Wakenya wanatuacha mbaaali sana Watanzania, Kwanini?

msumeno

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2009
Posts
2,826
Reaction score
1,738
Mpka leo sijui ni kwanini sisi Watanzania tuko nyuma ya waKenya kwa maujanja sijajua naomba nanyi mnijuze hapa!!!!Mimi hapa nitatoa ushahidi kama kuna mtu atapinga basi apinge kwa ushahidi.

Wakenya wanaongoza kwa madiaspora tena waKenya wengi wako kwenye kazi za maana ughaibuni. Ukweli usemwe!!

1. Nimefika Dubai Airport, mweusi anaefanya Duty free karibia zote ni mKenya... Kiswahili analonga
2. Airlines maarufu nyimngi waKenya wako pale wengine kama ma Pilots na maairhostess, anaebisha atoe nae hoja yake!!! . Mfano shirika la ndege la Fly Dubai wakenya wako pale waTZ Ziiiii why!!!

3. UNHAS hili ni shirika la la ndege la WFP kwenye Humanitarian movement, nimefika South Sudan, WaKenya ndio ma airhostess na ma Pilot karibia wote!!!, nikasema labda hapa SSD pekee maana ni jirani... aaa wapi bwana niko hapa DRC, waKenya ndio marubani wa ndege Zote za UNHAS na ma airhostess wote .. wanalonga kiswahili na English, asie elewa kazi kwake mkenya yuko job bwana.... why not waTZ?

4. Service providers wengi kwenye Humanitarian movment ni wa Kenya...... South Sudan kwa mfano Internet service provider wakubwa wa Visat, na items nyingine wakenya alieyefika WAU ni shahidi ..... Hapa DRC nilipo provider Mkenya!!!!

5. Kwenye hizi ndege biskuti, karanga, korosho made in Kenya!!!!!! imagine hata chakula cha wakimbizi kinatoka Kenya mfano PPN na maziwa anaebisha amwage hija!!!

5. Siku moja niko kwenye warsha mara akasimama Field manager mmoja akiongea kifaransa kibovu bovu akichangia mada nikashawishika nimuulize asili yake kwenye ''pose cafe''kwa kifaransa changu cha ma---vi ma...vi akacheka na kuniambia wewe jombaa mimi nduguyo.... mimi mkenya toka wakati huo tukawa ndugu.... mkenya tena!!!!!. Baada ya hapo nikaja kugundua maboss wengi hapa kwenye nyanja ya Humanitarian iwe UN iwe wapi ni Wakenya .....

Sisi ukisikia mtu akaenda America basi kafuata kaka yake .... au dada yake aliolewa na mzungu... ukimwambia South Sudan au Afghanstan utasikia aaaaa wapi nikafeee? au ukishare hapa job opportunities wataku PM kukuulza kuhusu usalama utasikia '' aaa mkuu wanalipa lakini? natumaje maombi? wakati kila kitu kimejieleza kwenye tangazo ... mwisho kabisa ATAKUAMBIA LAKINI MKUU USALAMA VIPIi? ..... imagine hata waganda wametushinda pale Iraq-Najaf Airport kuna kampuni moja ya ulizi waganda watupu mpaka mademu waganda.

Hapa Goma tulikua waTZ w 4 tu mmoja katimka ni member humu JF japo siji ID yake, tumebaki wa 3 tu lakini wakenya wa kumwaga tena huko UN ndo wamejaa... Uzuri wa hawa jamaa wakiwa nje ya Kenya ni kiswahili tu wakiwa wao kwa wao au wakikutana na wa TZ.....

Msinielewe vibaya sina maana ya kujisifia niliko swampa ila siku moja niko Bar moja huko Cote d'ivoire Abidjan mara wakaaingia hawa jamaa ... wanalonga kiswahili nikajisogeza niwasikie maana walikua wakizungumzia siasa za nchi yao .... waKenya tena sikuona mTZ hata mmoja pale SHIDA Ni nini?

