Wakili aeleza walivyosota gerezani na mkewe miezi 18, waamua kudai fidia

Coaster2015

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
2,535
2,000
Hii nchi ina mambo mengi sana, unamuweka mtu ndani muda wote huo bila dhamana na huna uthibitisho wa makosa yake, hii ni zaidi ya ukatili, atlist hata wangemuacha nje kwa dhamana wakati uchunguzi unaendelea

Wamempotezea muda, malengo, wameyumbisha familia yake, wamesimamisha mambo yake mengi, bad enough wamemkamata na mke wake pia
Wa hivyo wako wengi sana kwenye hayo mahakama yao, ile serikali ya yule mwenda zake ndio ilikuwa kazi yake, walimbambika kesi kabendera wakamlazimisha alipe million 100 ili wamwachie, walikuwa wanatafuta hela kwa nguvu ili kujengea hayo mamiradi ambayo jana tumeambiwa na serikali kwamba yanaendeshwa kwa mikopo mikubwa ambayo kuilipa ni kazi sana, yaani unamshikilia mtu mahabusu halafu unakuja kuibuka kutoka porini unasema hamna nia ya kuendelea na kesi, wakati mnamshika hamkujua kwamba hamna nia na makesi yenu hayo ??
 
Neurologist

JF-Expert Member
Nov 5, 2020
519
1,000

Ukiwaza sana haya mambo yanaumiza, kama sheria inapindishwa namna hii na watu wanaona ni sawa tu, basi tunapoelekea ni pagumu mnoo
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,511
2,000
Mbona mgongano wa maslahi hapo upo wazi kabisa. Yaani mke anakuletea michongo direct kutoka jikoni afu unagoma hamna mgongano wa maslahi hapo. Japo napinga style walotumia kuwabambikia kesi ila mlitakiwa msome alama za nyakati...mmetesa watoto kwa ujinga wenu
 
GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,426
2,000
Screenshot_20210617-160336.png

Wakili Peter Madeleka na mkewe, Jamila Augustine Ilomo wameishitaki Serikali wakidai fidia ya mali kwa kukaa gerezani kama mahabusu kwa zaidi ya miezi 18 na baadaye kuachiwa buru baada ya makubaliano na DPP.

Katika kesi Na. 10 ya mwaka 2021 aliyoifungua katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Madeleka anadai fidia kwa kusababishiwa hasara na kushushiwa hadhi mbele ya jamii kwa kitendo cha kushitakiwa kwa tuhuma ambazo Serikali imeshindwa kuzithibitisha.

Kisa kilivyoanza
Akizungumza hivi karibuni na Mwananchi, Wakili Madeleka, aliyewahi kuwa ofisa wa Jeshi la Polisi mwenye cheo cha mkaguzi kabla ya kuacha kazi hiyo mwaka 2016, alisema kisa kilianza baada ya kuhamia jijini Arusha na kufungua ofisi yake ya uwakili.

“Niliamua kuhamia Arusha nikimfuata mke wangu aliyekuwa ofisa uhamiaji. Yeye pia alikuwa mwanasheria kitaaluma,” alisema.

Hata hivyo, anasema mambo yalianza kubadilika baada ya kazi yake ya uwakili kuanza kupata mafanikio.

“Mimi kazi yangu ni kwenda kuwatetea watu wenye matatizo ya kisheria, wakiwemo waliokamatwa na uhamiaji. Siwezi kuwakataa watu waliokamatwa na uhamiaji anakofanya kazi mke wangu.

“Kukawa na malalamiko kutoka Idara ya Uhamiaji wakisema kuna mgongano wa kimasilahi. Mimi nikawaeleza kuwa kuoana na ofisa wao si kosa kisheria,” alisema.

Baadaye malalamiko yalipozidi, anasema alimwandikia barua Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kumjulisha malalamiko hayo na kwamba hana hatia. Lakini anasema barua hiyo ilimgeuka.

