Yanaweza kuwa ni maneno mageni miongoni mwetu hasa kwakuwa hayatumiki mara kwa mara au kwakuwa istilahi zake zinatumia maneno mengine
Wakushi ni aina ya watu au kabila ambao kiasili ni watumiaji wa bangi yani kwao bangi ni sehemu ya utamaduni wao mila na hata desturi! Kama wewe sio mkush usilazimishe wala usikubali kulazimishwa kuwa Mkushi
View attachment 408106
Towashi ni aina ya wanaume wasio na nguvu za kiume kabisa na wengine hawana uume kabisa
Kuna matowashi kwa kuzaliwa
Kuna matowashi wa kutengeneza(unakatwa uume)
Na kuna matowashi wa uamuzi binafsi
View attachment 408108
View attachment 408109
Siasa za Tanzania zimeingia kwenye duru mpya! Tunaunda kitu cha ajabu kweli kitu cha kuchekesha kitu cha kipuuzi hasa...kitu ambacho hata dunia nzima itatushangaa kama bado haitushangai
Tunajaribu kuua upinzani kwa gharama kubwa sana lakini kwa mbinu za kitoto kijinga na kipumbavu kabisa najiuliza tu hao Wapangaji wa hizo mbinu zinawa tosha kweli?
Unaua upinzani ili iweje? Mnajiandalia utawala wa milele? Kwa mbinu hizi?[emoji22] [emoji35] [emoji102] ?
Tunafisha na kuua ndoto nyingi za wanasiasa vijana wenye maono ya kuja kufanya mengi hapo mbeleni...tunachokiandaa ni matowashi wa kisiasa! Wanasiasa jina wanasiasa mavazi!
Kama ilivyo kwa matowashi halisi ni wanaume suruali wanaume sura lakini wasioweza kufanya chochote
Tunachokiandaa ni wanasiasa Wakushi wa kutengeneza! Wanachojua ni moshi , wape moshi na wakishapata stimu watafanya utakavyo wewe....utawapeleka utakavyo! Malengo yako yatatimia utapata unachokitaka lakini kumbuka na madhara pia utakayoacha nyuma na huko mbeleni
Kuna umuhimu mkubwa wa kujitafakari upya fanyeni vitu huku mkikumbuka kuna kesho na taifa linahitaji nguvu ya kila mmoja wetu..vitu vya kupita kama madaraka ya kisiasa yasiwatoe ufahamu kiasi hiki mkatumia mabilioni kuua upinzani huku tukiwa na vipaumbele muhimu kabisa
Tengeneni Wakushi na matowashi lakini kumbekeni msiba huu ni wetu sote na tanga tutalianua wote hata kabla ya kulala[emoji35] [emoji83] [emoji84] [emoji35] [emoji83] [emoji84] [emoji35] [emoji83] [emoji84]