Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Messages
5,473
Points
1,225

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2009
5,473 1,225
Wandugu,

Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.

Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;

" Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."

Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.

Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;

" Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....

Ni hayo tu kwa leo, je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini?
 

SheriaE

Senior Member
Joined
Aug 22, 2018
Messages
125
Points
225

SheriaE

Senior Member
Joined Aug 22, 2018
125 225
Nakumbuka Siku Moja Ticha Wa Hisabati Aliingia Clasi Akawa Anauliza Maswali Ukikosa Unakupga Fimbo. Alihakisha Kila Mtu Lazima Ampige. Me Nilikuwa Najifanya Najua Sana Bwana Si Yalinikuta Makubwa Baada Ya Kuniuliza Maswali Mengi Hatimaye Nikakosa, Nami Nkala Vyangu
 

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Messages
2,344
Points
2,000

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2018
2,344 2,000

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Messages
2,344
Points
2,000

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2018
2,344 2,000
Nakumbuka nilipofika la saba shule ikakumbwa na dhoruba ya kubakiwa na walimu wa kike tupu,wa kiume karibu wote wakapata majanga
Mmoja alipata ajali ya bike akapoteza fahamu miezi 4
Watatu wakaswekwa rumande kwa kuvujisha mtihani
Watatu walikuwa masomoni

Basi kilichofuata baada ya hapo hadi mwalimu wa nursery akapewa somokufundisha la saba,shughuli ikawa kwa mwalimu wa hesabu kila akishusha namba zinagoma basi akaona isiwe shida akanikabidhi darasa nikawa mwalimu wa hesabu mwanafunzi ila mshahara anakula yy

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Iyegu

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Messages
6,289
Points
2,000

Iyegu

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2014
6,289 2,000
Nakumbuka nilipofika la saba shule ikakumbwa na dhoruba ya kubakiwa na walimu wa kike tupu,wa kiume karibu wote wakaa somokufundisha la saba,shughuli ikawa kwa mwalimu wa hesabu kila akishusha namba zinagoma basi akaona isiwe sqhida akanikabidhi darasa nikawa mwalimu wa hesabu mwanafunzi ila mshahara anakula yy

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee
 

Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Messages
11,391
Points
2,000

Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2017
11,391 2,000

MAHENGE JR

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2014
Messages
475
Points
1,000

MAHENGE JR

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2014
475 1,000
Nilikuwa naweka maandazi kwenye kaptula ya shule na mchele wangu uliochanganywa na sukari+maji,maindi ya kuchoma na ya kukaanga hivyo darasa zima lilikuwa linanuka harufu ya maandazi na maindi alafu kukiwa na sherehe mtaani basi shule siendi na katika wanafunzi wachafu mimi nilikuwa no 1 hadi std 7 na nikapewa zawadi kwa kuwa kinara wa uchafu mpaka nahitimu....
 

Raynavero

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Messages
36,757
Points
2,000

Raynavero

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2014
36,757 2,000
ilikuwa tukimaliza masomo ya siku,ilikuwa ni darasa la pili miaka ya 80 tunapitia mashambani kwa watu kuiba machungwa ndizi etc, sasa tunalazimisha wasichana wakwee juu ili tuwachungulie chup** zao, mmoja wao one day akavua chu**pi akaiweka ndani ya mkoba ndo akakwea, huku anatamba mtangoja sana nyie!! mnataka mnichungulie chpi yangu leo hamuioni, kaacha duka wazi nasisi wala hatukuwa na hamu ya kuendelea kuchungulia kwani chpi ishavuliwa. daaahhh enzi za mwalimu bwana!
 

yna2

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2018
Messages
11,382
Points
2,000

yna2

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2018
11,382 2,000
Write your reply... Mimi na rafiki zangu tulikua na tabia ya kuiba mboga za shule tulizokua tunalima ...tukaona haitoshi tukan'goa zote

nakumbuka kuna rafiki rafiki angu alijinyea wakati anasubiri kusahihishiwa kazi na Mwalimu


kizuri kuliko vyote nilivyokua nawaburuza wasichana wenzangu..kwenye kumi bora msichana nilikuaga pekee hadi tunamaliza elimu ya msingi
 

Forum statistics

Threads 1,390,630
Members 528,220
Posts 34,057,002
Top