Uwiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!! Jamani TANESCO nimechokaaaa!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!! Jamani TANESCO nimechokaaaa!!!!!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Michael Amon, Apr 4, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Waswahili walisema kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho na sasa uvumilivu wangu kwa hawa watu wanaojiita TANESCO umefika mwisho sio siri TANESCO nasema mmenichoshana mambo yenu ya ajabu ajabu. Hivi majuzi militate taarifa kuwa mmeanzisha kamgao kenu ka umeme ka kimya kimya na tukawavumilia lakini safari hii siwezi kuwavumilia kwa Jezebel mlioufanya.

  Wana JF sio Kama nawaonea hawa jamaa ila kiukweqli wamenikera sana na huu uzembe wao uliopelekea kuleta hasara kubwa kwa wananchi. Tukio lenyewe lilikuwa Kama ifuatavyo:

  Jana majira ya saa tatu usiku ilitokea hitilafu ya umeme mtaani kwetu ambayo ilisababishwa na kuunganika kwa nyaya mbili za kusambaza umeme. Naambiwa tatizo hili lilianza mda mrefu likiwa kama fluctuation tu ya kuongezeka na kwa umeme kwa mara kwa mara na umeme kucheza cheza. Hawa jamaa walipotaarifiwa kuhusu hili tatizo hawakulitilia maanani na kuamua kulipotezea kana kwamba halikuwa na umhimu wowote.

  Uzembe wao huo. Ulisababisha maafa makubwa sana hadi kutufika hayo yaliyotufika. Hitilafu Ya kuongezeka kwa umeme zaidi ya volts 300, ulipelekea watu wote wa mtaani kwetu ambayo wapo katika line hayo ya umeme kuunguliwa na kila kifaa cha umeme ambacho kilikuwa on kwa wakati huo kuanzia bulb, TV radio, deki, subwoofer hadi mafriji. Kwa survey ambayo niliifanya jana hadi majira ya saa nne usiku haina kifaa chochote cha umeme ambacho kilikuwa on kwa wakati huo kilichosalimika na mpaka sasa ninvyoandika hii thread umeme bado haujarudi yaani hapa nimeandika hii thread kwa kutumia iPad ambayo ilikuwa na chaji kidogo.

  Hivi Jamani hii in haki kweli TANESCO kutufanyia hivi na kutusababishia hasara ambayo inatokana na uzembe wao? Nasema Mimi nimechoka, narudia tena nimechoka. nawafuata hawa TANESCO ofisini kwao. Leo watanitambua. Naenda kutandika viboko wote kuanzia meneja mpaka mlinzi ili waache uzembe wao. Kwa wale ambao wamechoshwa na huu upuuzi wa TANESCO tafadhali niungeni mkono ili tuukomeshe huu upuuzi wao.


  E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  pole, tanzania bila umeme inawezekana.....
   
 3. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nimesoma paragraph mbili tu zajuu lakn nimebaini ni kiasi gani wakerwa na kitendo husika, pole sana mkuu...
   
 4. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa.
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani ila sisi ndio tunaotaka kufanya iwezekane.
   
 6. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Yaani we acha tu. Hasa ukizingatia asilimia kubwa ya watanzania uchumi wao ni wa lipato cha chini. Sasa embu piga mahesabu mtu kajipinda kikweli kweli kanunua TV, friji na deki yake halafu vinakuja kuungua sababu ya uzembe wa watu flani. Inauma sana mkuu.
   
 7. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Na wewe unasupport?
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  sasa tufanyaje? Hatuna uwezo wa kuzalisha umeme....

  Mie mtaani nguzo zilikuwa zinagusana na kunatoa cheche toka mwanzo wa mwezi march nikawapigia simu tanesco, nimeishia kupewa namba eflu tano mia ngapi sijui na mpaka dakika hii hawajaja....

  Usiniulize tumesolve vipi tatizo..... Maana umeme ulikuwa unakatika viuno kama hauna akili nzuri.....
   
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Duh! Hii ni hatari mkuu maana hitilafu kama hiyo inaweza kusababisha vitu vyote vikaungua. Inabidi tuingilie kati hili swala mkuu maana wahenga samaki mkunje angali mbichi maana akikauka.......
   
 10. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Vp umeshawafata ofisini?
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Mimi tena nichelewe mkuu? Nimeshawaibuki mda mrefu.
   
 12. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kijana,siku nyingine rekebisha "uandikaji wako" wa kichwa cha habari... Unaandika utadhani umenaswa na huo umeme...!
   
 13. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Kwani kwenye heading nimeandika nimenaswa na umeme? Anyway thnx kwa ushauri.
   
 14. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Una lengo zuri la kunishukuru,lakini ushauri wangu,haujauelewa YM..

  Mbona ungeandika hiyo uwii... Ingeeleweka tu unachomaanisha?

  Neno moja, we unalirefusha..kwa maana ama faida ipi!

  Unaandika neno utadhani mtu aliyezoea "umbea" mkuu..
   
 15. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Wakati ule mzuka ulikuwa umenipanda mkuu ndio maana nikairefusha hivyo.
   
 16. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Kwani mtaani kwenu hakuna VISHOKA?!
  MP.
   
 17. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Vishoka halafu uje ulipishwe fine. SHida yote hiyo ya nini?
   
 18. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu weka Voltage regulator au stabilizer, funga circuit breaker (0.03mAMPs) electrical appliances zako zitasalimika.
   
 19. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Stabilizer ninayo lakini hiyo fluctuation ilikuwa ni ya haraka sana kiasi cha stabilizer kuchelewa kufanya kazi yake.
   
 20. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Poa na pole..

  Ila weka stabilizer zile za sh 70,000/- ndiyo za ukweli nadhani... Amps ngapi omba ushauri..

  Ila jua havijafa kabisa..kwa hela ya ufundi ndogo vinatengenezeka YM
   
Loading...