Ni dua yangu siku zote za Maisha yangu

Ni dua yangu siku zote za Maisha yangu

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
384
Reaction score
758
Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.

Yoshua 24:15

Kwa hiyo, Mimi pamoja na Nyumba yangu leo tarehe 27 julai 2026 tutamtumia Mungu aliye hai Yesu Kristo wa Nazareti aliye hai

Sijapigana vita na dhambi hadi kumwaga damu? Ila kiu yangu na dua yangu siku zote za maisha yangu nikiwa hai au nikiwa nimekufa

Ni dua yangu na maombi yangu Yesu Kristo wa Nazareti haijalishi dhambi itanisonga kiasi gani , haijalishi kizazi changu kitaenda mbali na uso wako kiasi gani? Dua yangu na maombi yangu hasiwepo hata mmoja katika kiuno changu ambaye hatakosa mbingu

Bwana wangu na Mungu wangu , ni maombi yangu rehema zako zisizokoma na huruma zako kwa wanadamu sizikome juu ya kizazi changu , rehema zako ulizomwonesha Mfalme Daudi , Mfalme Ahabu, Musa Mtumishi wako, na wote ambao wameandikwa katika biblia zisikome juu yangu na familia yangu.

Pendo lako lililo onekana pale msalabani kwa yule mwizi lisitupite watoto wako

Ile mbingu mpya ambao umetuaidi kwamba unakwenda kuandalia makao, ni dua yangu miongoni mwao watakao watakaoingia nyumbani kwako jina langu na ndugu zangu lisikosekane

Baba yangu na Mungu wangu hasiwepo hata mmoja katika ukoo wetu jina lake likakosekana katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo

Ni maombi yangu siku zote za maisha yangu nisije kuwa kama yule Tajiri na Lazaro mbele ya Ibrahimu, maombi yangu baba asiwepo hata mmoja kwenye kiuno changu hatakaye ikosa mbingu

Baba na Mungu wangu, wewe niko ambaye yuko, sawa sawa na neno lako nibora kupoteza kiungo kuliko kukosa mbingu, ni maombi yangu na dua yangu kiungo chochote kisitumike kuwa kikwazo cha mimi na nyumba yangu kuingia mbinguni, ni bora kuingia kilema kuliko kukosa mbingu yako

Baba itanifaa nini nikipata mali na hanasa za dunia lakini mwili wangu ukaishia jehanamu ya Moto

Maombi yangu na dua yangu jina langu na familia yangu lisikosekane katika kitabu cha uzima

Yesu wangu na Bwana wangu uhai wangu, roho yangu na mwili wangu na wa ndugu zangu navitoa vyote kwako siku zote za maisha yetu hapa duniani na mbinguni.

Kuishi kwangu siku zote kuwe ni Kristo na kufa kwangu kuwe ni Kristo, mwili wangu na nafsi yangu na roho yangu zibebe chapa ya Kristo siku zote za maisha yangu.Amen
 
Yeremia 9:24

Lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hii: kwamba ananifahamu na kunijua mimi, kwamba mimi ndimi BWANA, nitendaye wema, hukumu na haki duniani, kwa kuwa napendezwa na haya,” asema BWANA.
 
Yeremia 9:24

Lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hii: kwamba ananifahamu na kunijua mimi, kwamba mimi ndimi BWANA, nitendaye wema, hukumu na haki duniani, kwa kuwa napendezwa na haya,” asema BWANA.
Amina... !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom