Wakuu, nazeeka vibaya

Wakuu, nazeeka vibaya

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
38,070
Reaction score
57,721
Kutokana na uzee wangu, watoto wangu wote walishaondoka nyumbani na wako kwenye miji yao wakijitegemea. Wengine wameoa na wengine wameolewa.

Changamoto iliyopo kwa hawa watoto, kwa sasa hawanijali kabisa ata kuthamini ule mchango wangu uliowafikisha hapo walipo, pamoja na kuwasomesha na kuwakuza hawa watoto.

Mama yao ndio amekuwa akifaidi matunda yao na mimi hawanithamini tena, kwa sasa mama atulii nyumbani, siku zote amekuwa ni mtu wa safari.

Leo ataenda kwa mtoto yule, kesho kwa yule n.k na kupelekea muda mwingi kubaki mimi mwenyewe nyumbani nikiwa najipikilisha na huu uzee wangu.

Kutokana na mazingira ya kubaki mwenyewe nyumbani pamoja na uzee wangu, nimepata wazo la kuuza nyumba, mifugo na mashamba yangu, ili nipate hela nikasome ‘certificate’ kwenye vyuo mbalimbali ili kusogeza siku zangu za kuishi; kwa kukutana na vijana wa huko ambao watanipa kampani ili nisiwe mpweke na kufa kwa mawazo.

Nitakuwa nasoma kwa kujisajili vyuo mbalimbali, mwaka huu chuo hiki, mwaka kesho chuo kile n.k muhimu tu niwe bize, pia nipate kampani ya kuongea nao na kucheka.

Kwa miaka yangu hii 79 najua nikienda huko vyuoni nitapata amani zaidi kuliko kukaa hapa nyumbani mwenye nikiwa najipikilisha.
Yangu ndio hayo;au mna la kunishauri?

dz.jpg
 
Duuuh hapa sitii neno ongeza beki 3 km wawili hivi mmoja wa kukupikia chumbani mwingine wa kukupikia jikoni hela za pension si zinaingia kila mwisho wa mwezi au kwanini uteseke?
Wazo zuri sana hili, utakuwa umewaokoa wengi sana hapa jf kwa huu ushauri uliotukuka.
 
Kumbe uliwasaidia ili waje kukusaidia na sio kujenga kesho yao?...Watu weusi wataendelea kubaki nyuma sana katika Uchumi binafsi
Wanatakiwa waje waniokoe muda huu kama mimi nilivyo waokoa wakiwa wadogo.
 
79 yrs Mungu kakupa neema kubwa sana. Life expetation ni miaka70. Tayari una bonus ya 9.
Anza kutengeneza urafiki na kifo. Huna haja ya kurudi darasani. Zaidi kuwa mtu wa ibada na kusali sana.
Je maradhi ya watu wazima hayajakuandama? Pressure, kisukari, mgongo, kiuno, nk
 
Back
Top Bottom