Wale wagombanao ndio Wapatanao

Wale wagombanao ndio Wapatanao

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Muwazima wanamod wenzangu humu ndani? Mnaendeleaje

Ni siku ingine ya Blue Monday iliyojaa uchovu kwa wote waliokuwa katika pilikapilika za weekend,
na mihangaiko ya utafutaji wa shiilingi ktk kila kona ya mji.

Mwenzenu leo nimeonelea niwajie kwa jambo moja ambalo limekuwa na maswali mengi sana juu ya kichwa changu,
hasa hiyo mada hapo juu niliyotoa, nimeshindwa kuwaelewa wanadamu kwa vile walivyo, wengi wao wamekuwa
watu wa ajabu sana tena sana, Mtu anaamua tu kugombana na mwenzie ukiangalia wanachogombania ni kitu
cha kijinga sana hata ukitaka kuuliza watakwambia ameazima kiatu changu huu ni mwaka wa 3 na hataki kunipa
Sasa wewe ndugu yangu kiatu cha watu kwanini hutaki kumlejeshea unabaki nacho, atakwambia kuwa kiliharibika
au sina nishakitupa jalalani, kitu sio chako umekiazima kwanini usikirudishe kwa mwenyewe, unakaa nacho mpaka kinabaribika, kwanini jamani unakuwa una hata utu jamani?

Wengine humuhumu ndani ya JF CC wanaanza kugombana tu hovyo pasipo msingi wowote ukiuliza ni maandishi tu yaliteleza kidogo, mtu anawaka utafikiri gesi ya mtwara jamani. kwa hapa sitaki kueleza zaidi wenyewe mwafahamu
mpaka yapelekea kutokuwa na urafiki tena na mwananajf mwenzio. Jamani tuache tabia ya ugomvi humu ndani.tupendane na tuchukuliane na kujaliana huo ndio urafiki wa kweli.

Wengine hasa akina dada wenzangu walioko mahome utakuta mtu anagombana na mwenzio na kumporomoshea lugha zisizopendeza kisa eti kachukua mume wake, hii yote yatokana na nini jamani, kwanini tusipendane na kwanini tunachukiana kiasi hicho. Tabia ya ugomvi sio njema. Na makaka nao wanaugomvi wa kichinichini tena hao hata
kuuana wanauana ovyo utafikiri wamekazwa. Acheni jamani tabia hiyo haimpendezi Mungu kabisa.

Katika Nchi na Mataifa mengi yameingia katika ugomvi ambao unakuwa mkubwa na kuleta mapigano ya wenyewe kwa wenyewe (civil war) ambayo yanapelekea mauaji ya kutisha, unyama usioelezeka, njaa isiyoneneka, uharibifu wa maliasili, magonjwa, na hata kuleta chuki isiyoweza pimika.
Hivi kwanini jamani wanadamu tunakuwa hivi kwanini tusipendane jamani, mfano halisi ni nchi ya jirani hapo Kenya na hata hapa nchi kwetu napo hasa nyanda za juu kaskazini, Mwanza geita, na pwani pia tunakwenda wapi jamani kwanini tunagombana na kupigana hata kuuana? NINI KIPO NYUMA YA PAZIA LETU HAPA TANZANIA?
na kwanini viongozi wanashindwa kufuatilia majanga yanapotokea? Kwanini tunakuwa watu tusiopendana
na kufurahiana?

Kwa kweli waungwana nimeshindwa kueleza kwani hapa machozi yananitoka hususani kwa Taifa letu TZ tunakwenda wapi jamani? furaha ya kujiita mm mtanzania sasa imetoweka, kutokana na vita hivi vya wenyewe kwa wenyewe, kwani wandugu marafiki zangu nyie hamuoni hili? Najua mnaliona basi ni vyema tumuombe Mungu atuepushe na mambo haya, tuwe watu wenye kujaliana, kupendana, kutakiana heri, na hata kuhurumiana kwani wale wagombanao ndio wapatanao.
Hebu tujifunze kumpenda / kuwapenda mwenzio / wenzio na sio kumchukia kwa kisa kidogo tu, hata kama amekukosea usimlipize kisasi, kwani kisasi ni cha Bwana muumba wako.
siku njema marafiki.

copy to: Erickb52, Mamndenyi, Filipo, Arushaone, my cousin charminglady, Ruttashobolwa, Madame B, watu8, passion lady, Bakulutu, Mentor, Jiwe Linaloishi, gfsonwin, na mpiganaji mwenzangu Smile

hebu angalia hapa:
 
Last edited by a moderator:
Sijui kama nimesoma nikaelewa vema!

