Wakinadada ni wabahili jamani

Wakinadada ni wabahili jamani

...
Labda niwaulize hela zenu wakina dada huwa mnazipeleka wapi hata kusema baba ni kichwa cha familia muda mwingine jamani wanaume tunachoka sana tuwe tunasaidiana jamani sometimes.

Ni hayo tu, nawasilisha
Jibu:-
Zinaishia kwa kuwapa ndugu zao na wazazi wao, maana akinamama wengi wanaamini usemi usemao damu nzito kuliko maji
 
Hiki kizazi cha wanaume kimekua na tabia za ulalamishi kuliko hata kinadada wenyewe kha.
 
Tatizo linaanzia kwa wanaume. Mnajikakamua kwamba mna pesa na mtaweza kumtunza. Sasa akibania hela yake usilalamike. Kuna mambo yanatakiwa kuwekewa utaratibu tangu siku ya kwanza. Mojawapo ni kuhusu kipato na matumizi ya familia. Pesa ya baba na mama ni ya familia, inakaa kwenye POOL, kisha mna orodhesha mahitaji yenu kama familia.

Kwenye POOL mwanaume anaweza kuweka mshahara wake bila shida. Issue inakuja kwenye extra income.

Mwanamke akionyesha kuwa yuko open na pesa zake, ni rahisi kwa mwanaume ku declare extra income. Lakini akiwa bahili, kufichaficha au anatumia principle ya "chako chetu, changu ni changu" itakula kwake.
 
Mpendwa unaunga mkono kulipiwa kodi ya nyumba na ada????
Mpendwa mbona umeshangaa sana..Hiki kitu kigeni kwako?...Yani jinsi ulivyouliza ni kana kwamba jukumu la Ada ya watt na Kodi ni la Mzazi mmoja peke yake..Nwei inaweza kuwa hivyo kama hayo ndo makubaliano yenu

So unataka kuniambia Baba yuko safari na ww unatakiwa kulipa kodi utasubiri mpaka arudi?..Au ndo utalipa zen akirudi unamdai..Watt wanadaiwa Ada,utaruhusu wakae home kumsubiri baba yao arudi ilhali na we pesa unayo?

Dhana kubwa hapa ni kusaidiana..Kama wote mnafanya kazi na mnaingiza kipato kwa nn umuachie mume wako tu ndo afanye kila kitu..

Labda uniambie ww matumizi ya pesa ya mwanamke kwenye ndoa ni yapi na ya mwanaume ni yapi
 
Sio wote jamani.Mimi siwezi kusubiri mwanaume afanye kila kitu mwenyewe ndani, kwa sababu nampenda vyote vilivo ndani ya uwezo wangu(financially)huwa navitekeleza nisipo fanya ujue kweli sina hela.
Hayo ya ubahili labda kwenye courtship ndo yanakuwepo ila mtu ambae ni nyama katika nyama zangu siwezi kumfanyia ubahili.Letu lazima liwe moja.

Hongera kwa kuwa na moyo wa namna hiyo
kwani ni wachache sana huwa wanajitoa kimaso maso.
 
Mpendwa mbona umeshangaa sana..Hiki kitu kigeni kwako?...Yani jinsi ulivyouliza ni kana kwamba jukumu la Ada ya watt na Kodi ni la Mzazi mmoja peke yake..Nwei inaweza kuwa hivyo kama hayo ndo makubaliano yenu

So unataka kuniambia Baba yuko safari na ww unatakiwa kulipa kodi utasubiri mpaka arudi?..Au ndo utalipa zen akirudi unamdai..
Kodi sio emergency bana mpendwa kwamba imekuja bila taarifa unajua kabisa lini unatakiwa kulipa ukisafiri acha mbesa nyumbani au tarehe zikifika tuma mshiko
 
Teh teh..Mpendwa naona unachagua vitu vya kusoma kwenye biblia..Yani ndo umeamua kusoma hapo tu??

Nasoma vitu vingi na nnavifuata mpendwa, nimepewa kazi ya kuzaa kwa uchungu af nijiongezee tena na kula kwa jasho....hapana bana
 
Kodi sio emergency bana mpendwa kwamba imekuja bila taarifa unajua kabisa lini unatakiwa kulipa ukisafiri acha mbesa nyumbani au tarehe zikifika tuma mshiko
Duuh!!! i wish nije kumpata mke asiye na aibu kama huyo ili nishangae vizuri..Yani unanipigia simu kwa tatizo ambalo liko ndani ya uwezo wako???..Ntakushangaa kwa kweli..Unless hiyo pesa ni tatizo kwako
 
Nasoma vitu vingi na nnavifuata mpendwa, nimepewa kazi ya kuzaa kwa uchungu af nijiongezee tena na kula kwa jasho....hapana bana
Subiri, unaenda kazini either kwa kuajiriwa au kujiajiri?
 
Nasoma vitu vingi na nnavifuata mpendwa, nimepewa kazi ya kuzaa kwa uchungu af nijiongezee tena na kula kwa jasho....hapana bana
Teh teh..Mpendwa basi kasome na Mithali 31:10 na kuendelea zen uniambie kama umeambulia chochote
 
Back
Top Bottom