“Nilipomwandikia barua hiyo Kamishna Jenerali mwaka 2017, hatua iliyofuata ikawa ni kuhamishwa kwa mke wangu kutoka Arusha kwenda Singida na familia yetu iliathirika.

“Mimi nikamwambia mke wangu aache kazi, wakati huo alikuwa na nyota tatu na amesomea sheria. Aliporudi tukaendelea na kazi zetu za uwakili,” anasema.

Kesi ndani ya kesi
Ilipofika Agosti 2, 2019 ikatokea kesi inayohusu idara ya uhamiaji ambayo pia alikwenda kutetea wateja wake.

“Kuna mtu alitoka Afrika Kusini, alikamatwa akiwa na visa feki za Tanzania. Agosti 11, 2019 mtu huyo akapelekwa mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa kamishna wa sheria wa uhamiaji. Mimi nikaenda kumtetea huyo kamishna baada ya kuombwa na ndugu zake,” anasema.

Alisema kitendo hicho kiliibua hasira ya uhamiaji na hapo mzozo mpya ukaanza.

“Kwa hiyo nilipokuwa katika harakati za kumtetea yule kamishna ndipo nilikamatwa mimi, mke wangu pamoja na wakili mmoja aliyekuwa kwenye ofisi yangu,” anasema.

Anasema wakati kesi ikiwa imetajwa mara mbili, polisi walikwenda kwenye nyumba aliyofikia Upanga na kumkamata.

“Siku hiyo hiyo, mke wangu aliyekuwa Arusha naye akakamatwa na yule wakili mwingine, wakasafirishwa kuja Dar es Salaam, tukaunganishwa kwenye hiyo kesi ya visa feki.”

Anasema walifikishwa mahakamani Agosti 25, 2019 wakihusishwa na utengenezaji wa visa feki na kosa la utakatishaji fedha.

“Ilikuwa kesi ya uhujumu uchumi Na. 81 ya mwaka 2019. Tukapelekwa gereza la Segerea ambako tulikaa miezi saba,” alisema.

Kuanzia Agosti 25, 2019 alisema walikuwa wanahudhuria mahakamani na kuambiwa upelelezi unaendelea hadi Mei 12, 2020 Serikali iliposema haina nia ya kuendelea na kesi hiyo, hivyo ikafutwa wakaachiwa huru.

“Wakati tunatoka mahakamani Kisutu tukijiandaa kwenda nyumbani, tukakamatwa tena na kuambiwa tuna kesi nyingine inayotukabili Arusha, hivyo tuko chini ya ulinzi, tukapelekwa Kituo cha Polisi Mburahati tukalala mpaka Mei 13, 2020 tukasafirishwa kwenda Arusha.”

Anasema wakiwa Arusha Mei 14, 2020 wakapelekwa mahakama ya Arusha wakituhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, hivyo baada ya kesi kutajwa wakapelekwa gereza la Kisongo ambako walikaa miezi 11 na siku 13.

Anasema huko nako kesi ilikuwa ikitajwa lakini haiendelei.

“Nilijaribu kumwandikia barua Jaji anayesikiliza kesi na hakimu kwa kuwa niliona kesi yenyewe ni ya kunikomoa tu, lakini walikuwa wakipiga chenga.”

Hata hivyo, anasema ilipofika Machi 30, 2021, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), (sasa Jaji Biswalo Mganga), alitembelea gereza la Kisongo na kumtafuta.

“Alisema siwezi kutoka gerezani mpaka tufanye makubaliano, vinginevyo, nitaozea huko gerezani,” anasema.

Alisema baada ya ujumbe huo, mwakilishi wa DPP Mkoa wa Arusha alimwandikia barua mkuu wa magereza mkoani humo akiwaarifu watuhumiwa wanaotaka kumaliza kesi kwa majadiliano na DPP waandike barua.

“Kwa hiyo na mimi nikaandika barua, lakini nikijua kwamba utaratibu anaoagiza wa plea bargain umekosewa.