Ila kwa UN mission za kijeshi nasisi tuko safi

Jana nimekereka sana nikitoke BENI Rubani Mkenya... Msaidizi... Mkenya.... Airhostess Mkenya.... Karanga na biscukuti tulizopewa made in Kenya.... aaaaaa wajameni WHY??????

Tutoke waTZ uoga haufai... wengi wetu sasa ni wanasiasa kila mtu POLITIK why???
 
Kwani aliyekwambia kwamba TanZania ni mshindani wa Kenya ni nani?
 
Kuzubaa tumezubaa
kingereza nacho mtihani
kuchelewa ku embrace market economy
roho mbaya nayo inatuponza
tunashindana wenyewe kwa wenyewe badala ya kusaidiana
ndo maana tunasifika kwa uchawi

Magufuli nimesikia hataki wanajeshi waende nje kwa mission za kigeni
kama kweli basi hilo nalo tutapoteza

na hii sheria ya watumishi wote wa umma waombe vibali ikulu vya kusafiri
tegemea idadi zaidi kupungua...
tutazidi kuwa 'kienyeji zaidi'

Wakenya walitangulia....lakini na sisi tumezubaa
 
Sisi Watanzania kutoka Ukanda wa Pwani tangu hapo ni vilaza; tunachoweza ni madrasa! Ndugu mleta mada, unataka kusema hata wale Watanzania wa mikoa ya bara na mikoa ya Kaskazini wenye IQ kubwa nao hujawaona huko? Au ndo wao wanaendaga Uropa na Marekani kwa dada zao?! Mleta mada acha uongo wako bhana, hebu fanya tafiti zako vizuri! Goooosh! Kumbe umefanya utafiti kwenye makambi ya Wakimbizi... ndo maana! Hebu piga pande za IMF, World Bank, Wall Street, UNDP and in fact, kama shida yako ni kuona ma-hostess and pilots wa Kitanzania; stop searching for us kwenye mashine za kuruka angani... na badala yake tutafute kwenye airlines like Emirates, Qatar or at least British or Turkish Airlines!
 
Watanzania tuna shida hatuna dhiki. Bahati mbaya yetu ni kwamba tuna habati nzuri sana. Uwepesi wa maisha Tz umefanya akili za waTz kulala fofofo. Huu ugumu wa maisha tunaolalamika sio ugumu haswa nishida za kutatuka kwa akili ndogo ila tumezoa wepesi kila kitu tunaona ni mtihani.

Kenyans wanashida bana, wamepita vipindi vigumu ila wamejifunza Kucapitalize on shida hadi kutoboa. Kwenda nje ya nchi sio sifa muda wote ila wao wamelazimika kuwa nje wengi sababu ya dhiki ndani ya nchi yao, ilifika wakati kila mkenya anawaza kwenda Ulaya na hiyo ipo hadi Leo wakati mTz kwenda nje anajiuliza kufanya nini wakati anapata kila kitu home kwa mantiki hiyo uwiano wa wakenya nje na waTz hauwezi kufanana. Wamejifunza kutumia shida kama fursa na sasa wako mbali I got to give them that
 
