Wakenya wanatuacha mbaaali sana Watanzania, Kwanini?

Wakenya wanatuacha mbaaali sana Watanzania, Kwanini?

Mpka leo sijui ni kwanini sisi Watanzania tuko nyuma ya waKenya kwa maujanja sijajua naomba nanyi mnijuze hapa!!!!Mimi hapa nitatoa ushahidi kama kuna mtu atapinga basi apinge kwa ushahidi.

Wakenya wanaongoza kwa madiaspora tena waKenya wengi wako kwenye kazi za maana ughaibuni. Ukweli usemwe!!

1. Nimefika Dubai Airport, mweusi anaefanya Duty free karibia zote ni mKenya... Kiswahili analonga
2. Airlines maarufu nyimngi waKenya wako pale wengine kama ma Pilots na maairhostess, anaebisha atoe nae hoja yake!!! . Mfano shirika la ndege la Fly Dubai wakenya wako pale waTZ Ziiiii why!!!

3. UNHAS hili ni shirika la la ndege la WFP kwenye Humanitarian movement, nimefika South Sudan, WaKenya ndio ma airhostess na ma Pilot karibia wote!!!, nikasema labda hapa SSD pekee maana ni jirani... aaa wapi bwana niko hapa DRC, waKenya ndio marubani wa ndege Zote za UNHAS na ma airhostess wote .. wanalonga kiswahili na English, asie elewa kazi kwake mkenya yuko job bwana.... why not waTZ?

4. Service providers wengi kwenye Humanitarian movment ni wa Kenya...... South Sudan kwa mfano Internet service provider wakubwa wa Visat, na items nyingine wakenya alieyefika WAU ni shahidi ..... Hapa DRC nilipo provider Mkenya!!!!

5. Kwenye hizi ndege biskuti, karanga, korosho made in Kenya!!!!!! imagine hata chakula cha wakimbizi kinatoka Kenya mfano PPN na maziwa anaebisha amwage hija!!!

5. Siku moja niko kwenye warsha mara akasimama Field manager mmoja akiongea kifaransa kibovu bovu akichangia mada nikashawishika nimuulize asili yake kwenye ''pose cafe''kwa kifaransa changu cha ma---vi ma...vi akacheka na kuniambia wewe jombaa mimi nduguyo.... mimi mkenya toka wakati huo tukawa ndugu.... mkenya tena!!!!!. Baada ya hapo nikaja kugundua maboss wengi hapa kwenye nyanja ya Humanitarian iwe UN iwe wapi ni Wakenya .....

Sisi ukisikia mtu akaenda America basi kafuata kaka yake .... au dada yake aliolewa na mzungu... ukimwambia South Sudan au Afghanstan utasikia aaaaa wapi nikafeee? au ukishare hapa job opportunities wataku PM kukuulza kuhusu usalama utasikia '' aaa mkuu wanalipa lakini? natumaje maombi? wakati kila kitu kimejieleza kwenye tangazo ... mwisho kabisa ATAKUAMBIA LAKINI MKUU USALAMA VIPIi? ..... imagine hata waganda wametushinda pale Iraq-Najaf Airport kuna kampuni moja ya ulizi waganda watupu mpaka mademu waganda.

Hapa Goma tulikua waTZ w 4 tu mmoja katimka ni member humu JF japo siji ID yake, tumebaki wa 3 tu lakini wakenya wa kumwaga tena huko UN ndo wamejaa... Uzuri wa hawa jamaa wakiwa nje ya Kenya ni kiswahili tu wakiwa wao kwa wao au wakikutana na wa TZ.....

Msinielewe vibaya sina maana ya kujisifia niliko swampa ila siku moja niko Bar moja huko Cote d'ivoire Abidjan mara wakaaingia hawa jamaa ... wanalonga kiswahili nikajisogeza niwasikie maana walikua wakizungumzia siasa za nchi yao .... waKenya tena sikuona mTZ hata mmoja pale SHIDA Ni nini?