“Mimi nikafanya hivyo, Nikapeleka hizo fedha zilikuwa Sh2 milioni kwenye akaunti ya DPP ya BoT. Aprili 27 mwaka huu nikaitwa mahakamani, DPP akasema ameshakubaliana na mimi, akaomba mahakama iniachie.”

Baada ya kutoka jela Madeleka na mkewe sasa wamefungua kesi wakitaka walipwe fidia na Serikali, japo anasema kiasi cha fidia hiyo kitaamuliwa na mahakama.

Kuhusu kesi ya pili, Madeleka anasema bado yuko mbioni kufungua nyingine kupinga mchakato wa plea bargain uliomfanya akiri kosa na kulipa Sh2 milioni.

“Kiutaratibu, plea bargain inatakiwa ifanywe na mwendesha mashtaka wa kesi husika, lakini DPP alitaka afuatwe Dodoma, halafu yeye ndiye ajadiliane na mtuhumiwa na fedha ziwekwe kwenye akaunti yake iliyoko Benki Kuu ya Tanzania.

“Kwa mujibu wa kanuni ya 21(3(a) ya kanuni za plea bargain zilizotiwa saini na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, zinasema anayetakiwa kulipwa fedha ni msajili wa hazina ambaye yuko chini ya Wizara ya Fedha,” alisema.

Anaitaja pia kanuni ya 23 inayosema; kama plea bargain itafanyika kinyume cha hapo kwa namna yoyote ile basi aliyefanya plea bargain anaweza kwenda mahakamani na hiyo hukumu itatenguliwa.

Source: Mwananchi
 
GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,426
2,000
Haya sasa kesi za uhujumu uchumi zinaanza kuleta sokomoko la wadai fidia
 
Jaluo_Nyeupe

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
2,513
2,000
Ukisoma vizuri kuna maelezo ameficha, inaonyesha wazi kulikuwa na mgongano wa kimaslahi kwa yeye kusimamia kesi za uhamiaji wakati mke wake yupo huko. Naunga mkono polisi kukamata watu kama hao wanaichafua sana nchi.
Na vipi kuhusu biashara. Je unaruhusiwa kufanya biashara kama mke/mume wako ni afisa wa kodi TRA?
 
Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
8,023
2,000
Mateso ya hali ya juu kumweka Mr & Mrs rumande kwa miezi 18 bila dhamana.
Na kosa lenyewe la kubambikwa!

Mama SSH jitenge na hii laana,wacha iende na ligasi ya Mwendazake.
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,819
2,000
Ukisoma vizuri kuna maelezo ameficha, inaonyesha wazi kulikuwa na mgongano wa kimaslahi kwa yeye kusimamia kesi za uhamiaji wakati mke wake yupo huko. Naunga mkono polisi kukamata watu kama hao wanaichafua sana nchi.
Acha hizo, Kwani si alihamishwa na baadaye akaamuwa kuacha kazi? Mgongano gani wa kimaslahi? Walibambikiwa kesi ili kuwakomoa. Tulia na utafakari ukiwa sober.
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
7,933
2,000
THURSDAY JUNE 17, 2021Dar es Salaam. Wakili Peter Madeleka na mkewe, Jamila Augustine Ilomo wameishitaki Serikali wakidai fidia ya mali kwa kukaa gerezani kama mahabusu kwa zaidi ya miezi 18 na baadaye kuachiwa buru baada ya makubaliano na DPP.

Katika kesi Na. 10 ya mwaka 2021 aliyoifungua katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Madeleka anadai fidia kwa kusababishiwa hasara na kushushiwa hadhi mbele ya jamii kwa kitendo cha kushitakiwa kwa tuhuma ambazo Serikali imeshindwa kuzithibitisha.

Kisa kilivyoanza

Akizungumza hivi karibuni na Mwananchi, Wakili Madeleka, aliyewahi kuwa ofisa wa Jeshi la Polisi mwenye cheo cha mkaguzi kabla ya kuacha kazi hiyo mwaka 2016, alisema kisa kilianza baada ya kuhamia jijini Arusha na kufungua ofisi yake ya uwakili.

