi (kima cha chini kiwe angalau Milioni Moja), mazingiza ya kufundishia yawe Bora na huduma zingine wanazolalamikia.
 
binafsi nafikiri amejitahidi kujaribu anachofikiria kama kinawezekana.yeye hana fedha alichotumia in nafasi ndogo ya kisiasa aliyo nayo kutoa mchango wake kwa jamii hilo linahitaji pongezi lakini kinachotakiwa in jinsi gani hili wazo lake liboreshwe ikiwa ni pamoja na manispaa husika kuangalia uwezekano wa kuwapa waalimu posho ya usafiri kitu ambacho wanaweza wastani wa shilingi 3000 kwa Sikh kwa mwezi SK 20 sawa na shs 60,000 tu sidhani kama manispaa waalimu wanazidi 3000 . si vzr kubeza kabla ya kubeza angalia wewe umetoa mchango gani kwa jamii au unaongeza vyeti tu? tujifunze kushukuru kisha ndipo tuone jinsi ya kupambanua changamoto zake kwanza in swala la hiyari halazimishi mwalimu kuchukua kitambulisho
 
Waendelee kulipa nauli.

Kama kweli wanawajali wawaongezee mishahara.

Haya mambo ya kupanda panda bure vyombo vya usafiri yamepitwa na wakati.

Mafuta kila siku yanapanda bei.

Sasa hao Walimu si wanaharibu hesabu hapo.

Angalieni na upande wa pili, mmiliki wa chombo.

Kwakuwa unamiliki chombo cha usafirishaji haina maana kwamba wewe unaemiliki chombo hauna matatizo
 
Hebu nyie wenyewe angalieni.

Polisi apande bure.

Mwanajeshi apande bure.

Na Mwalimu apande bure.

Jamani, kazi si watakuwa wanafanyiwa wao.

Na huo muda waliowekewa Walimu ndio muda wa kazi, baada ya saa Mbili asubuhi vichwa vinakuwa vya kuokota
 
Usiwe mtabiri kwa kitu usichokijua! tumeelezwa kuwa DC makonda kafanya kikao na wamiliki wa daladala na wakakubaliana mambo kadhaa, unafahamu msingi wa makubaliano hayo yalivyofikiwa?
Hebu Ww Tuambie Huo Msingi Wa Hayo Mazungumzo Basi!! Narudia Kama Hajui Uliza, Hilo Suala Si La Kisiasa!!! Kwani Kukutana Na Wamiliki Ndio Nini!!?? Wamiliki Umeona Wapi Wakiendesha Hizo Daladala Zao!!!?? Au Lini Wamewapatia Mikataba Ya Ajira Hao Wanaoziendesha Hizo Daladala!!!?? Kama Wao Wamiliki Wanachokijua Ni HESABU Yao Ya Siku Na Gari Lake Limejazwa Mafuta!! Sasa Suala La Kukubali Hao Waalimu Wanasafiri Bure Ktk Magari Yao Linawahusu Nini!!?? WAO Wanajua Mzigo Huo Utakuwa Wa Madereva Na Makondakta Wao, Kwa Kukosa Posho Zao!! Kama Kweli Hao Wamiliki Sio Wanafiki Wanaotumika Tu!! Wawapatie Watumishi Wao Mikataba Yao Ya Ajira, Wawalipe Mishahara Na Kuwalipia Bima Za Afya, Mifuko Ya Kijamii, Walipe Kodi Kutoka Mishahara Yao!! Ama Wapunguze Sehemu Yao Hesabu Zao Za Kila Siku, Ili Kufidia Gharama Za Kuwasafirisha Waalimu, Polisi Na Wanajeshi Bure!! Otherwise Ni Wanafiki Wakubwa!!! Wanajua Ni Nani Ambaye Ataubeba Mzigo Huo!!!
 