Ugomvi wa cc ni wa ndoa
ndoa zinabuma hata honey moon haijaisha.

Ugomvi wa kitaifa labda kuleee kwenye lile jukwaa tata
ndo wanajua zaidi

copy Baba V
 
Mkwe naomba unisaidie kusoma halafu unieleweshe.. Samahani lakini.
 
Last edited by a moderator:
Sawa tutawacha ugomvi.. kwa masuala ya kuchinja yapo beyond chitchat tuwaachie jukwaa la stress.Na kwa kuanzia tu.
Smile nimekusamehe kiatu ulichonikopa..
Asprin zile 200 za nauli nilikuwa nakudai usinilipe.
Nicas Mtei na wewe nimekusamahe jelo
Jiwe Linaloishi nimefuta deni..
Kaizer na wewe liwalo na liwe..
Paloma kigauni changu cheupe cha white party ulikimwagia strawberry lips nimekusamehe..copy Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
mkwe summary hii hapa:

Wale wagombanao ndio Wapatanao

Ø Mtu anaamua tu kugombana na mwenzie ukiangalia wanachogombania ni kitu
cha kijinga sana

Ø Wengine humuhumu ndani ya JF CC wanaanza kugombana tu hovyo pasipo msingi wowote ukiuliza ni maandishi tu yaliteleza kidogo,

Ø Wengine hasa akina dada wenzangu walioko mahome utakuta mtu anagombana na mwenzio na kumporomoshea lugha zisizopendeza kisa eti kachukua mume wake

Ø Katika Nchi na Mataifa mengi yameingia katika ugomvi ambao unakuwa mkubwa na kuleta mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Ø Hivi kwanini jamani wanadamu tunakuwa hivi kwanini tusipendane jamani,

Ø Kwa kweli waungwana nimeshindwa kueleza kwani hapa machozi yananitoka hususani kwa Taifa letu TZ tunakwenda wapi jamani?

Ø Najua mnaliona basi ni vyema tumuombe Mungu atuepushe na mambo haya, tuwe watu wenye kujaliana, kupendana, kutakiana heri, na hata kuhurumiana kwani wale wagombanao ndio wapatanao.
Hebu tujifunze kumpenda / kuwapenda mwenzio / wenzio na sio kumchukia kwa kisa kidogo tu, hata kama amekukosea usimlipize kisasi, kwani kisasi ni cha Bwana muumba wako.

Mkwe naomba unisaidie kusoma halafu unieleweshe.. Samahani lakini.
 
kwani hujaeelewa kilichoandikwa na huyo Mamnyemi au waota ndoto za mchana wewe, ngoja nikusaidie kidogo ugomvi wa humu CC ni wakuhusu NDOA,(kwenye Ndoa watu wanachukuliana ovyo wake/waume zawatu humu na wale waliopangwa kwenye kamati hawatekelezi maagizo waliyopewa hususani Baba V.) KEJELI NA KUPONDA, MANENO YASIYOFAA nadhani hapo utaelewa kidogo
Mkwe naomba unisaidie kusoma halafu unieleweshe.. Samahani lakini.
 
Last edited by a moderator:
ladyfurahia
hivi unaamini kuwa humu namo kuna ndoa kweli?