“Niliamua kuhamia Arusha nikimfuata mke wangu aliyekuwa ofisa uhamiaji. Yeye pia alikuwa mwanasheria kitaaluma,” alisema.

Hata hivyo, anasema mambo yalianza kubadilika baada ya kazi yake ya uwakili kuanza kupata mafanikio.

“Mimi kazi yangu ni kwenda kuwatetea watu wenye matatizo ya kisheria, wakiwemo waliokamatwa na uhamiaji. Siwezi kuwakataa watu waliokamatwa na uhamiaji anakofanya kazi mke wangu.

“Kukawa na malalamiko kutoka Idara ya Uhamiaji wakisema kuna mgongano wa kimasilahi. Mimi nikawaeleza kuwa kuoana na ofisa wao si kosa kisheria,” alisema.

Baadaye malalamiko yalipozidi, anasema alimwandikia barua Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kumjulisha malalamiko hayo na kwamba hana hatia. Lakini anasema barua hiyo ilimgeuka.

“Nilipomwandikia barua hiyo Kamishna Jenerali mwaka 2017, hatua iliyofuata ikawa ni kuhamishwa kwa mke wangu kutoka Arusha kwenda Singida na familia yetu iliathirika.

“Mimi nikamwambia mke wangu aache kazi, wakati huo alikuwa na nyota tatu na amesomea sheria. Aliporudi tukaendelea na kazi zetu za uwakili,” anasema.

Kesi ndani ya kesi

Ilipofika Agosti 2, 2019 ikatokea kesi inayohusu idara ya uhamiaji ambayo pia alikwenda kutetea wateja wake.

“Kuna mtu alitoka Afrika Kusini, alikamatwa akiwa na visa feki za Tanzania. Agosti 11, 2019 mtu huyo akapelekwa mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa kamishna wa sheria wa uhamiaji. Mimi nikaenda kumtetea huyo kamishna baada ya kuombwa na ndugu zake,” anasema.

Alisema kitendo hicho kiliibua hasira ya uhamiaji na hapo mzozo mpya ukaanza.

“Kwa hiyo nilipokuwa katika harakati za kumtetea yule kamishna ndipo nilikamatwa mimi, mke wangu pamoja na wakili mmoja aliyekuwa kwenye ofisi yangu,” anasema.

Anasema wakati kesi ikiwa imetajwa mara mbili, polisi walikwenda kwenye nyumba aliyofikia Upanga na kumkamata.

“Siku hiyo hiyo, mke wangu aliyekuwa Arusha naye akakamatwa na yule wakili mwingine, wakasafirishwa kuja Dar es Salaam, tukaunganishwa kwenye hiyo kesi ya visa feki.”

Anasema walifikishwa mahakamani Agosti 25, 2019 wakihusishwa na utengenezaji wa visa feki na kosa la utakatishaji fedha.

“Ilikuwa kesi ya uhujumu uchumi Na. 81 ya mwaka 2019. Tukapelekwa gereza la Segerea ambako tulikaa miezi saba,” alisema.

Kuanzia Agosti 25, 2019 alisema walikuwa wanahudhuria mahakamani na kuambiwa upelelezi unaendelea hadi Mei 12, 2020 Serikali iliposema haina nia ya kuendelea na kesi hiyo, hivyo ikafutwa wakaachiwa huru.

“Wakati tunatoka mahakamani Kisutu tukijiandaa kwenda nyumbani, tukakamatwa tena na kuambiwa tuna kesi nyingine inayotukabili Arusha, hivyo tuko chini ya ulinzi, tukapelekwa Kituo cha Polisi Mburahati tukalala mpaka Mei 13, 2020 tukasafirishwa kwenda Arusha.”

Anasema wakiwa Arusha Mei 14, 2020 wakapelekwa mahakama ya Arusha wakituhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, hivyo baada ya kesi kutajwa wakapelekwa gereza la Kisongo ambako walikaa miezi 11 na siku 13.

Anasema huko nako kesi ilikuwa ikitajwa lakini haiendelei.

