Wakikutana Dar

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,401
1,604
Hii nayo ni sheeedar!!!!!!!

Utakuta watu walikuwa marafiki sana kipindi cha nyuma,wamesoma wote, wamecheza wote lakini kimbembe huja pale wakikutana Dar.

Hapa nazungumzia wale wenzangu na mie ambao Dar tumekuja tayari tumeshaota Ma..vuzi na ndevu. Yaani tumekuja na mbio za Mwenge au Gari la kabichi.

Yaani mtu mliyekuwa mnafahamiana vizuri kabisa, siku mnakutana nae mlimani city
either:

-Atakupita kama hakujui

-Kukuuliza kama nimeshawahi kukuona sehem ila sikumbuki ni wapi

-Anakuuliza hivi wewe sindio unaitwa Jumanne wakati anafahamu fika kuwa unaitwa Joshua
-nk.....nk....nk.....nk.....nk

SWALI LANGU: Kwanini hii situation hutokea watu wakikutana Dar tu?

Mbona tukikutana mikoa mingine huwa tunakumbukana vizuri tu? Au ndio uzuzu wa jiji?
 
Homeboy sio Dar tu hata maisha yanapobadilika kwa baadhi ya watu ambao mko sehemu moja tabia za hivyo hujitokeza kwa wale malimbukeni wala sitoshangaa kwa kuleta hoja yako hapa jukwaani, hujakosea ni kweli.

Na cha ajabu ukirekebisha shobo linaanza sasa muda wote mlikuwa wapi?

Namalizia hakuna lolote zaidi ya ulimbukeni yani huoni thamani ya mtu hadi awe na kitu
 
Kukimbiana kupo hasa kutegemea na hali ya kiuchumi wa mhusika kwa wakati huo....Ukikuta mmoja wapo hali yake sio nzuri halafu wakati huo yuko shule alikuwa matawi ya juu fulani...
 
Homeboy sio Dar tu hata maisha yanapobadilika kwa baadhi ya watu ambao mko sehemu moja tabia za hivyo hujitokeza kwa wale malimbukeni wala sitoshangaa kwa kuleta hoja yako hapa jukwaani, hujakosea ni kweli.

Na cha ajabu ukirekebisha shobo linaanza sasa muda wote mlikuwa wapi?

Namalizia hakuna lolote zaidi ya ulimbukeni yani huoni thamani ya mtu hadi awe na kitu

word!!!!
 
Kuna demu tulimaliza nae chuo juzi kati hapo,

Tulikutana ubungo sema ilikuwa kigiza fulani hivi

Ilikuwa ni shider, sijamaliza kumsalimia mwenzangu alishanipita hatua kama 5 hivi,

Niliishia kumpungia mkono tu
 
Kwa mwanamke inategemea, mara nyingi wanawake huwa hawakazii watu macho kama wako barabarani, yeye anajua kila mtu anamtazama hivyo anaconcentrate na mikogo, usimlaum sana bana wanawake ndivyo walivyo! Inatokea mara nyingi tu unaweza kuwa umekaa sehem, tena counter kabisa anakuja anaagiza kinywaji anatengenezewa anachukua...kama haujamshtua hawezi kukuona, hasa kukiwa na mwanga mdogo, msiwaseme dada zangu ni jinsi walivyo wala si kwamba amekudharau!
 
Sometimes its the other way round...mtu aliyechoka ndo anamkimbia yule aliye vizuri, kwa kuona aibu etc...Ilishawai kunitokea nilikutana mshikaji nilisomanae form 1 sasa anaendesha bajaji. Nikasimamisha akawa anakuja kwa karibu tulivyotiana machoni jamaa akarudi barabarani nikaambulia kivumbi tu
 
Nadhani hii hali huchagiwa na mambo mengi nikitazama Dunia na maisha yamebadilika sana, Upendo wa kweli umekwisha, Ugumu wa maisha, Ulimbukeni wa mjini, Kuogopa kuchekwa (kafulia), Time management, Kukwepa mizinga, nk
 
hili jiji la shida na raha kujuana mikoani huko tatizo mkuu unaweza ukamshtua hapohapo hacheleweshi anakulilia shida hiyo ndo tabia ambayo watu wengi huwa hawapendi.
 
bora mi nipo zangu huku! mbagala three color ninakaribia mwaka sijafika dar .........
 
Homeboy sio Dar tu hata maisha yanapobadilika kwa baadhi ya watu ambao mko sehemu moja tabia za hivyo hujitokeza kwa wale malimbukeni wala sitoshangaa kwa kuleta hoja yako hapa jukwaani, hujakosea ni kweli.

Na cha ajabu ukirekebisha shobo linaanza sasa muda wote mlikuwa wapi?

Namalizia hakuna lolote zaidi ya ulimbukeni yani huoni thamani ya mtu hadi awe na kitu

Yaaap,ni kweli kabisa nakuunga mkono mkuu,ni ushamba tuu huu,hakuna kingine.
 
1. Wapo ambao wanamajivuno na ulimbukeni wa jiji
2.Wapo ambao wanaogopa kupigana vibomu ( kukopana)
3.Wapo ambao wanahofia utawaharibia mahusiano yao mapya hivyo wanaona suluhisho ni kukupotezea.
4.Wapo ambao wanahisi utawang'ang'ania na maisha haya.

Nikikutana na mdada anajifanya kaka kama nakufananishaaa!!! namjibu hujakosea nakufahamu. akiuliza tulionana wapi namjibu pale ulipojamba darasani ukahama shule kwa aibu. Hahahahaaaa
 
Situation hii haitokei dar tu, ila kwa sababu ulienda dar kwa gari la kabichi unakuwa unajistukia tu. Yaani ukumbukwe wewe ni meya ama baba mwenye nyumba wangu? Ni sawa na katabia ka kuuliza mpiga simu nani mwenzangu, anaanza kulalama umedelete namba yangu. Khaa, kwani wewe zimamoto ama ambulance?
 
Hii nayo ni sheeedar!!!!!!!

Utakuta watu walikuwa marafiki sana kipindi cha nyuma,wamesoma wote, wamecheza wote lakini kimbembe huja pale wakikutana Dar.

Hapa nazungumzia wale wenzangu na mie ambao Dar tumekuja tayari tumeshaota Ma..vuzi na ndevu. Yaani tumekuja na mbio za Mwenge au Gari la kabichi.

Yaani mtu mliyekuwa mnafahamiana vizuri kabisa, siku mnakutana nae mlimani city
either:

-Atakupita kama hakujui

-Kukuuliza kama nimeshawahi kukuona sehem ila sikumbuki ni wapi

-Anakuuliza hivi wewe sindio unaitwa Jumanne wakati anafahamu fika kuwa unaitwa Joshua
-nk.....nk....nk.....nk.....nk

SWALI LANGU: Kwanini hii situation hutokea watu wakikutana Dar tu?

Mbona tukikutana mikoa mingine huwa tunakumbukana vizuri tu? Au ndio uzuzu wa jiji?

Hii nahisi iko maalum kwa nyie mliokuja Dar kwa "magari ya kabichi",hahaha...
 
Back
Top Bottom