Guasa Ambonii
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 8,545
- 10,303
Swadakta maneno murua sana na ujumbe makhsusi kwa zama zile ukikumbuka. Ahsante sana mdau kwa kujazia nyama
Ninachokumbuka yule jamaa anaeonesha hio kila aki-slide anakwambia hapo ni Mecca sijui nini....jamaa alikuwa anajuaje kuwa ikitoka hii inakuja hii?Sikumbuki uzuri kama gharama zake za kuangalia ilikuwa senti hamsini (thumni )au shilingi moja aaah ilikuwa ndio fashion hiyo unapaona makka (mecca )nafsi yako ina burudika kabisa. Waqt sijui umekwenda wapi!
Weweeee umetisha nililetewa na baba mwa 1976 kutoka Zambia hiyo duu!!!? wewe mkali
hahahahahahaah, aiseeeMhenga mwenzetu mwaka 1976 nilikuwa ninakwenda nursery kwasababu ya uji wa bulgar ulioletwa kwa hisani ya watu wa Marekani
Wacha kabisa jamaa walikuwa wazuri wa kukariri walitukusanya sana waqt uleNinachokumbuka yule jamaa anaeonesha hio kila aki-slide anakwambia hapo ni Mecca sijui nini....jamaa alikuwa anajuaje kuwa ikitoka hii inakuja hii?
Kuna Jirani yetu mmoja henzi hizo alirudi toka ulaya ndo akaja na hiyo cinema, tulikuwa tunapangana nyumbani kwake kuangalia cinema kwa zamu zamu. ipo siku niliwahi foleni saa 12:30 Asbh nilifanikiwa kuona hiyo Cinema saa 10 Jioni.
Huyo Jirani ni mhaya design si akaanza kuleta uhaya wake eti akawa ajifanya mzungu kazoea ulaya, anatigisha kichwa kwa nyuma afu anafanya kama anarudisha nywele Nyuma kama mzungu kana kwamba nywele zinaziba macho.
Kweli [HASHTAG]#Tumetokambalipamoja[/HASHTAG]