Ila kwa UN mission za kijeshi nasisi tuko safi

Jana nimekereka sana nikitoke BENI Rubani Mkenya... Msaidizi... Mkenya.... Airhostess Mkenya.... Karanga na biscukuti tulizopewa made in Kenya.... aaaaaa wajameni WHY??????

Tutoke waTZ uoga haufai... wengi wetu sasa ni wanasiasa kila mtu POLITIK why???

Tatizo letu sisi ni kuendekeza uswahili kwa maana ya USWAHILI
 
Siku hizi maendeleo ni kwenda kufanya kazi nyingine za ovyo ughaibuni?
Honestly, kuna vitu Kenya imetuzidi lakini sio hiyo mifano ya mleta maada.
Mkuu wasomi wetu sisi ni wa viwango vya VETA hawana uwezo wa kuingia kwenye soko la ajira la kimataifa huu ndiyo ukweli.
 
Mkuu wasomi wetu sisi ni wa viwango vya VETA hawa uwezo wa kuingia kwenye soko la ajira la kimataifa huu ndiyo ukweli.
Sikubaliani na ww hata kidogo. Hivi ushawahi enda huko kwenye mataifa kufanya utafiti.
 
Sisi Watanzania kutoka Ukanda wa Pwani tangu hapo ni vilaza; tunachoweza ni madrasa! Ndugu mleta mada, unataka kusema hata wale Watanzania wa mikoa ya bara na mikoa ya Kaskazini wenye IQ kubwa nao hujawaona huko? Au ndo wao wanaendaga Uropa na Marekani kwa dada zao?! Mleta mada acha uongo wako bhana, hebu fanya tafiti zako vizuri! Goooosh! Kumbe umefanya utafiti kwenye makambi ya Wakimbizi... ndo maana! Hebu piga pande za IMF, World Bank, Wall Street, UNDP and in fact, kama shida yako ni kuona ma-hostess and pilots wa Kitanzania; stop searching for us kwenye mashine za kuruka angani... na badala yake tutafute kwenye airlines like Emirates, Qatar or at least British or Turkish Airlines!
Kote huko wakenya wako wengi, hata unapokutaja wewe. Tukienda mbali zaidi university zote UK na US zina wakenya wengi kuliko wa TZ na Ugandans combined.
Kama boss alivyosema tumechelewa ku embrace Market economy na sasa hivi tutarudi nyuma zaidi. Swala Dogo tu la dual citizenship ni issue, halafu unataka watu wako wafanye kazi sehemu mbali mbali, wanafanya bila documents?
 
Mpka leo sijui ni kwanini sisi Watanzania tuko nyuma ya waKenya kwa maujanja sijajua naomba nanyi mnijuze hapa!!!!Mimi hapa nitatoa ushahidi kama kuna mtu atapinga basi apinge kwa ushahidi.

Wakenya wanaongoza kwa madiaspora tena waKenya wengi wako kwenye kazi za maana ughaibuni. Ukweli usemwe!!

1. Nimefika Dubai Airport, mweusi anaefanya Duty free karibia zote ni mKenya... Kiswahili analonga
2. Airlines maarufu nyimngi waKenya wako pale wengine kama ma Pilots na maairhostess, anaebisha atoe nae hoja yake!!! . Mfano shirika la ndege la Fly Dubai wakenya wako pale waTZ Ziiiii why!!!

3. UNHAS hili ni shirika la la ndege la WFP kwenye Humanitarian movement, nimefika South Sudan, WaKenya ndio ma airhostess na ma Pilot karibia wote!!!, nikasema labda hapa SSD pekee maana ni jirani... aaa wapi bwana niko hapa DRC, waKenya ndio marubani wa ndege Zote za UNHAS na ma airhostess wote .. wanalonga kiswahili na English, asie elewa kazi kwake mkenya yuko job bwana.... why not waTZ?