“Nilijaribu kumwandikia barua Jaji anayesikiliza kesi na hakimu kwa kuwa niliona kesi yenyewe ni ya kunikomoa tu, lakini walikuwa wakipiga chenga.”

Hata hivyo, anasema ilipofika Machi 30, 2021, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), (sasa Jaji Biswalo Mganga), alitembelea gereza la Kisongo na kumtafuta.

“Alisema siwezi kutoka gerezani mpaka tufanye makubaliano, vinginevyo, nitaozea huko gerezani,” anasema.

Alisema baada ya ujumbe huo, mwakilishi wa DPP Mkoa wa Arusha alimwandikia barua mkuu wa magereza mkoani humo akiwaarifu watuhumiwa wanaotaka kumaliza kesi kwa majadiliano na DPP waandike barua.

“Kwa hiyo na mimi nikaandika barua, lakini nikijua kwamba utaratibu anaoagiza wa plea bargain umekosewa.

“Mimi nikafanya hivyo, Nikapeleka hizo fedha zilikuwa Sh2 milioni kwenye akaunti ya DPP ya BoT. Aprili 27 mwaka huu nikaitwa mahakamani, DPP akasema ameshakubaliana na mimi, akaomba mahakama iniachie.”

Baada ya kutoka jela Madeleka na mkewe sasa wamefungua kesi wakitaka walipwe fidia na Serikali, japo anasema kiasi cha fidia hiyo kitaamuliwa na mahakama.

Kuhusu kesi ya pili, Madeleka anasema bado yuko mbioni kufungua nyingine kupinga mchakato wa plea bargain uliomfanya akiri kosa na kulipa Sh2 milioni.

“Kiutaratibu, plea bargain inatakiwa ifanywe na mwendesha mashtaka wa kesi husika, lakini DPP alitaka afuatwe Dodoma, halafu yeye ndiye ajadiliane na mtuhumiwa na fedha ziwekwe kwenye akaunti yake iliyoko Benki Kuu ya Tanzania.

“Kwa mujibu wa kanuni ya 21(3(a) ya kanuni za plea bargain zilizotiwa saini na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, zinasema anayetakiwa kulipwa fedha ni msajili wa hazina ambaye yuko chini ya Wizara ya Fedha,” alisema.

Anaitaja pia kanuni ya 23 inayosema; kama plea bargain itafanyika kinyume cha hapo kwa namna yoyote ile basi aliyefanya plea bargain anaweza kwenda mahakamani na hiyo hukumu itatenguliwa.

Chanzo: Mwananchi
Mi naona kama vipi wakurudishie 2m. zako halafu urudi rimandi na mkeo hadi kesi yako itakapoisha kihalali chini ya hukumu ya mahakama. Hii plea bargaining hata mimi siiungi mkono.
 
Kilwa94

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
2,226
2,000
Kwenye hii story nimejifunza upendo wa dhati kwa hawa wanandoa, nampa honngera sana huyo mama.

Pia nawapa hongera wote wawili ni risk takers hasa, kuacha kazi kirahisi tu kwa cheo cha mkaguzi wa polisi au nyota tatu wa uhamiaji sio jambo jepesi kikawaida.
Itakuwa maafisa vipenyo hao.
 
Cliffhanger

JF-Expert Member
May 22, 2018
720
1,000
Mateso ya hali ya juu kumweka Mr & Mrs rumande kwa miezi 18 bila dhamana.
Na kosa lenyewe la kubambikwa!

Mama SSH jitenge na hii laana,wacha iende na ligasi ya Mwendazake.
Hii nchi ndani ya miaka mitano iliyopita iligeuka pango la wanyang'anyi!
 
Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,884
2,000
Hapo jamaa kaamua tu kukomaa Ila

Inawezekanaje mtu unafanya kesi za uhamiaji na mkeo akiwa ofisa uhamiaji , mgongano wa kimaslahi upo wazi kabisa na ukute hapo alikua akimtumia mkewe kupiga madili uhamiaji.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
176,377
2,000
THURSDAY JUNE 17, 2021Dar es Salaam. Wakili Peter Madeleka na mkewe, Jamila Augustine Ilomo wameishitaki Serikali wakidai fidia ya mali kwa kukaa gerezani kama mahabusu kwa zaidi ya miezi 18 na baadaye kuachiwa buru baada ya makubaliano na DPP.