Utani wa jadi kati ya:-
Mgambo na wamachinga
Simba na Yanga
Konda na mwanafunzi akikaa
Konda na mwalimu akitoa kitambulisho.
Niwatakie kila la heri walimu wangu katika pambano linalosubiriwa kwa hamu kati ya Konda na Ticha ila niwakumbushe msivae nguo nyeupe au tai vifinyo vya konda vitakuumbua duh walimu nawaelewa sana wenyewe wapo kimya naamini kuondoa shari watavipokea vitambulisho na ITV itaonyesha laivu makabidhiano ila siamini kama watavitumia.
 
Nashindwa kuelewa....hiv kuna siku siku walimu wamewahi kuwalalamikia nauli?au ndo Yale ya kuomba mkate na kupewa jiwe?
 
Kweli
Kama watatengenzewa kitambulisho ambacho kinawekeka mfukoni au kwenye handbags sioni Kama kutakuwa na manyanyaso mana mwalim ataingia kwenye Gari bila hata kujulikana Kama ni mwalim ila wakat wa konda anadai chake ndo pale anaonyeshwa kitambulisho, pia nafkiri iwekwe sheria kali kwa konda yoyote atakae mnyanyasa mwalim.mbona hatujawah kuskia wanajeshi wananyanyasika kwenye madaladala? Hii nchi sheria zikisimamiwa vizuri kila mtu atakuwa na adabu na hata mwanafunzi anaweza kusafiri bure tuache ujinga ujinga
bwana Katamya:Tatizo wanachi wengi sasa tumekuwa majuha mimi nadhani suala hili si baya.Kwa nyongeza nadhani serikali za Dar zingeangalia pia walimu wanao hamishika waende hukohuko wanako tokea ili kupunguza sasa kasi ya kusafiri. Mfano. Mwalimu kajenga Bunju anafundisha majimatitu akahamishiwe Bunju hukohuko au shule jirani yake. Anayeishi Mbezi Kwa Msuguli na anafundisha Kigamboni au mbagala au maeneo mengine kama huko wanabadilishiwa mwelekeo wanafundisha Karibu.Suala hili litasaidi kupunguza tatizo la walimu hao kurundikana kwenye daladala moja kwani mrundikano kwenye daladala ndo chanzo cha manung'uniko. Daladala ikiwa na askali 2,walimu 3, wanafunzi 3 ndo ugomvi unaanza tu. Huo ni mtazamo wangu usio hitaji matusi. Big Up DC Makonda.
 
Mawazo ni mazuri lakini changamoto yake ni kubwa Sana. Walimu wetu watanyanyasika Sana. Wazo nzuri ni kuwapa pre-paid card ambazo zimelipiwa tayari na makonda waelemishe maana ya hizo pre-paid cards,lakini bure itakuwa kuwavunjia heshima walimu mbele ya jamii na wanafunzi wao.
YAP. Niwazo zuri pia.Nadhani wapekuzi wanayafanyia kazi Bw. Julius
 
Hiyo siy
Shida ya walimu sio kusafiri bure sio nauli shida ya walimu ni maslai mishara mizuri sehemu Bora ya kufanyia kazi waboreshe shule vifaa kama kila shule ziwe Na maabara Na library wapewe na nyumba za kuishi hapo ndio atakuwa katatua shida za walimu askari wapewe mishara mizuri Na maslai Bora
o shida ya mwalimu wala askari.Hiyo ni shida ya watumishi tulio wengi.Jiulize wewe PS wanakuzidi mshaara? nao wanasafiri kutoka Kimbiji kwenda posta kutafuta riziki.Mimi nilipofundishwa LABOUR ECONOMICS nikagundua sina ajira ninatibu kiu tu hapa.Ilinibidi nihamie sehemu ambayo hata nitalima mahindi and I am doing well. Kwahiyo suala la mishaara haliwezi kutosha ndo maana kulia hakuishi. Kama umesoma UDSM kumbuka kila wanafunzi wakilalamika wanataka ela ya kujikimu iongezeke SIRIKALI Inaongeza na huduma kwenye kantini zinapanda. Angalia kila wakisema petroli na dizeli vimeshuka bei nauli haishuki wakati inapandishwa kwa kisingizio cha nishati hiyo kupanda bei katika soko la dunia. Hapa cha msingi ni udhibiti wa serikali katika maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom