Duh! Maajabu haya! Mi ni very critic against Kenya lakini kusema eti Tanzania ilikuwa imeiacha Kenya hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 ni uongo usio na maana hata kidogo. Baada ya Mwalimu kutangaza Azimio la Arusha na kujikita kwenye uchumi wa kijamaa; nchi yetu ilianza vizuri sana tena sana! Unfortunately, kati kati ya miaka ya 70 tukaanza kupata matatizo ambayo mengine yalikuwa beyond our control. Matatizo haya yakaja kupokewa na vita vya Uganda ambayo hatimae iliharibu kila kitu! Kwisha kwa vita vya Uganda kukopokewa na economic liberalization policy duniani kote ambayo Mwalimu hakuwa tayari kusujudu kwa Wazungu na kuwafanya wawe ndio wa kupanga nini sisi cha kufanya! Hadi Mwalimu anatoka, hali ilikuwa ngumu kweli kweli kiasi cha utawala wa Mwinyi kufikia kukopeshwa na Zimbabwe!Hujui ulisemalo. Fyi Tz ilikua imeiacha Kenya mbali hadi mwanzoni mwa 2000's ndio Kenya imeipiku Tz, hivyo hoja za sijui wakoloni hazina mashiko
Mwinyi alipoingia alichofanya ni kuachia milango kv nchi haikuwa na chochote! Before that, bidhaa yoyote ambayo ungeikuta madukani basi ingekuwa ni kutoka Kenya na nyingi zilikuwa zinaingizwa isivyo halali! Na hapa ndipo ulitokea msingi wa vita dhidi ya magendo na ulanguzi ambayo iliasisiwa na Sokoine!
Baada ya Mwinyi kuingia madarakani na kuruhusu bidhaa kumwagika sokoni, nafuu kwa mlaji ndo ikaanza kuonekana lakini hali ya uchumi bado iliendelea kuwa mbaya kiasi kwamba inflation ulifika hadi 20%+ na kugota! Savings on Interest Accounts nayo ilikuwa juu ile mbaya! Alipoingia Mkapa ndipo akaanza kuweka mambo sawa na kuanzia hapo ndipo tukaanza kuwa tishio kwa Kenya na sio kabla ya hapo!
Ambacho kilitokea kwa Kenya ni kwamba miaka ya mwisho ya Daniel arap Moi ukuaji wa uchumi wa Kenya ulishuka sana lakini hata hivyo si kwamba ulishuka na kuwa mbya kuliko Tanzania-- hiyo haijawahi kutokea ingawaje ipo njiani kutokea manake, kwa mfano kwenye sekta ya Utalii tushaanza kuwawashia indiketa!
Uchumi wa Kenya ulikuwa weak by the time reference to the past performance of their own economy na sio eti kwa kulinganisha na Tanzania or any East African country! Remember, hata wakati tunafungua milango yetu ya biashara, ni Wakenya ndio wali-dominate investment hapa Tanzania! Itoshe tu kusema kwamba, nayasema haya kwa uchungu na inda manake furaha yangu kila ni kuiponda Kenya huku post yangu ya mwisho ikiwa ni kuponda ujenzi wa new terminal pale Jomo Kenyatta! Lakini pale penye dhahuri iliyo bayana itakuwa ni ukosefu wa weledi kutoiweka dhahiri hiyo panapo sahili!