Katika kesi Na. 10 ya mwaka 2021 aliyoifungua katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Madeleka anadai fidia kwa kusababishiwa hasara na kushushiwa hadhi mbele ya jamii kwa kitendo cha kushitakiwa kwa tuhuma ambazo Serikali imeshindwa kuzithibitisha.

Kisa kilivyoanza

Akizungumza hivi karibuni na Mwananchi, Wakili Madeleka, aliyewahi kuwa ofisa wa Jeshi la Polisi mwenye cheo cha mkaguzi kabla ya kuacha kazi hiyo mwaka 2016, alisema kisa kilianza baada ya kuhamia jijini Arusha na kufungua ofisi yake ya uwakili.

“Niliamua kuhamia Arusha nikimfuata mke wangu aliyekuwa ofisa uhamiaji. Yeye pia alikuwa mwanasheria kitaaluma,” alisema.

Hata hivyo, anasema mambo yalianza kubadilika baada ya kazi yake ya uwakili kuanza kupata mafanikio.

“Mimi kazi yangu ni kwenda kuwatetea watu wenye matatizo ya kisheria, wakiwemo waliokamatwa na uhamiaji. Siwezi kuwakataa watu waliokamatwa na uhamiaji anakofanya kazi mke wangu.

“Kukawa na malalamiko kutoka Idara ya Uhamiaji wakisema kuna mgongano wa kimasilahi. Mimi nikawaeleza kuwa kuoana na ofisa wao si kosa kisheria,” alisema.

Baadaye malalamiko yalipozidi, anasema alimwandikia barua Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kumjulisha malalamiko hayo na kwamba hana hatia. Lakini anasema barua hiyo ilimgeuka.

“Nilipomwandikia barua hiyo Kamishna Jenerali mwaka 2017, hatua iliyofuata ikawa ni kuhamishwa kwa mke wangu kutoka Arusha kwenda Singida na familia yetu iliathirika.

“Mimi nikamwambia mke wangu aache kazi, wakati huo alikuwa na nyota tatu na amesomea sheria. Aliporudi tukaendelea na kazi zetu za uwakili,” anasema.

Kesi ndani ya kesi

Ilipofika Agosti 2, 2019 ikatokea kesi inayohusu idara ya uhamiaji ambayo pia alikwenda kutetea wateja wake.

“Kuna mtu alitoka Afrika Kusini, alikamatwa akiwa na visa feki za Tanzania. Agosti 11, 2019 mtu huyo akapelekwa mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa kamishna wa sheria wa uhamiaji. Mimi nikaenda kumtetea huyo kamishna baada ya kuombwa na ndugu zake,” anasema.

Alisema kitendo hicho kiliibua hasira ya uhamiaji na hapo mzozo mpya ukaanza.

“Kwa hiyo nilipokuwa katika harakati za kumtetea yule kamishna ndipo nilikamatwa mimi, mke wangu pamoja na wakili mmoja aliyekuwa kwenye ofisi yangu,” anasema.

Anasema wakati kesi ikiwa imetajwa mara mbili, polisi walikwenda kwenye nyumba aliyofikia Upanga na kumkamata.

“Siku hiyo hiyo, mke wangu aliyekuwa Arusha naye akakamatwa na yule wakili mwingine, wakasafirishwa kuja Dar es Salaam, tukaunganishwa kwenye hiyo kesi ya visa feki.”

Anasema walifikishwa mahakamani Agosti 25, 2019 wakihusishwa na utengenezaji wa visa feki na kosa la utakatishaji fedha.

“Ilikuwa kesi ya uhujumu uchumi Na. 81 ya mwaka 2019. Tukapelekwa gereza la Segerea ambako tulikaa miezi saba,” alisema.

