Mpe na mama hongera zake bana usijichukulie wewe tuu maana kazi yake ilikuwa zio mchezo kulea mimba miezi tisa na kuingia kwenye kile chumba na kutoka sio mchezo mkuu Safety last
hongera sana sana baba, sasa majukumu yameongezeka, muombee akue, awe na afya njema na awe na nidhamu na hofu ya Mungu
Hongera sana.......msaidiane kufua nepi na nguo zake mtoto....
Hongera sana
hahahha mkuu itabidi nimfungulie huu upage ili azione pongezi kutoka kwenu.thank you again mkuu
hongera sana baba domi
Karibu kwenye ulimwengu wa kuwa baba mkuu na ujue majukumu yanaongezeka na sio kufurahia tuu kuja kwake ila ujue sasa budget yako unapanga na yeye pia
Hongereni sana baba na mama Dominick Safety last
Baraka za Mungu ziwe nawe na kwa Captain Dommy!! Faraja ya Salaama kwa Wife, Na mumlee/mumkuzee mwana (captain) kwa ushirikiano mmoja.AMINheshima mbele wajameni ,niko kwenye pozi la furaha baada ya wife kujifungua mtoto wangu wa kwanza ..baby Dominick...nimeona nishare nanyi huu wakati wa furaha na baraka.Nawatakia kila la heri wale wote wajawazito,Mungu awalinde mjifungue salama.
hahaha asante dada husninyo nawe mama nani.....?
Hongera sana!!!Na usimpe jina la utani mwekundu kama alivyosema julius mahinya maana ni moto wa kuotea mbali :smile-big:
Hongera sana sana,
Mpe mama Hongera sana sana,
Msalimie baby Dominick .......
hahaha, mie mama kijacho. lol
sawa.....!kitakuwa kijacho cha ngapi hiki....?
ni kweli mkuu majukumu hayaepukiki hata kumleta tu lilikuwa jukumu tunamshukuru mungu limeisha salama"ule msemo wa kuzaa si kazi kazi kulea " ndio unachukua nafasi yake kamanda...