1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,802
- 10,291
Vipi kuhusu askari
Akili yako haijapishana sana na ya Makonda au Makondakta.
Askari kinachowasaidia ni Uniform wanazovaa.
Na huko Dsm tu lakini baadhi ya mikoa wanalipa nauli hasa wanapokwenda mbali.
Askari akivua gwanda anadaiwa nauli kama kawaida na akimzingua konda basi ni vurumai nguo kuchanika.
Hili la walimu litakua gumu sana kutekelezeka kwani hata askari hawalipi nauli kisheria bali ni ile hali tu ta makondakta kuwaonea aibu na mara nyingine ni kama wanabebana. Yaani mfano trafiki na madereva ni watu wanaofanya kazi pamoja barabarani na kila mmoja ananafasi ya kumpa mwenzake unafuu kwa kumsidia kwenye utafutaji wake.
Askari anaweza akamsamehe dereva wa daladala aliyefanya kosa na hivyo dereva huyo kunusuru hela yake iliyokuwa itoke kama faini hivyo dereva huyo atakuwa na nafasi kubwa ya kumbeba akari bure akiwa na uniform au akiwa anamfahamu.
Kwa walimu ile ni siasa tu lakini ni ngumu mno kutekelezwa bila kutungiw sheria .
Cha msingi ni kuwawekea walimu wote posho maalum ya Usafiri ,maji,umeme na kodi ya nyumba. Pia wajengewe nyumba karibu na Shule.
Makonda angehamasisha ujenzi wa nyumba za walimu ili waishi karibu na shule zao.
Ikimbukwe kuwa Wamilikibwa daladala ni wafanyabiashara na makondakta nao wanataka posho za kuendesha maisha yao ambayo ni duni sana.
Makonda aishawishi serikali yake iwalipe walimu posho usafiri ili kuwajengea heshma zaidi walimu na sio kuwaombea lift kwenye magari ya watu.