Wako wapi wanafunzi bora (Tanzania One) wa miaka ya nyuma?

Wana jamii huwa najiuliza sana toka nikiwa shule ya msingi nasikia tanzaniaa one form 4, 6 na hata vyuoni. Nikiwa udsm nilipata kujionea mtu mmoja aliyekuwa amenitangulia mwaka mmoja chuoni nikiwa nasoma degree program kama yake alikuwa udsm one . lakini toka nihitimu udsm huku mtaani siwaoni hawa vipaji wetu. nauliza huwa wanapotelea wapi?. au elimu yetu ni mbwembwe ya makaratasi tu?.
Wewe mwenyewe mbona hatukuoni au unataka maTO tuwe tunafufua watu?
 
Jamani lazima kujua kwamba elimu yetu inapima kwa mtihani wa mwisho tu, hiki kitu siyo sahihi maana inategemea sana mtu gani kalala na kuamukaje siku husika ya mtihani. Mie nadhani T.Os wa uhakika wanapatikana kwenye matokeo ya kuhitimu bachelor degree kwa maana ya inclusive results (coursework+UE). Mtu anayeweza kutoka ka 5, 4.9,4.8 au hata 4.7 huyu kweli anaouwezo katika fani husika. Kwa vile hawa hawatangazwi nje ya vyuo ndiyo maana hatuwajui na kuwafuatilia kwa karibu. Kwangu mie hawa ndiyo walistahili kuwa T.Os wa ukweli.
Kuna masomo ya kulala na kuamka, sasa wewe lala na kuamka na physics, math
 
Kuna mmoja tunae kazini, Ni kichwa balaa. Akiongea hata white people wanakaa kumsikiliza.
Mko shirika gani mkuu na hao whites pamoja na T.O mkuu nami nipate nafasi hata ya usafi wa kila Aina nipate tu Kodi ya meza kwa familia yangu
 
Kuna jamaa wakuitwa raymond kichwa sana huyu jamaa amepiga kibaha kama sikosei 2005 o level. Sijui yuko wapi anaejua jamani
 
Martin Chegere:

1. T. O Darasa la saba.
2. T. O Form 2 wastani wa 98.
3. T. O Form 4 Mau Seminary I-7.
4. T. O Form 6 Pugu Secondary (EGM) I-3.
5. T. O University / Degree UDSM GPA-4.9 (Economics & Statistics).
6. T. O University /Master's UDSM Economics GPA-5.
7. T. O University/PhD Gothenburg University

Yuko UDSM ana fundisha...
Hiyo namba saba hiki chuo kipo Tanzania? Au Thailand au Togo. Maana TO ni Tanzania One
 
LUSEKELO wa MZUMBE ni Noma yule jamaa,kwanza Baada ya kuongoza Alevel Science hope PCM,Alikwenda kusoma Mzumbe University BAF,Then kipindi yuko mwaka wa Pili akafanya CPA Akaongoza wa kwanza kwenye hiyo mitihani ya CPA.Jamaa yupo vizuri sana.....
Kuna Mtu Mwingine anaitwa MANGULA MICHAEL...Ni lecture Mzumbe university huyu jamaa ni Balaa,Alisoma Kantalamba PCB Akapata Division Two point 12.akafanikiwa kuingia chuo Mzumbe Miaka ya 2003.jamaa aliondoka na 4.9 GPA,Akaenda kusoma Udsm Masters ya Engineering akapata 4.8 GPA,Jamaa ni Nomaa...Yupo pale Mzumbe University anafundisha..Huwa anajiita Fast learner Au Son of Peasant.
Kantalamba hakujawahi kuwa na PCB tangu shule ianzishwe
 
Back
Top Bottom