Wakuu naombeni msaada wenu katika hili

Wakuu naombeni msaada wenu katika hili

Romanus js

Member
Joined
Jul 6, 2026
Posts
24
Reaction score
52
Nimekuwa nikifanya utafiti wa kina na maandalizi ya bidhaa moja ya kibunifu (innovative product) kwenye sekta ya vinywaji hapa nchini. Bidhaa hii inaleta suluhisho la kipekee sokoni na tayari nimeshaanza hatua za msingi za kisheria na usajili na mamlaka husika (TBS/TRA) ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda kwa viwango.


Kwa sasa, nipo hatua ya kutafuta washirika au mtaji ili kuingia sokoni kwa kishindo. Hivyo, natafuta fursa yoyote kati ya zifuatazo:


1. Ubia/Uwekezaji: Natafuta mtu au kampuni yenye mtaji na maono ya kibiashara anayependa kuwekeza kwenye miradi yenye tija. Ikiwa utakuwa na nia, tunaweza kukaa mezani na kuweka Mkataba wa Kutokufichua Siri (Non-Disclosure Agreement - NDA) ili nikupe maelezo kamili ya bidhaa hii, soko lake, na jinsi inavyofanya kazi kabla ya kuamua kuwekeza.


2. Fursa ya Kazi: Endapo mwekezaji hajatokea kwa haraka, niko tayari kufanya kazi ili nijipatie mtaji wangu mwenyewe na niweze kufanikisha lengo hili.

Sitatoa maelezo yoyote ya kina kuhusu bidhaa hii hapa hadharani ili kulinda wazo langu (IP). Hata hivyo, kwa yeyote mwenye nia ya dhati ya kushirikiana nami au mwenye taarifa za nafasi ya kazi, karibu tuwasiliane:
🙏🏻🙏🏻
 
Back
Top Bottom