WAKILI MAARUFU MADELEKA KUPEWA KESI YA UGAIDI ?

WAKILI MAARUFU MADELEKA KUPEWA KESI YA UGAIDI ?

Huu ugaidi unalazimishwa kila uchao, ipo siku utatokea kweli. Ni suala tu la muda. Inaonekana wanaupenda sana,huku madhara yake wakiwa hawayajui.
 
Kwa kile kinacho onekana kuendelea kukomoa raia yeyote anae enda kinyuma na usawa na haki , Mhimili wa Dola , Mahakama na Polisi wameamua kufungulia kesi za Ugaidi wote watakaoisema serikali ya Samia vibaya. Huku Jeshi la Polisi likiwa kinara kupin point anaefuata wa kupewa kesi ya Ugaidi jambo ambalo wananchi wanalichukia sana.
Kufuatia Mhadhili wa Chuo kikuu kubambikwa kesi ya Ugaidi akiwa anafundisha darasani hali iliyoleta sintofahamu na hofu kubwa kwa walimu wa chuo pia.
Tayari vijana kadhaa wamebambikwa kesi za Ugaidi na Waziri wa mambo ya ndani kasisitiza kua ni MAGAIDI na washughulikiwe.
Mtaani panaendelea kuwepo na wimbi la wananchi wenye hasira kali dhidi ya vyombo vya dola na watawala (maana hawa sio viongozi).
Je panaweza kuibua maandamano makubwa nchi nzima kushinikiza dola itende haki na isitumike kisiasa ?

Kesi za UGSIDI Tanzania kwa sasa zitakuwa ni nyingi kuliko za ujambazi.
 
Back
Top Bottom