Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 25,443
- 46,198
Wakili wa kujitegemea Peter Madeleka, ameachiwa jioni ya leo, Agosti 17, 2026 bila masharti yoyote.
Akizungumza na NipasheDigital, kwa njia ya simu muda mfupi uliopita, Wakili na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, William Maduhu, amesema Madeleka ameachiwa bila masharti na kwamba hana tuhuma zinazomkabili.
“Ametolewa huru jioni hii bila masharti yoyote, hakuna kesi mahakamani, hakuna chochote,” amesema Wakili Maduhu.
Madeleka ameachiwa bila masharti baada ya mawakili kufuatilia dhamana yake katika Kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam, kuanzia asubuhi leo.
Madeleka, alikamatwa Ijumaa iliyopita kwa tuhuma za kudharau agizo la Mahakama.
Soma Pia:
Wakili Paul Kisabo, amesema mapema leo asubuhi alifika kituoni hapo akiwa na mawakili wenzake pamoja na baadhi ya ndugu wa Madeleka, na kuelekezwa warejee saa 8:00 mchana kwa ajili ya kumdhamini.
“ZCO amekubali tumdhamini, na tumemdhamini watu watatu. Mimi na ndugu zake wawili, lakini ZCO amesema hatamwachia sasa hivi wao kama jeshi la polisi watampeleka nyumbani kabla ya saa 6:00 usiku. Ndicho ambacho ZCO ametuambia ingawa kwa mujibu wa sheria, mtu akidhaminiwa muda huo inabidi atoke, anaondoka na wadhamini wake anaenda anakokwenda.
“Lakini yeye ametoa amri kwamba jeshi la polisi watampeleka nyumbani kabla ya saa 6:00 usiku wa leo. Bado tupo Central tunaendelea kufuatilia dhamana yake ingawa tayari tumeshajaza fomu tumemdhamini,” alisema Wakili Kisabo.
Madeleka alikamatwa na Polisi Ijumaa iliyopita kwa tuhuma za kudharau amri zilizotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Taarifa ya Kamanda Muliro Ijumaa Agosti 14, 2026 ilisema wakili Madeleka alikamatwa majira ya saa 9:30 alasiri katika eneo la Mikocheni B, Wilaya ya Kinondoni, kwa tuhumi za kukiuka na kudharau amri halali za mahakama zilizotolewa mnamo tarehe 27 Julai 2026 na tarehe 13 Agosti 2026.
Agizo la Mahakama lilitolewa na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, C. M.Tengwa, kupitia taarifa yake kwa umma, aliwataka mawakili wote kuzingatia Kanuni za Maadili ya Mawakili (Tangazo la Serikali Na. 118 cha mwaka 2018) pamoja na Ibara ya 30 (1) na (2)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

- Polisi: Madeleka tunamshikilia kwa kudharau amri ya mahakama Kuu
- Malisa: Wakili Madeleka amekamatwa na watu waliojitambulisha ni polisi