4. Service providers wengi kwenye Humanitarian movment ni wa Kenya...... South Sudan kwa mfano Internet service provider wakubwa wa Visat, na items nyingine wakenya alieyefika WAU ni shahidi ..... Hapa DRC nilipo provider Mkenya!!!!

5. Kwenye hizi ndege biskuti, karanga, korosho made in Kenya!!!!!! imagine hata chakula cha wakimbizi kinatoka Kenya mfano PPN na maziwa anaebisha amwage hija!!!

5. Siku moja niko kwenye warsha mara akasimama Field manager mmoja akiongea kifaransa kibovu bovu akichangia mada nikashawishika nimuulize asili yake kwenye ''pose cafe''kwa kifaransa changu cha ma---vi ma...vi akacheka na kuniambia wewe jombaa mimi nduguyo.... mimi mkenya toka wakati huo tukawa ndugu.... mkenya tena!!!!!. Baada ya hapo nikaja kugundua maboss wengi hapa kwenye nyanja ya Humanitarian iwe UN iwe wapi ni Wakenya .....

Sisi ukisikia mtu akaenda America basi kafuata kaka yake .... au dada yake aliolewa na mzungu... ukimwambia South Sudan au Afghanstan utasikia aaaaa wapi nikafeee? au ukishare hapa job opportunities wataku PM kukuulza kuhusu usalama utasikia '' aaa mkuu wanalipa lakini? natumaje maombi? wakati kila kitu kimejieleza kwenye tangazo ... mwisho kabisa ATAKUAMBIA LAKINI MKUU USALAMA VIPIi? ..... imagine hata waganda wametushinda pale Iraq-Najaf Airport kuna kampuni moja ya ulizi waganda watupu mpaka mademu waganda.

Hapa Goma tulikua waTZ w 4 tu mmoja katimka ni member humu JF japo siji ID yake, tumebaki wa 3 tu lakini wakenya wa kumwaga tena huko UN ndo wamejaa... Uzuri wa hawa jamaa wakiwa nje ya Kenya ni kiswahili tu wakiwa wao kwa wao au wakikutana na wa TZ.....

Msinielewe vibaya sina maana ya kujisifia niliko swampa ila siku moja niko Bar moja huko Cote d'ivoire Abidjan mara wakaaingia hawa jamaa ... wanalonga kiswahili nikajisogeza niwasikie maana walikua wakizungumzia siasa za nchi yao .... waKenya tena sikuona mTZ hata mmoja pale SHIDA Ni nini?

Ila kwa UN mission za kijeshi nasisi tuko safi

Jana nimekereka sana nikitoke BENI Rubani Mkenya... Msaidizi... Mkenya.... Airhostess Mkenya.... Karanga na biscukuti tulizopewa made in Kenya.... aaaaaa wajameni WHY??????

Tutoke waTZ uoga haufai... wengi wetu sasa ni wanasiasa kila mtu POLITIK why???

Elimu..Elimu..Elimu...socialism mindset..hapo ndio mlipoteza timing atii!
 
Kote huko wakenya wako wengi, hata unapokutaja wewe. Tukienda mbali zaidi university zote UK na US zina wakenya wengi kuliko wa TZ na Ugandans combined.
Kama boss alivyosema tumechelewa ku embrace Market economy na sasa hivi tutarudi nyuma zaidi. Swala Dogo tu la dual citizenship ni issue, halafu unataka watu wako wafanye kazi sehemu mbali mbali, wanafanya bila documents?
Kwamba hivi sasa tunarudi nyuma; HAPANA! Hamna kipindi ambacho mabepari wa Kenya kama akina Kenyatta wamekuwa wakiiogopa Tanzania kama sasa na ndio maana hata ukiangalia harakati za Kenyatta na Kenya yake ni kujitahidi kila hali kutaka kuizuia Tanzania isije ku-take over!!!! Chukulia mfano wa reli ya Standard Gauge kule Kenya... ile project ilikuwa ni ya muda mrefu sana lakini Kenyatta alipoingia tu; ili apate kutupiga bao, akai-speed up ile project na kutengeneza fitina ndani ya jumuiya kupitia kile ambacho kilijulikana kama Coalition of Willing! Haraka ile ya Kenyatta ilikuwa ni kutaka kuziteka Uganda na hususani Rwanda kutoka ku-join reli ya kati! Akina PK nao na bifu zao na JK wakaingia kichwakichwa huku mtu kama PK akisahau kwamba ni too risky kutegemea reli inayopita nchi mbili tofauti (Kenya & Uganda) wakati nchi zenyewe stability yake haitabiriki!

