Amasa popote ulipo nakukumbuka sana, nakupenda sana hata wewe hilo unalijua. Nilipendwa na wasichana wengi enzi zile lakini hawakuwa na mapenzi ya kweli labda walikuwa wanataka kuwa na Mimi ili wajipatie umaarufu kwa kutembea na H.boy na hiki ndicho kilifanya wakuchukie sana.
Lakini siku zote tulipendana sana na kweli tulishinda vishawishi.
Siwezi kuwalaumu wazazi wako kwa kukuhamisha na kukupeleka mbali na Mimi kwasababu labda ilikuwa ni njia ya wewe kupata mafanikio zaidi.
Machozi yako siku ulipokuwa unaondoka bado yananiumiza hadi leo nikiyakumbuka.
Naweza kuwa na mwanamke yoyote lakini wewe ni wapekee kabisa moyoni mwangu.
Ulipo hamishwa kwenda UK nilibaki mpweke sana lakini namshukuru Mungu nilimaliza na kwa sasa nina maisha yangu mazuri tu.
Mungu akutangulie huko uliko ila penzi la kweli kamwe halifutiki, naamini ipo siku tutaonana.
Mimi ni yule yule D wako.