Hii ni mada nzuri, lakini najua kuna watu kwa sababu ya 'blind nationalism' au ubishi wa kipuuzi wataleta maudhui nyingine zisizo na mashiko au hata kumkashifu aliyeleta thread. Tatizo ni kuwa wengi wa wanaofanya hivyo hawajatoka nje na kwao Dar ni 'jiji'. Ni kama chura aliye ndani ya dimbwi anaona hiyo ndiyo dunia. Jaribu kumwambia kuna bahari pia.....atajibu g'waaaaaa!
Kwa kweli mleta mada suala kama hilo limenitafuna sana akili. Lakini hatimaye nikafikia nadharia hii:
Ukoloni, pamoja na ubaya wake, una mambo mengi mazuri. Tofauti kubwa baina ya Tanzania na nchi za Kenya na Uganda kwa kweli ni kwa sababu Mkoloni alitawala nchi hizo. Katika kesi ya Kenya, kwa kweli hakutaka hata kuondoka. Kumbuka sisi hatukutawaliwa kwa maana ya 'colonization' walikuja wazungu wachache tu kufanya admin ili kutimiza jukumu la Umoja wa Mataifa. Kenya, kama South Afrika, ilikusudiwa Wazungu waishi kama kwao, ingawaje sehemu Fulani. Hivyo, kilipoingia kipindi cha Uhuru Wakenya tayari walikuwa mbele sana. Kuwa mbele si kwa majengo na miundombinu tu, bali pia kwa 'mentality'. Kwa sababu ukikaa karibu na mtu aliyeendelea na wewe utaendelea. Ujamaa ukatuongezea mzizimo wa akili. Kwa maana watu wakawa tegemezi kwa serikali na hata ndugu. Hushangaa sana nchini Kenya, mtu akiwa amefanikiwa kifedha si aghalabu kuona ndugu 'wakimnonea' wakitarajia awasaidie kwa hili na lile. Tanzania tabia hii imeenea sana kiasi cha kuwarudisha nyuma hata wale waliondelea kidogo.
Pengine nimetoka kwenye maudhui kidogo, lakini kwa ujumla yote hayo yanafasiri kwa nini itatuchukua muda mrefu hata kuwakaribia Wakenya. Kweli, Tanzania ni tajiri kuliko Kenya na yumkini ikaweza siku moja kuwa na majengo na barabara nzuri kuliko Kenya, lakini maendeleo ya mtu itachukua muda mrefu sana.
Hata hapa unasoma kuna watu wanaona Wakenya kufanya kazi UAE au hapa na pale....ni kwa sababu ya shida, au dhiki! Hiyo ndiyo mentality ya Wabongo.