Hata hivyo, Rwanda wameshajitoa kwenye uke mpango na mwezi july mwaka jana wakakubaliana na Tanzania kujenga reli ya pamoja! Uganda nao ni kama wame-relax kwa sasa... nguvu zao zote wameelekeza South Sudan ambako nako hakutaki kutulia! Watani zetu hawataki tu kusema lakini ule mradi wa Standard Gauge ushaanza kuzua hofu Kenya manake uwekezaji wa reli ya standard gauge ni very expensive ambao kutegemea tu domestic transportation ni very risk.

Kuhusu suala la dual citizenship haliwezi kuwa sababu kwanini Wakenya wamekuwa sehemu nyingi kuliko Watanzania! Hata hao Wakenya wanaoenda huko kufanya kazi huwa wanaenda wakiwa na uraia mmoja tu... KENYAN CITIZENSHIP tukiacha wanaopata uraia mwingine kutoka kwa wazazi wao! Umuhimu wa dual citizenship unakuja pale ambapo wakati mtu tayari ni Mkenya lakini bado anachukua uraia wa nchi nyingine ile kuweza ku-grab more opportunities!

Kuna ukweli hapa tunatakiwa kuukubali na tusione aibu ku-admit! Si kwamba eti Wakenya ni wasomi sana kama wengine wanavyotaka tuamini! Na wala si kwamba Wakenya ni watalaamu sana au ni very smart lakini kinachowasaidia Wakenya ni kwamba wapo very aggressive! Mtu aliyekuwa aggressive kwenye kutafuta ana nafasi kubwa ya kupata kile anachokitaka kuliko asiye aggressive hata kama yule asiye aggressive ndie mtalaamu kwelikweli! Hizi opportunities huwa haziji by chance au by means of good lucky... hazibishi hodi mlango wa yeyote! Opportunities zinatafutwa! Na wakati wewe unatafuta kuna mamilioni ya mamilioni ya wengine wanatafuta same opportunities na hapo kinacho-matter ni zaidi ya elimu but how aggressive you're!
 
Kutowaona watz huko maeneo sio kigezo kuwa sio wajanja, hamia basi kenya nawew tukuite mkenya maana maona hicho ndo unachokitaka
 
Watanzania tukubali Wakenya wanatuzidi kwenye nyanja nyingi sana huo ndo ukweli na utabakia kuwa ukweli.

1.Nenda pale TIC Tanzania Investment centre cheki Taifa la pili kuwekeza Tanzania kwa wingi ni Kenya,Je sisi ni wangapi kule kwao?

2. Watanzania hatuthamini vitu vyetu. Nenda Kenya kama kuna mkenya anatazama sijui TBC, au ITV au EATV, ila Tanzania kila siku ni ciityzentv, au KCB,
3. Sijawahi ona magazeti ya Tanzania kenya but Magazeti ya Kenya Tanzania ni hadi mtwara unayapata.

3. Wakenya wanafanya kazi sana, na wanajituma na hii ni kutokana na shida walizo nazo.

4. Nenda kacheki barabara zao flyover zao, sisi wakati tunaplani kujenga fly over wao wanajikita kwenye treni za umeme.

Wabongo tunaoneana wivu sisi kwa sisi, tunarudihsana nyuma sisi kwa sisi, mchawi wetu ni sisi wenyewe, kuanzia taasisi za serilkali mpaka wananchi wenyewe.