Ni kweli, wakenya ni eastern/african cheap labour, wakenya kazi ya dola 2000 anaweza akafanya kwa dola 500, yeye anataka doo (pesa kwanza) na hachagui kazi kama sisi watanzania. Mwanzaoni lilifikiri kenya wanalipa mishahara vizuri sana kumbe la, serikalini wanalipwa kama watanzania tu, hata kwenye makampuni mishahara ni ileile kama ya tz, dola 500-2000, wengi wao wanapata net ya elfu 60, 70, 80, hadi laki ambayo ni mil 1-2 za kibongo. Sasa makampuni mengi/nchi nyingi wanapenda sana kuwatumia wakenya , na english ni mara chache sana wanatumia, muda mwingi wanapiga kiswahili, hata maofisini, utakuja anaongea ngeli kisela anashushia kiswahili, hawajali wanaongea kingeleza kizuri wala laa, sisi watanzania ni uoga na hatuko tayari kwenda nje kufanya kazi, english tuliyonato inatosha sema tunabaki kulalamika tu.Kingine, watanzania sisi tunatka leo tukifanya kazi kesho tuwe na nyumba, gari starehe ....... , hatutaki kukubali kuwa mafanikio ni safari ndefu over 10-20yrs. Tujiulize, kinachotufanya tusiende kenya kufundisha kiswahili nin? au kutangaza kwenye tv nin? , ukiwa kenya ukisema tu mimi ni mtz baada ya siku mbili utaona mkenya anakuambia sasa buda si uniangalizie kakzi huko kwenu hata kuendesha gari buda, na wakenya wengi sio tegemezi , ndo maana kila mtu anatafuta maisha kivyake, tz tumelemaa kwa sababu ya mambo haya sijui mjomba mara shangazi nini haya yanatulemaza. Lakini ukienda ukanda wa kusini mwa africa namibia ,botswana au SA kuna watz kibao ,tena wanamawe ya kutosha, lakini wengi wao wanapiga biashara. Ukiachia usubutu wa wakenya kufanya kazi yeyote , pia suala la ukabila nalo linachangia, kenya kuna usenge mmoja, ukikuta company boss ni mkikuyu ujue wafanya kazi 80% watakuwa ni kikuyu, ukikuta ni luo pia wote wwafanyakazi watakuwa luo, ukikuta kalenjini maana yake wafanyakazi wote ni kalenjini etc, sasa wao wenye inakuwa kazi ngumu kupeana kazi nchini kwao hivyo kukimbilia nchi nyingine, mimi nimefanya kazi zaidi miaka 6 kenya, hr ukimkuta ni kabila fulani utaona staff wote ni kabila hilo, hata akija mtu wa kabila tofauti anakuambia kabisa hapa nimeleta cv tu lakini najua sipati job, mfano angalia equity bank ile ya wakikuyu, hapo kabila lingine hata kupata loan ni issue, kwa tz au uganda hakuna hayo mambo hivyo watu wanaona ni easy kufanya kazi home. Ndo maana hii east africa sidhani kama mtz au mganda anaweza pata kazi easily kenya, maana wao kwa wao ni issue , labda liwe kampuni la wageni na upate kazi nje ya kenya na wakuambie ukareport kenya, lakini wao kwa tz au uganda inakuwa ni easy maana hatuna utamaduni wa kuangalia majina na kujua huyu ni kabila fulani bali ni qualification tu ya mtu . Mie naona serikali ya tz nayo inachangia, ilitakiwa serikali ianze kwenda nchi jirani kuwekeza ili ichukue watz kwenda kule kufanya kazi, leo hii ukiangalia NMB ipo tu tz, wameshindwa hata kwenda nchi jirani, ATCL imekufa, ndege moja, angalia nchi kubwa haina supermarket owned by government na ikatoka kwenda nchi jirani kuwekeza , ITV, na star tv wote wako busy tz.
 
Peleka upuuzi wako kama hizo nafasi ni za maana sana basi GDP yao ingekuwa twice yetu! Sio lazma kuwa kama wao kila nchi ina economic models zake. We inaelekea ushamba flani unakusumbua
 
Sisi Watanzania kutoka Ukanda wa Pwani tangu hapo ni vilaza; tunachoweza ni madrasa! Ndugu mleta mada, unataka kusema hata wale Watanzania wa mikoa ya bara na mikoa ya Kaskazini wenye IQ kubwa nao hujawaona huko? Au ndo wao wanaendaga Uropa na Marekani kwa dada zao?! Mleta mada acha uongo wako bhana, hebu fanya tafiti zako vizuri! Goooosh! Kumbe umefanya utafiti kwenye makambi ya Wakimbizi... ndo maana! Hebu piga pande za IMF, World Bank, Wall Street, UNDP and in fact, kama shida yako ni kuona ma-hostess and pilots wa Kitanzania; stop searching for us kwenye mashine za kuruka angani... na badala yake tutafute kwenye airlines like Emirates, Qatar or at least British or Turkish Airlines!