Na kama zipo ni high blood pressure.

kwani hujaeelewa kilichoandikwa na huyo Mamnyemi au waota ndoto za mchana wewe, ngoja nikusaidie kidogo ugomvi wa humu CC ni wakuhusu NDOA,(kwenye Ndoa watu wanachukuliana ovyo wake/waume zawatu humu na wale waliopangwa kwenye kamati hawatekelezi maagizo waliyopewa hususani Baba V.) KEJELI NA KUPONDA, MANENO YASIYOFAA nadhani hapo utaelewa kidogo
 
Last edited by a moderator:
mkwe summary hii hapa:

Wale wagombanao ndio Wapatanao

Ø Mtu anaamua tu kugombana na mwenzie ukiangalia wanachogombania ni kitu
cha kijinga sana

Ø Wengine humuhumu ndani ya JF CC wanaanza kugombana tu hovyo pasipo msingi wowote ukiuliza ni maandishi tu yaliteleza kidogo,

Ø Wengine hasa akina dada wenzangu walioko mahome utakuta mtu anagombana na mwenzio na kumporomoshea lugha zisizopendeza kisa eti kachukua mume wake

Ø Katika Nchi na Mataifa mengi yameingia katika ugomvi ambao unakuwa mkubwa na kuleta mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Ø Hivi kwanini jamani wanadamu tunakuwa hivi kwanini tusipendane jamani,

Ø Kwa kweli waungwana nimeshindwa kueleza kwani hapa machozi yananitoka hususani kwa Taifa letu TZ tunakwenda wapi jamani?

Ø Najua mnaliona basi ni vyema tumuombe Mungu atuepushe na mambo haya, tuwe watu wenye kujaliana, kupendana, kutakiana heri, na hata kuhurumiana kwani wale wagombanao ndio wapatanao.
Hebu tujifunze kumpenda / kuwapenda mwenzio / wenzio na sio kumchukia kwa kisa kidogo tu, hata kama amekukosea usimlipize kisasi, kwani kisasi ni cha Bwana muumba wako.

ahsante sana Mkwe. Sasa nimeelewa.. Bahati nzuri ni kwamba katika moyo wangu na ubongo wangu hakuna kitufe cha ugomvi.
 
kwani hujaeelewa kilichoandikwa na huyo Mamnyemi au waota ndoto za mchana wewe, ngoja nikusaidie kidogo ugomvi wa humu CC ni wakuhusu NDOA,(kwenye Ndoa watu wanachukuliana ovyo wake/waume zawatu humu na wale waliopangwa kwenye kamati hawatekelezi maagizo waliyopewa hususani Baba V.) KEJELI NA KUPONDA, MANENO YASIYOFAA nadhani hapo utaelewa kidogo

Kumbe humu kuna ndoa? Na watu huwa wanagombana kwa sababu ya ndoa hzo?
 
Last edited by a moderator:
aisee wewe kweli ulikuwa una wadaiwa sugu hao wote uliwapa vitu vyako na wala hawakukurudishia jamani sio utu huo mrudishien mwenzenu vitu vyake hata wewe Nicas Mtei ulimkopa dada wa watu jamani, lakini amewasemehe hivyo ndivyo tunavyotakiwa kuishi sister Zion Daughter
Sawa tutawacha ugomvi.. kwa masuala ya kuchinja yapo beyond chitchat tuwaachie jukwaa la stress.Na kwa kuanzia tu.
Smile nimekusamehe kiatu ulichonikopa..
Asprin zile 200 za nauli nilikuwa nakudai usinilipe.
Nicas Mtei na wewe nimekusamahe jelo
Jiwe Linaloishi nimefuta deni..
Kaizer na wewe liwalo na liwe..
Paloma kigauni changu cheupe cha white party ulikimwagia strawberry lips nimekusamehe..copy Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Mamndenyi siwezi elezea kuwa ninaamini au siamini kama ndoa zipo lakini mbona wako waliooana kama Madame B na Chimbuvu au ni utani tu? namwingine ni Filipo, au nakosea mie mhm!lakini
Teh teh hao wameoana kwa kupitia katiba ya nchi ya chitchat chini ya Wakili muozeshaji Baba V .
Kwanza hebu tukuulize wewe na Mentor ndoa yenu ilipitia kwenye kamati ya Baba V au ni ya aina gani??Hebu tupe ushuhuda
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom