Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,446
- 7,822
Mahakama Kuu iliwaamuru wafanyabiashara Albert Msando na Jacquelene Msando, kumlipa mfanyabiashara Bahati Mgonja anayemiliki kampuni ya Y&H Mgonja Enterprises, Sh175 milioni kama fidia ya biashara ya vinywaji.
Albert Msando, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, yeye na mkewe ndio wamiliki wa klabu maarufu ya The Don’s Lounge ya jijini Arusha.
Hata hivyo, Msando amesema atakata rufaa hukumu ya Mahakama Kuu, akisema mawakili wake wako katika mchakato wa kupinga hukumu hiyo, akitoa sababu mbili.
“Tutakata rufaa kwa hukumu hiyo. Hoja yangu ya kwanza ni kwamba biashara inayolalamikiwa ni kati ya Y&H Mgonja Enterprises na The Don’s Group Tanzania, mimi ni mwanahisa na mkurugenzi, kwa hiyo biashara sijafanya mimi, bali The Don,” amesema.
Pia, soma=> Wakili Msando na mkewe wachemka mahakamani, waamuriwa kulipa fidia ya milioni 175