Mjinga mmoja. Kwani lazima utukane Madrasa? Shwaini weee. Mbona sisi wengine tumesoma Madrasa na naweza kukuajiri kama msafisha nyumba yangu. Kama huna la kuchangia usitukane watu. Shwaini tena.
 
Watanzania tuna shida hatuna dhiki. Bahati mbaya yetu ni kwamba tuna habati nzuri sana. Uwepesi wa maisha Tz umefanya akili za waTz kulala fofofo. Huu ugumu wa maisha tunaolalamika sio ugumu haswa nishida za kutatuka kwa akili ndogo ila tumezoa wepesi kila kitu tunaona ni mtihani.

Kenyans wanashida bana, wamepita vipindi vigumu ila wamejifunza Kucapitalize on shida hadi kutoboa. Kwenda nje ya nchi sio sifa muda wote ila wao wamelazimika kuwa nje wengi sababu ya dhiki ndani ya nchi yao, ilifika wakati kila mkenya anawaza kwenda Ulaya na hiyo ipo hadi Leo wakati mTz kwenda nje anajiuliza kufanya nini wakati anapata kila kitu home kwa mantiki hiyo uwiano wa wakenya nje na waTz hauwezi kufanana. Wamejifunza kutumia shida kama fursa na sasa wako mbali I got to give them that

ni kama Wa South Africa
hawawazi kabisa kwenda USA wala Europe
tena wao hata visas hawahitaji...lakini wao ni nchi yao tu ndo wanaipenda
 
Mjinga mmoja. Kwani lazima utukane Madrasa? Shwaini weee. Mbona sisi wengine tumesoma Madrasa na naweza kukuajiri kama msafisha nyumba yangu. Kama huna la kuchangia usitukane watu. Shwaini tena.
Badala ya kutoa matusi ungeishughulisha akili yako kuelewa nilichoandika!!
 
Hii ni mada nzuri, lakini najua kuna watu kwa sababu ya 'blind nationalism' au ubishi wa kipuuzi wataleta maudhui nyingine zisizo na mashiko au hata kumkashifu aliyeleta thread. Tatizo ni kuwa wengi wa wanaofanya hivyo hawajatoka nje na kwao Dar ni 'jiji'. Ni kama chura aliye ndani ya dimbwi anaona hiyo ndiyo dunia. Jaribu kumwambia kuna bahari pia.....atajibu g'waaaaaa!
Kwa kweli mleta mada suala kama hilo limenitafuna sana akili. Lakini hatimaye nikafikia nadharia hii:
Ukoloni, pamoja na ubaya wake, una mambo mengi mazuri. Tofauti kubwa baina ya Tanzania na nchi za Kenya na Uganda kwa kweli ni kwa sababu Mkoloni alitawala nchi hizo. Katika kesi ya Kenya, kwa kweli hakutaka hata kuondoka. Kumbuka sisi hatukutawaliwa kwa maana ya 'colonization' walikuja wazungu wachache tu kufanya admin ili kutimiza jukumu la Umoja wa Mataifa. Kenya, kama South Afrika, ilikusudiwa Wazungu waishi kama kwao, ingawaje sehemu Fulani. Hivyo, kilipoingia kipindi cha Uhuru Wakenya tayari walikuwa mbele sana. Kuwa mbele si kwa majengo na miundombinu tu, bali pia kwa 'mentality'. Kwa sababu ukikaa karibu na mtu aliyeendelea na wewe utaendelea. Ujamaa ukatuongezea mzizimo wa akili. Kwa maana watu wakawa tegemezi kwa serikali na hata ndugu. Hushangaa sana nchini Kenya, mtu akiwa amefanikiwa kifedha si aghalabu kuona ndugu 'wakimnonea' wakitarajia awasaidie kwa hili na lile. Tanzania tabia hii imeenea sana kiasi cha kuwarudisha nyuma hata wale waliondelea kidogo.
Pengine nimetoka kwenye maudhui kidogo, lakini kwa ujumla yote hayo yanafasiri kwa nini itatuchukua muda mrefu hata kuwakaribia Wakenya. Kweli, Tanzania ni tajiri kuliko Kenya na yumkini ikaweza siku moja kuwa na majengo na barabara nzuri kuliko Kenya, lakini maendeleo ya mtu itachukua muda mrefu sana.
Hata hapa unasoma kuna watu wanaona Wakenya kufanya kazi UAE au hapa na pale....ni kwa sababu ya shida, au dhiki! Hiyo ndiyo mentality ya Wabongo.
 
