Wakenya wanatuacha mbaaali sana Watanzania, Kwanini?

Wakenya wanatuacha mbaaali sana Watanzania, Kwanini?

Umeangalia upande mmoja wa shilingi. Hebu chemsha bongo kidogo na swali hili.Kama kwenu nyumba ni kubwa hata mkiwa mia mnatosha na chakula kinapatikana kwa urahisi na mwenzako kwao nyumba ndogo upatikanaji wa chakula mgumu unadhani kati ya wewe na jirani yako nani atatoka kwenda kwa watu kufanya kibarua? Pili jumlisha watu kama kina kazi walizokuwa wanafanya kina Muhongo ,Tibaijuka, Asha Rose Migiro Salim ahmed salim Mchechu huku Ughaibuni JIBU utalipata usiangalie ukubwa wa pua kupima makamasi.
 
Mpka leo sijui ni kwanini sisi Watanzania tuko nyuma ya waKenya kwa maujanja sijajua naomba nanyi mnijuze hapa!!!!Mimi hapa nitatoa ushahidi kama kuna mtu atapinga basi apinge kwa ushahidi.

Wakenya wanaongoza kwa madiaspora tena waKenya wengi wako kwenye kazi za maana ughaibuni. Ukweli usemwe!!

1. Nimefika Dubai Airport, mweusi anaefanya Duty free karibia zote ni mKenya... Kiswahili analonga
2. Airlines maarufu nyimngi waKenya wako pale wengine kama ma Pilots na maairhostess, anaebisha atoe nae hoja yake!!! . Mfano shirika la ndege la Fly Dubai wakenya wako pale waTZ Ziiiii why!!!

3. UNHAS hili ni shirika la la ndege la WFP kwenye Humanitarian movement, nimefika South Sudan, WaKenya ndio ma airhostess na ma Pilot karibia wote!!!, nikasema labda hapa SSD pekee maana ni jirani... aaa wapi bwana niko hapa DRC, waKenya ndio marubani wa ndege Zote za UNHAS na ma airhostess wote .. wanalonga kiswahili na English, asie elewa kazi kwake mkenya yuko job bwana.... why not waTZ?

4. Service providers wengi kwenye Humanitarian movment ni wa Kenya...... South Sudan kwa mfano Internet service provider wakubwa wa Visat, na items nyingine wakenya alieyefika WAU ni shahidi ..... Hapa DRC nilipo provider Mkenya!!!!

5. Kwenye hizi ndege biskuti, karanga, korosho made in Kenya!!!!!! imagine hata chakula cha wakimbizi kinatoka Kenya mfano PPN na maziwa anaebisha amwage hija!!!

5. Siku moja niko kwenye warsha mara akasimama Field manager mmoja akiongea kifaransa kibovu bovu akichangia mada nikashawishika nimuulize asili yake kwenye ''pose cafe''kwa kifaransa changu cha ma---vi ma...vi akacheka na kuniambia wewe jombaa mimi nduguyo.... mimi mkenya toka wakati huo tukawa ndugu.... mkenya tena!!!!!. Baada ya hapo nikaja kugundua maboss wengi hapa kwenye nyanja ya Humanitarian iwe UN iwe wapi ni Wakenya .....


Sisi ukisikia mtu akaenda America basi kafuata kaka yake .... au dada yake aliolewa na mzungu... ukimwambia South Sudan au Afghanstan utasikia aaaaa wapi nikafeee? au ukishare hapa job opportunities wataku PM kukuulza kuhusu usalama utasikia '' aaa mkuu wanalipa lakini? natumaje maombi? wakati kila kitu kimejieleza kwenye tangazo ... mwisho kabisa ATAKUAMBIA LAKINI MKUU USALAMA VIPIi? ..... imagine hata waganda wametushinda pale Iraq-Najaf Airport kuna kampuni moja ya ulizi waganda watupu mpaka mademu waganda.

Hapa Goma tulikua waTZ w 4 tu mmoja katimka ni member humu JF japo siji ID yake, tumebaki wa 3 tu lakini wakenya wa kumwaga tena huko UN ndo wamejaa... Uzuri wa hawa jamaa wakiwa nje ya Kenya ni kiswahili tu wakiwa wao kwa wao au wakikutana na wa TZ.....

Msinielewe vibaya sina maana ya kujisifia niliko swampa ila siku moja niko Bar moja huko Cote d'ivoire Abidjan mara wakaaingia hawa jamaa ... wanalonga kiswahili nikajisogeza niwasikie maana walikua wakizungumzia siasa za nchi yao .... waKenya tena sikuona mTZ hata mmoja pale SHIDA Ni nini?

Ila kwa UN mission za kijeshi nasisi tuko safi

Jana nimekereka sana nikitoke BENI Rubani Mkenya... Msaidizi... Mkenya.... Airhostess Mkenya.... Karanga na biscukuti tulizopewa made in Kenya.... aaaaaa wajameni WHY??????


