Wakinadada ni wabahili jamani

Wakinadada ni wabahili jamani

Habari zenu wanajamii forum,

Leo ngoja niongee na kina dada na tabia zao za ubahili.

Yaani utakuta hata mpenzi wako anakuwa mgumu kukusaidia inapotoke shida fulani lakini wao ni wepesi sana kuomba kusaidiwa sijui hizo hela zenu mnapeleka wapi jamani.

Hii nimeishuhudia hata kwa kaka yangu mke wake ni mgumu sana inapofika mumewe kaishiwa.

Hata utakuta msichana mnapendana sana ila suala la kutoa ni wagumu hawa viumbe aisee yaani yupo radhi akuachie ulipie kodi nyumba,ulipie watoto ada na mahitaji mengine yeye anauchunaa mpaka ukute mmekabwa sana ndio utaona anajitoa tena kiubahili
.

Labda niwaulize hela zenu wakina dada huwa mnazipeleka wapi hata kusema baba ni kichwa cha familia muda mwingine jamani wanaume tunachoka sana tuwe tunasaidiana jamani sometimes.

Ni hayo tu, nawasilisha
Anaweza akawa mgumu kwako lakini kuna wakaka na wababa labda kazini kwao hata wakimtania kumuomba anawapa na hata hawadai.
 
Sio wanawake wote, kuna wanawake wanajitoa sana kifedha kusaidia waume zao.

Unajua muhimu ni upendo,na jinsi gani huyo mwanaume anakujali. Mnapokuwa na upendo kati yenu pesa haiwezi chukua nafasi.
Unajua mwanaume ukimpenda mkeo, ukimuheshimu na kujali mbona mwanamke atatoa tu pesa zake. Tena mtashirikiana vizuri kupanga bajeti.
 
Koh koh koh.... Mwanaume aliwekwa kumtunza mwanamke
Hapa ndo kwenye tatizo yani mabadiliko upande mmoja lakini upande mwingine dhambi,wanataka kuwa mapadri,wawe marais nk,usawa uwe kotekote.
 
Mpendwa unaongelea hilo kwenye u boyfriend girlfriend au kwenye ndoa?. Boyfriend simlei, akikwamaaa ntamtafutia sehemu amazing ya kukopa. Ila kwa mume wangu najiongeza mapema. Maisha magumu haya, sio wanaume wote ni kina Reginald Mengi kwamba wataafford each and everything on their own
 
hahahahahaha naona umemfikishia wife ujumbe kiaina....
 
Mpendwa unaongelea hilo kwenye u boyfriend girlfriend au kwenye ndoa?. Boyfriend simlei, akikwamaaa ntamtafutia sehemu amazing ya kukopa. Ila kwa mume wangu najiongeza mapema. Maisha magumu haya, sio wanaume wote ni kina Reginald Mengi kwamba wataafford each and everything on their own
sikuhizi wachache wanaolewa wakawe wamama wa nyumbani bali unaolewa ukawe msaidizi wengi wenu bado hamjajua au mnajifanya hamjui.
 
Sio wanawake wote, kuna wanawake wanajitoa sana kifedha kusaidia waume zao.

Unajua muhimu ni upendo,na jinsi gani huyo mwanaume anakujali. Mnapokuwa na upendo kati yenu pesa haiwezi chukua nafasi.
Unajua mwanaume ukimpenda mkeo, ukimuheshimu na kujali mbona mwanamke atatoa tu pesa zake. Tena mtashirikiana vizuri kupanga bajeti.

akika umenena unaonekana ni mke mwema kama hautajali niPM
H
 
sikuhizi wachache wanaolewa wakawe wamama wa nyumbani bali unaolewa ukawe msaidizi wengi wenu bado hamjajua au mnajifanya hamjui.
Teh tunajijua bana kuwa sisi ni wasaidizi. Sasa kila mtu ana definition yake ya neno "msaidizi"
 
Maisha siku izi yamebadilika wenye tabia hizi nao wabadilike maisha kusaidiana aiseee
 
Duuh!!! i wish nije kumpata mke asiye na aibu kama huyo ili nishangae vizuri..Yani unanipigia simu kwa tatizo ambalo liko ndani ya uwezo wako???..Ntakushangaa kwa kweli..Unless hiyo pesa ni tatizo kwako

Ukimaliza kunishangaa utume hela ya kodi
 
Mpendwa unaongelea hilo kwenye u boyfriend girlfriend au kwenye ndoa?. Boyfriend simlei, akikwamaaa ntamtafutia sehemu amazing ya kukopa. Ila kwa mume wangu najiongeza mapema. Maisha magumu haya, sio wanaume wote ni kina Reginald Mengi kwamba wataafford each and everything on their own

Good.Kuna wanawake jamani wana roho ngumu. anafanya kazi lakini ni wagumu hata matumizi ya kawaida hapo nyumbani kuhudumia.Cha msingi mi naona mnapoana ni kuwekana sawa swala zima la pato lenu.Kila mmoja aujue wajibu wake.
 
Habari zenu wanajamii forum,

Leo ngoja niongee na kina dada na tabia zao za ubahili.

Yaani utakuta hata mpenzi wako anakuwa mgumu kukusaidia inapotoke shida fulani lakini wao ni wepesi sana kuomba kusaidiwa sijui hizo hela zenu mnapeleka wapi jamani.

Hii nimeishuhudia hata kwa kaka yangu mke wake ni mgumu sana inapofika mumewe kaishiwa.

Hata utakuta msichana mnapendana sana ila suala la kutoa ni wagumu hawa viumbe aisee yaani yupo radhi akuachie ulipie kodi nyumba,ulipie watoto ada na mahitaji mengine yeye anauchunaa mpaka ukute mmekabwa sana ndio utaona anajitoa tena kiubahili
.

Labda niwaulize hela zenu wakina dada huwa mnazipeleka wapi hata kusema baba ni kichwa cha familia muda mwingine jamani wanaume tunachoka sana tuwe tunasaidiana jamani sometimes.

Ni hayo tu, nawasilisha

Ingekuwa vyema sana kama ungetumia neno BAADHI YA.....!!
Pole kwa kulamba garasa wadada wanaochangia majukumu kwenye familia wapo pia! Kama ilivyo kwa BAADHI ya wanaume wasiojua watoto wao wanakula nini, wanasomaje au wanavaa nini!!
 
Back
Top Bottom