Kuna sehemu nyingi tu watanzania wapo, mfano china-guangzhou, matajiri wengi sana ni watanzania, botswana pia nilikutana na watanzania kibap, tena wengi wanafanya biashara, lakini wakenya wapo wamefungua shule za medium, zambia watz kibao, tena hadi waganga wa jadi wamejaa kutoka tz. Lakini lilishangaa mwaka 2008 aliletwa professor mkenya kuja china kufundisha kiswahili wachina ,nakumbuka yalikuwa maandalizi ya olympic, nilishangaa pamoja na uhusiano mzuri wa china -tanzania bado hawajui kama tunaongea kiswahili zaidi kuliko wakenya? na mkenya alivyo mjanja akawa ananiletea home yake ambayo ameanda kuwafundisha wachinese nimuangalizie kama iko sawa, hapo ndo nilijua wakenya wasanii.
 
Peleka upuuzi wako kama hizo nafasi ni za maana sana basi GDP yao ingekuwa twice yetu! Sio lazma kuwa kama wao kila nchi ina economic models zake. We inaelekea ushamba flani unakusumbua
Lakini Mkuu Geza mbona sisi tuna Madini, Mbuga za kutosha, Ardhi kubwa yenye rotuba, Ukanda mkubwa wa bahari, Mlima Mrefu Afrika, Makaa ya mawe, Uranium, Chuma lakini GDP yetu haiko twice as theirs???
 
Kuna sehemu nyingi tu watanzania wapo, mfano china-guangzhou, matajiri wengi sana ni watanzania, botswana pia nilikutana na watanzania kibap, tena wengi wanafanya biashara, lakini wakenya wapo wamefungua shule za medium, zambia watz kibao, tena hadi waganga wa jadi wamejaa kutoka tz. Lakini lilishangaa mwaka 2008 aliletwa professor mkenya kuja china kufundisha kiswahili wachina ,nakumbuka yalikuwa maandalizi ya olympic, nilishangaa pamoja na uhusiano mzuri wa china -tanzania bado hawajui kama tunaongea kiswahili zaidi kuliko wakenya? na mkenya alivyo mjanja akawa ananiletea home yake ambayo ameanda kuwafundisha wachinese nimuangalizie kama iko sawa, hapo ndo nilijua wakenya wasanii.
Hao matajiri wakubwa wa huko China ndio hawa wachuuzi wanaotuletea toilet papers, tissues, toothpicks na bidhaa zingine ambazo tulipaswa kuzitengeneza wenyewe hapa nyumbani... Kwa ufupi hawana msaada wowote kwenye uchumi wetu zaidi ya kujitajirisha wao wenyewe..
 
Badala ya kutoa matusi ungeishughulisha akili yako kuelewa nilichoandika!!

Ok. Wee unakashifu waliosoma Madrasa kama mimi , sasa nakutaka tuandike comment hapa kwa lugha za Kifaransa, kiingereza, Kitaliano na Kiarabu.... kama utaweza. Yaani unajiona una akili nyingi kuliko waliosoma Madrasa, kitu gani kinakupa ujeuri na dharau hiyo? Ni hatari kwa watu kama nyie mkipewa kompyuta mnajificha nyuma yake na kujifanya mmeelimika. Madrasa inatufundisha hata ukiwa na elimu namna gani ukumbuke " hamkupewa elimu ila kidogo tu" In fact, mtu mwenye elimu ya kweli huogopa kusema ana elimu kwa sababu kila unavyoendelea kusoma unakuta elimu ni bahari na huwezi kuimaliza. Mwenye elimu ya kweli yuko humble sio kama wewe. Ujue comment zako zinatuudhi sana na hustahiki kuheshimiwa.
 
Back
Top Bottom