Tutoke waTZ uoga haufai... wengi wetu sasa ni wanasiasa kila mtu POLITIK why???
Huko kote ulikopita mkuu mtanzania alikuwepo, na alikuwa ni wewe
 
Huko kote ulikopita mkuu mtanzania alikuwepo, na alikuwa ni wewe

dah sijui nisemeje unielewe.... vijana wamesoma sana Tanzania na kazi hakuna za kuwatosha.. mimi sio msomi kuwashinda ila nimethubutu na wapo waliothubutu ila idadi yetu hailingani na waKenya... sasa unaona vijana wetu wengi wako mitaani na wengi wameaamua kujiigiza kwenye siasa, sio jambo baya ila sasa kila mtu atakua mwanasiasa? tusiogope.... hali si kama inavyokuwa inaelezwa kwenye TV .... Afghanstan sio yote inamwagika damu ... hapa DRC kuna sahem ni salama sana.... nimeleta huu uzi nakumbuka mwaka jana niliwahi kutoa website hapa za kazi PM nilizo pata ni za ajanu sana....... tujitupe kama kaka zetu miaka ya 80s.... wasomi wapo kabisa TZ ila sijui nini hasa au sisi tulioko huku tuna Roho mbaya!!! nisaidie kufahamu
 
dah sijui nisemeje unielewe.... vijana wamesoma sana Tanzania na kazi hakuna za kuwatosha.. mimi sio msomi kuwashinda ila nimethubutu na wapo waliothubutu ila idadi yetu hailingani na waKenya... sasa unaona vijana wetu wengi wako mitaani na wengi wameaamua kujiigiza kwenye siasa, sio jambo baya ila sasa kila mtu atakua mwanasiasa? tusiogope.... hali si kama inavyokuwa inaelezwa kwenye TV .... Afghanstan sio yote inamwagika damu ... hapa DRC kuna sahem ni salama sana.... nimeleta huu uzi nakumbuka mwaka jana niliwahi kutoa website hapa za kazi PM nilizo pata ni za ajanu sana....... tujitupe kama kaka zetu miaka ya 80s.... wasomi wapo kabisa TZ ila sijui nini hasa au sisi tulioko huku tuna Roho mbaya!!! nisaidie kufahamu
Nimekuelewa vizuri sana mkuu, it was a joke. Mimi nipo pia nchi za wenzetu, watanzania ni wachache sana ila tatizo ni moja na kila mtu aliniambia hivyo hivyo. Wabongo wengi tunajudge kila kitu, na elimu tuliyoipata haimfanyi mtu ajiamini, wabongo hawajiamini na lugha nitatizo kubwa sana. Utamwambia mtu njoo huku kwa wenzetu kunakazi jibu litakuwa umeniona mimi wakubeba box? Pia ujamaa umetuharibu sana, bongo huna kazi ila utakula utalala na kunywa, hiyo haiwezi mfanya mtu awe mtafutaji. Wenzetu elimu inamfanya mtu ajielewe na aelewe namna ya kujichanganya na dunia, umesoma sheria ila uko tayari kufanya kazi yoyote ile ili uweze survive but bongo mtu hawezi fanya hivyo.
 
Kuzubaa tumezubaa
kingereza nacho mtihani
kuchelewa ku embrace market economy
roho mbaya nayo inatuponza
tunashindana wenyewe kwa wenyewe badala ya kusaidiana
ndo maana tunasifika kwa uchawi

Magufuli nimesikia hataki wanajeshi waende nje kwa mission za kigeni
kama kweli basi hilo nalo tutapoteza

na hii sheria ya watumishi wote wa umma waombe vibali ikulu vya kusafiri
tegemea idadi zaidi kupungua...
tutazidi kuwa 'kienyeji zaidi'

Wakenya walitangulia....lakini na sisi tumezubaa
Magufuli kukataa si vibaya, maana ni unafiki kuonekana tunawapenda wa nje halafu ndani tunachukiana
 
Mjinga mmoja. Kwani lazima utukane Madrasa? Shwaini weee. Mbona sisi wengine tumesoma Madrasa na naweza kukuajiri kama msafisha nyumba yangu. Kama huna la kuchangia usitukane watu. Shwaini tena.
Mtu akikuambia wewe si mwanaume, ukavua suruali na chupi hadharani ili kuonyesha umwanaume haikuongezei chochote , elekezaneni, yote tuliyakuta tukasimuliwa, pia tutayaacha
 
mji mkuu wa nchi hii ungekuwa ARUSHA WATANZANIA tungechangamka sana...tatizo ni Pwani...Darisalama kwa wazaramo

Sisi Watanzania kutoka Ukanda wa Pwani tangu hapo ni vilaza; tunachoweza ni madrasa! Ndugu mleta mada, unataka kusema hata wale Watanzania wa mikoa ya bara na mikoa ya Kaskazini wenye IQ kubwa nao hujawaona huko? Au ndo wao wanaendaga Uropa na Marekani kwa dada zao?! Mleta mada acha uongo wako bhana, hebu fanya tafiti zako vizuri! Goooosh! Kumbe umefanya utafiti kwenye makambi ya Wakimbizi... ndo maana! Hebu piga pande za IMF, World Bank, Wall Street, UNDP and in fact, kama shida yako ni kuona ma-hostess and pilots wa Kitanzania; stop searching for us kwenye mashine za kuruka angani... na badala yake tutafute kwenye airlines like Emirates, Qatar or at least British or Turkish Airlines!
 
Watanzania wengi hawana hustler's ambitions. Na wengi mawazo yao 'yameishia Kibamba'.
 
Watanzania tunacho kiweza ni Majungu, roho mbaya, na ushabiki wa siasa
 
Naweza sema vichwa vya kondoo tumeinamia chini wasomi tulio nao sijui ni wasomi dizaini gani? Watu wanawaza hapahapa ajira zimezuiliwa watu wanabanana hapahapa hawana la kufanya hawawazi njia mbadala
 
Back
Top Bottom