Wakumbuka nini enzi za Shule ya MSingi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakumbuka nini enzi za Shule ya MSingi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lucchese DeCavalcante, Jan 8, 2010.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wandugu,

  Thread hii ni mahususi kwa chochote unachokumbuka enzi unasoma shule ya msingi.

  Mimi binafsi nakumbuka enzi zile nasoma Issale primary school kule wilayani Mbulu miaka ya 1986-1991 wanafunzi tulikuwa nadhifu, tunaopenda shule, wenye heshima sana. Pia nakumbuka tulikuwa tunacheza halaiki shuleni na hata kwenye matukio kama ya mbio za Mwenge au Kiongozi wa kitaifa akitembelea wilaya yetu. Moja ya nyimbo za halaiki zinazonikuna mpaka leo ni hii hapa;

  " Chama chetu kilituongoza hadi uhuru tulipoupata na kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa... Mwenyekiti Mwl. Nyerere mwenye hekima na wingi wa Sifa Tanzania..."

  Ama kwa hakika enzi hizo zilikuwa tamu sana na tulipokuwa tukiimba nyimbo hizi tulikuwa tunanyoosha mkono kuelekea kwenye picha ya Baba wa Taifa wakati huo akiwa mwenyekiti wa chama na Raisi wa Tanzania.

  Pia nakumbuka kuna waalimu fulani ambo walikuwa wamepitia mafunzo wa JKT basi zamu zao zikifika wanapiga magwanda na wiki hiyo inakuwa mchaka mchaka sio mchezo. Bila kusahau kukimbia mchaka mchaka asubuhi au tukienda kuchota maji Lambo na madumu ya lita tano huku tukiimba nyimbo za uhamisishaji kama;

  " Mchaka mchaka chinja... Aliselema....na Mbuga za wanyama Tanzaniaaaah ya kwanza ni Serengetiii Ngorongoroooh Manyaraaa na Mikumiii oooh Tanzania hoooye....

  Ni hayo tu kwa leo je na wewe ulisoma shule gani ya msingi na wakumbuka nini???
   
 2. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mm kwakweli nakumbuka kuwekea watu vioo chini ili niwachungulie,pia nakumbuka siku ya usafi likuwa ni j3 na alhamisi nilikuwa nafua lesso ili kucha zing'ae
   
 3. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Tulikuwa tunapenda sana kuchezea maji na utelezi hasa mvua inponyesha tena bila viatu kama picha hii inavyoonyesha

  [​IMG]
   
 4. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Mambo ya kuimba halaiki daah inanikumbusha mbali sana...
   
 5. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Bila kusahau kuruka ukuta na kutokea dirishani hasa wakati wa kwenda kufagia viwanja na kunyeshea maua sie "wajanja" tulikuwa tunasepa

  [​IMG]
   
 6. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Shule zetu nyingi tulizosoma zilikuwa hivi na akili zilikuwemo leo hii mazingira mazuri na facility kwenye shule nyingi hasa za mjini zipo ila mitoto bomu bomu sijui tatizo ninini hasa au ndio hivyo tena nchi imeharibika na haina mwenyewe kuanzia chini hadi kwa wenye nchi???
  [​IMG]
   
 7. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tena Hapo unaongeza na kile kigeregere kikaliiiiii cha iyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu,iyuuuuuuuuuuuuu,alafu Hodi Hodi Twaingia!..................
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  umenikumbusha mbali saaana mkuu!YOU HAVE MY THANKS
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  nilikuwa mchelewaji afu muoga kupindukia!!! nilikuwa namtanguliza mlw mkuu mbele afu mimi ndo naingia shule kama waziri wa elimu!!! (as if mi ndo nilimwajiri)

  siku moja alinibamba akaniambia nimsubiri ofcn kwake...kama alinipata......
   
 10. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  najua nilikuwa dem mkali wakati wa kuwahi no always nachelewa lakin sikosi no
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  .......halafu ulikuwa mwoga sana kukoga...!unakaa hadi wiki nzima...!:D
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,032
  Likes Received: 23,781
  Trophy Points: 280
  Na ile ya kukojoa kitandani mbona huisemi wewe?
   
 13. bht

  bht JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hahaa ka ulikuwepo na kule kwetu baridi kama makambako....i used to do it once a week (aftarol si nilikuwa mtoto kwani nini mbaya?)
   
 14. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa nasubiri wakati wa mapumziko kukunua bagia,mabumunda,visheti na ubuyu,na iskirim alafu unatemea mate ili usiombwe
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  haaa nilikuwa nalowanisha kweli maza akaamua nisitumie vimiminika usiku!!!
   
 16. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,032
  Likes Received: 23,781
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi umekua? Mbona mwoga?
   
 17. bht

  bht JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hahaaaa hivi wewe nani kakuamsha leo lakini!!!!!!!!!!!!!!! aaaaaaaaaaah mule mule tuuuu LOL!!!!!!!! U ARE KILLING ME PEARL!!
   
 18. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  halafu umesahau ulikuwa unakaa msuchana peke yako kwenye dawati la wavulana
   
 19. bht

  bht JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Naogopa maji?????????? weeeeeeeeee hayakwepeki sasa!!
   
 20. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  alafu kwa sisi wasichana break unasubiri kucheza lede
   
Loading...