Kenya wako mbali sana, hilo halina ubishi, na kushindana nao inahita kazi na si porojo, hatuwezi shindana nao kwa porojo za vijiweni na kwenye keybord.
 
Penda usipende Bila kujua English fluently utaachwa nyuma kimataifa, nashangaa watanzania tunapiga vita lugha ya kiingereza na hata juzi kwenye mdahalo wa ITV walimu wanadai lugha ya kufundisha kutoka shule ya awali hadi Chuo Kikuu iwe kiswahili!? Kiingereza ndio Kiswahili cha Dunia, hapa nchini ajira hamna na hata mataifa ya nje yakija kufanya biashara hapa agent wao ni wakenya kwa sababu ya communication tu, tukubali ukweli, tuache siasa.
 
bado nina wasiwasi sana na ideology ya socialism na impact yake katika uchumi, sawa imesababisha political stability ya nchi na kiasi kikubwa umoja wa nchi, lakini ni wazi kuwa inadumaza mno upeo wa kukuza uchumi katika ngazi ya nchi....unahitaji kuwa very smart kuendelea katika mfumo wa kijamaa, smart kama china ambayo portion kubwa ya population ni wachapakazi, sisi ni tofauti kabisa ndio maana hatujaweza kutumia fursa tulizonazo to their full potential, hata hiyo china ya sasa haipo kijamaa kama maana halisi ya ujamaa ilivyo....BTW hata Tz kuna mabadiliko ya sera na ndio maana uchumi kwa kiasi flani unakua kwa kasi japo bado tunahitaji usimamizi bora zaidi wa sera na mipango ya uchumi kuweza kufikia full potential ya utilization ya resources zilizopo
 
Kuzubaa tumezubaa
kingereza nacho mtihani
kuchelewa ku embrace market economy
roho mbaya nayo inatuponza
tunashindana wenyewe kwa wenyewe badala ya kusaidiana
ndo maana tunasifika kwa uchawi

Magufuli nimesikia hataki wanajeshi waende nje kwa mission za kigeni
kama kweli basi hilo nalo tutapoteza

na hii sheria ya watumishi wote wa umma waombe vibali ikulu vya kusafiri
tegemea idadi zaidi kupungua...
tutazidi kuwa 'kienyeji zaidi'

Wakenya walitangulia....lakini na sisi tumezubaa
Nakuunga mkono mkuu
 
Nasikia tuliwadhulumu na mbuga ya serengeti na mlima Kilimanjaro!!!! -ama kweli sie watanzania bure kabisa
 
Hujui ulisemalo. Fyi Tz ilikua imeiacha Kenya mbali hadi mwanzoni mwa 2000's ndio Kenya imeipiku Tz, hivyo hoja za sijui wakoloni hazina mashiko

Kuhusu Kenyans wengi kuwa nje ya nchi sio sifa muda wote, umewahi jiuliza kwanini kuna nchi zimeendelea na ni very rare kukuta raia wake nje ya mipaka yao, mathalani Scandinavian countries au kwa Africa SA, Kenyans wapo nje sababu ndani kumebanwa kuna watu wanahodhi uchumi wa nchi Lakini wametumia fursa vizuri maana kuna nchi kama Rwanda watu kibao wapo nje ila hamna cha maana wamefanya. Kwahiyo bahati mbaya ya waTz ni kuwa tunabahati nzuri sana
Hujui unachosema. Tanzania ilikuwa mbele ya Kenya katika nini? Mambo haya nilidhani yamekwisha kwa ujio wa internet ambapo figure zote ziko wazi na zimefanyiwa utafiti. Tuliishinda katika nini- elimu, usambazaji wa maji, umeme, per capita, GDP au nini?
 
D
Peleka upuuzi wako kama hizo nafasi ni za maana sana basi GDP yao ingekuwa twice yetu! Sio lazma kuwa kama wao kila nchi ina economic models zake. We inaelekea ushamba flani unakusumbua

Duh,,aisee
 
Ok. Wee unakashifu waliosoma Madrasa kama mimi , sasa nakutaka tuandike comment hapa kwa lugha za Kifaransa, kiingereza, Kitaliano na Kiarabu.... kama utaweza. Yaani unajiona una akili nyingi kuliko waliosoma Madrasa, kitu gani kinakupa ujeuri na dharau hiyo? Ni hatari kwa watu kama nyie mkipewa kompyuta mnajificha nyuma yake na kujifanya mmeelimika. Madrasa inatufundisha hata ukiwa na elimu namna gani ukumbuke " hamkupewa elimu ila kidogo tu" In fact, mtu mwenye elimu ya kweli huogopa kusema ana elimu kwa sababu kila unavyoendelea kusoma unakuta elimu ni bahari na huwezi kuimaliza. Mwenye elimu ya kweli yuko humble sio kama wewe. Ujue comment zako zinatuudhi sana na hustahiki kuheshimiwa.
Mkuu msamehe bure mjinga Huyo,,
 
Na kuwasifia koooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooote... Kenya imeshindwa kutibu ukabila na ukanda... Nenda kenya uone huo ukabila then uje usimulie hapa
 
Sisi Wa
Kutowaona watz huko maeneo sio kigezo kuwa sio wajanja, hamia basi kenya nawew tukuite mkenya maana maona hicho ndo unachokitaka

tanzania kutoka Ukanda wa Pwani tangu hapo ni vilaza; tunachoweza ni madrasa! Ndugu mleta mada, unataka kusema hata wale Watanzania wa mikoa ya bara na mikoa ya Kaskazini wenye IQ kubwa nao hujawaona huko? Au ndo wao wanaendaga Uropa na Marekani kwa dada zao?! Mleta mada acha uongo wako bhana, hebu fanya tafiti zako vizuri! Goooosh! Kumbe umefanya utafiti kwenye makambi ya Wakimbizi... ndo maana! Hebu piga pande za IMF, World Bank, Wall Street, UNDP and in fact, kama shida yako ni kuona ma-hostess and pilots wa Kitanzania; stop searching for us kwenye mashine za kuruka angani... na badala yake tutafute kwenye airlines like Emirates, Qatar or at least British or Turkish Airlines!

Sasa chukua hii!!!! mpaka sasa nje ya Tanzania hasa Ulaya na at least kule niliko fika mimi ukiwa park au puplic places yoyote ukiongea kiswahili na nduguyo iwe kwa simu au mko wawili au zaidi utasikia hata ka ajuza kakikuuliza '' are you Kenyan? for sure utasema Noooo am Tanzanian..... utakakasikia tena Tanzania? where is that ..... sasa hapo inabidi ukaze misuli hasa Tanzania is Country of Kilimanjaro .... katarudi tena Kililmanjaro not in Kenya? noooooo is in Tanzania.... Ok so where is Tanzania... ukitaka ufupishe maneno na ka ajuza hako wewe sema is comibination of Zanzibar and Tanganyika.... hapo mapengo yote utayaona nje ...... Zanzibaaaaaa I want to go there before I die.... wanaijua Zanzibar kweli watu wa ughaibuni.... huku Afrika Tanzania inafahamika sana japo umaarufu wa Zanzibar uko juu sana... kuhusu Kiswahili hawa wakenya wametupora tena.... amini usiamini.... wengi wanajua Kiswahili asili yake ni KENYA hasa huko Uzunguni
 
Na kuwasifia koooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooote... Kenya imeshindwa kutibu ukabila na ukanda... Nenda kenya uone huo ukabila then uje usimulie hapa
Hakuna taifa lililokamilika hivyo, ukabila uliopo Kenya haubadili ukweli katika hili tunalozungumzia....tujifunze mazuri yao mabaya tuwaachie tutafika mbali...
 
Back
Top Bottom