Kuanzia Agosti 25, 2019 alisema walikuwa wanahudhuria mahakamani na kuambiwa upelelezi unaendelea hadi Mei 12, 2020 Serikali iliposema haina nia ya kuendelea na kesi hiyo, hivyo ikafutwa wakaachiwa huru.

“Wakati tunatoka mahakamani Kisutu tukijiandaa kwenda nyumbani, tukakamatwa tena na kuambiwa tuna kesi nyingine inayotukabili Arusha, hivyo tuko chini ya ulinzi, tukapelekwa Kituo cha Polisi Mburahati tukalala mpaka Mei 13, 2020 tukasafirishwa kwenda Arusha.”

Anasema wakiwa Arusha Mei 14, 2020 wakapelekwa mahakama ya Arusha wakituhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, hivyo baada ya kesi kutajwa wakapelekwa gereza la Kisongo ambako walikaa miezi 11 na siku 13.

Anasema huko nako kesi ilikuwa ikitajwa lakini haiendelei.

“Nilijaribu kumwandikia barua Jaji anayesikiliza kesi na hakimu kwa kuwa niliona kesi yenyewe ni ya kunikomoa tu, lakini walikuwa wakipiga chenga.”

Hata hivyo, anasema ilipofika Machi 30, 2021, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), (sasa Jaji Biswalo Mganga), alitembelea gereza la Kisongo na kumtafuta.

“Alisema siwezi kutoka gerezani mpaka tufanye makubaliano, vinginevyo, nitaozea huko gerezani,” anasema.

Alisema baada ya ujumbe huo, mwakilishi wa DPP Mkoa wa Arusha alimwandikia barua mkuu wa magereza mkoani humo akiwaarifu watuhumiwa wanaotaka kumaliza kesi kwa majadiliano na DPP waandike barua.

“Kwa hiyo na mimi nikaandika barua, lakini nikijua kwamba utaratibu anaoagiza wa plea bargain umekosewa.

“Mimi nikafanya hivyo, Nikapeleka hizo fedha zilikuwa Sh2 milioni kwenye akaunti ya DPP ya BoT. Aprili 27 mwaka huu nikaitwa mahakamani, DPP akasema ameshakubaliana na mimi, akaomba mahakama iniachie.”

Baada ya kutoka jela Madeleka na mkewe sasa wamefungua kesi wakitaka walipwe fidia na Serikali, japo anasema kiasi cha fidia hiyo kitaamuliwa na mahakama.

Kuhusu kesi ya pili, Madeleka anasema bado yuko mbioni kufungua nyingine kupinga mchakato wa plea bargain uliomfanya akiri kosa na kulipa Sh2 milioni.

“Kiutaratibu, plea bargain inatakiwa ifanywe na mwendesha mashtaka wa kesi husika, lakini DPP alitaka afuatwe Dodoma, halafu yeye ndiye ajadiliane na mtuhumiwa na fedha ziwekwe kwenye akaunti yake iliyoko Benki Kuu ya Tanzania.

“Kwa mujibu wa kanuni ya 21(3(a) ya kanuni za plea bargain zilizotiwa saini na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, zinasema anayetakiwa kulipwa fedha ni msajili wa hazina ambaye yuko chini ya Wizara ya Fedha,” alisema.

Anaitaja pia kanuni ya 23 inayosema; kama plea bargain itafanyika kinyume cha hapo kwa namna yoyote ile basi aliyefanya plea bargain anaweza kwenda mahakamani na hiyo hukumu itatenguliwa.

Chanzo: Mwananchi
Utawala wa sheria unarejea kwa kasi...wote waliofutiwa kesi kwa makubaliano na DPP wakiamua kudai fidia serikali itaumia kwa upuuzi wa punguani mmoja tuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
6,330

Katiba yetu ni mbovu sana kiasi cha kuruhusu kichaa kuwa rais na kuharibu kila kitu. Asante Mungu kwa upendo wako kwetu tumeuona
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom