Wakuu tupeni pole jamani

jamani namshukuru mungu kwa ulinzi wake wa kiungu mm na familia yangu na majirani zangu na wote tulio nusurika na janga la mabomu la gmboto. kifupi cjasimuliwa bali nilishuhudia na kunusurika yote haya yakitokea nilikuwa kama mita 100 hivi na nyumbani tunapata soda na jirani zangu gafla tukaanza kusikia milio ilikuwa tu poa tukasema majambazi yamevamia uko moshi bar hyo ilikuwa mida ya saa 2 pm kufika saa 2 na nusu yakaongezeka tukasema ni radi kuanzia hapo atukuitaji kuambiwa ni mabomu mana aielezeki nilichokumbuka akilini ni kukimbilia familia yangu nilipata tabu kwani ninakoeleke ndiko watu wanakotoka na mabomu ndio yameshamiri yanadondoka ovyo nikasema no mapaka nifike om kufika nikakuta awapo nikakimbilia kwa jirani nikauta wamekimbia wote hofu yangu ikawa kwa mtt wangu 5yrs ambaye alikuwa na msichana wangu kwa vile mabomu ndio yanashamiri kurindima ukweli ilifika mahali nikagivup maana ilikuwa toomuch nikalala tu chini unatimuliwa na vumbi vipande vinapiga kwenye mabati vishindo na mitikiso ya yaloanguka karibu kabisa jamani kweli mliosimuliwa ombeni hivyo hivyo ila msiombee yawakute ata mm naomba yasijetokea mna kwa masaa yote zaidi ya 3 si mchezo.

nashukuru mungu jana niliweza kumpata mtt na dada yake pamoja na mdogo wangu nimeshuhudia mabomu zaidi ya 10 na nimepiga picha baadhi yalotua kwenye maeneo yakwetu watu wameibiwa wamekimbia makazi yao watt wamepotea ni mengi yalotokea jana nilitamani sana kuwajuza wana jf mapema ila cm ziliisha chaji jana yote nzima nilikuwa na majukumu mengi ila leo nimeweza kuingia hewani nilikosa pole zenu asa kwa pearl kwani ndio mwana jf anayejua mpaka om kwa hilo nampa bun anless wana jf wamtetee.

Poleni sana na tunashukuru Mungu mmeokoka
 
pole sana mwathirka mwenzangu angalau nikiongea utaelewa namaanisha nn ebu niambie yale mabomu yaliyoaanza kulipuka mfulilizo mida ya saa 4 kama na nusu jamani ule mwanga ata kama umeangusha sindano chini unaiona live alafu yaliganda kama dk 20 na kitu mfulilizo acheni jamani yani kunguru ucku huo unamkwepa unafikiria ni bomu kumbe na yy anaokoa roho yake

ninadhani kwa watu wa gongolamboto na maeneo jirani Ijumaa ya leo kwa waislam, jumamosi ya kesho kwa wasabato na jumapili ya kesho kutwa kwa waabudio jumapili mahudhurio yao misikitini na makanisani yatakuwa mazuri mno!!!
 
mkuu kwa furaha nikichinja itabidi wana jf wote nile nao ck hyo bila hivyo ckubali

Ukichinja uchague aliyenona maana hiyo itakuwa ni sadaka. Pole sana ndio hivyo maana majibu yao nimeyasikia hii leo ni ya mzaha mzaha tu politiki hadi JWTZ.
 
Pole sana mpendwa na majirani zako. Mungu ni mwema azidi kuwatia nguvu. Najua adha ya vita/milipuko na displacement. Glory to GOD mu wazima
 
Pole sana mpendwa na majirani zako. Mungu ni mwema azidi kuwatia nguvu. Najua adha ya vita/milipuko na displacement. Glory to GOD mu wazima

thanks binamu fikiria hii aikuwa vita ni uzembe wa watunza ghala la silaha sizani kama kunalingine hapo
 
Ukichinja uchague aliyenona maana hiyo itakuwa ni sadaka. Pole sana ndio hivyo maana majibu yao nimeyasikia hii leo ni ya mzaha mzaha tu politiki hadi JWTZ.

kweli kabisa itabidi awe ngombe mana jf tupo wengi
 
ninadhani kwa watu wa gongolamboto na maeneo jirani Ijumaa ya leo kwa waislam, jumamosi ya kesho kwa wasabato na jumapili ya kesho kutwa kwa waabudio jumapili mahudhurio yao misikitini na makanisani yatakuwa mazuri mno!!!

no comment mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom