Wakenya na Ardhi ya Tanzania. Tuweni Makini!

Mwingereza

JF-Expert Member
Jan 21, 2014
1,111
2,741
Leo nikiwa mmoja ya Watanzania walioalikwa kwenye mnuso na Wakenya iliyofanyika nyumbani kwa Mkenya mmoja maeneo ya Mbezi Beach, baada ya kupiga gambe la uhakika, Wakenya walianza kuropoka. Ila nilishtushwa na kushanganzwa jinsi walivyokuwa wakisema waziwazi, kwamba maendeleo ya Kenya hasa kwenye sekta ya chakula/viwanda inahitaji Tanzania kwa 65%.

Kwa maana hiyo ni lazima waje kwa wingi maana serikali iinawahimiza kuja Tanzania. Kuna baadhi ya wakenya ambao wako Tanzania, na kazi yao kubwa ni kuwatafutia ajira wenzao nchini Tanzania. Mmoja amesema amehitimu 2016 na Kabla ya graduation, alipewa mtonyo wa kazi. Alipoenda, alipewa namba ya mtu anayefanya usahili ya watu wanaokuja Tanzania kutafuta ajira. Maongoezi yaliendelea, huku kila moja anasema ujanja wake.

Wallienda mbali zaidi na kusema, "sasa hivi ni tuoe hawa wanawake zao juu tupate hii land ambayo hiko mingi na hakuna kazi" kama unaenda huku, Tabora imejaa mapori hakuna maendeleo wowote. Mwingine akasema, Mimi sijaoa mwanamke wa TZ, lakini nina land Mbweni ya kujenga hao yangu, by June next year, na shamba ya 20 acres kule morogoro. Nataka kwenda kulima maua"

Walienda mbali zaidi na kusema, kwa sasa, Raia wao wengi wako kwenye kila idara nchini Tanzania, na wengi wao wana vibali vya kazi wanazoletewa majumbani kwao na ni halali. . Nadhani pombe iliwasahaulisha kwamba watanzania tulikuwepo. Wakaenda mbali zaidi na kujigamba walivyo na Passport na vitambulisho via Taifa. Wanasema kwamba kupata Pasi ya Tanzania ni rahisi mno, ni chapa yako tu.

Mwingine mdada, kasema yeye amekamatwa mara 4, kaambiwa hadi aondoke lakini hawezi kuondoka, maana watu wa imagreshon wanahitaji hela tu. Yaani mambo yalikuwa ni mengi. Na pale hakuna wa kurudi, ni kuoa Tanzania, kununua Ardhi, Kazi na kujenga.

Swali langu. Hivi ukioa mtanzania ardhi ni free access?
 
Hukufanikiwa kurekodi japo ka-audio? Kama hujarekodi na una simu yenye uwezo wa kurekodi, basi hii itakuwa ni porojo Kama porojo zingine.
 
Mwanzo nilitaka kukuamini na stori yako hii, lakini mwisho nikaona unapiga kona nyingi bila sababu.

Wewe ulialikwa hapo uje utusimulie wanavyowaona nyinyi marafiki zao mlivyo vilaza?

Na unapokuja kutusimulia hapa JF, unategemea nini kifanyike, tukawabebe mzobe mzobe na kuwatupa nje ya mpaka wetu?

Wewe binafsi umefanya nini ili kuhakikisha hayo mapori wanayotaka kuvamia na wewe utaambulia chochote usije ukajikuta kama walivyojikuta huko kwao hawana lolote hadi ikabidi wakimbilie huku?

Wakishayagawana hayo mapori, wewe na vijukuu zako mtakimbilia wapi, huko kwao?

Naweza kukuuliza maswali mengi sana ambayo hutaweza kuwa na majibu yake; lakini ngoja nikupe ushauri tu: Haitoshi kuja hapa na kulalamikia hawa watu ambao ni wazi wanawatumia nyinyi wenyewe (wewe pamoja na waalikwa wenzio). Nyinyi ndio mnaotumiwa na hawa watu, halafu unajigeuza na kuja kulialia hapa.

Ukitoka hapa baada ya kuona watu wakililalia juu ya mada yako hii, unakwenda kujifurahisha na hao marafiki zako kwa matokeo mliyoyapata kuwatia jambajamba waTanzania.

Nikwambie jambo. Kenya sio lolote kwa Tanzania. Mtahangaika sana lakini hamtaweza kuizuia Tanzania kuchukuwa nafasi yake ya heshima katika eneo hili. Muda si muda mtakuwa mkija hapa kutufanyia kazi kama mnavyowafanyia waarabu huko ghuba. Kwa hiyo hatutishiki, hamtutishi kwa lolote.

Nenda kawaambie hivyo hao rafiki zako.
 
Mimi sielewi kwann watu wanaogopa wakenya watachukua ardhi yetu as if huwa wanapora mtu.

Sasa mimi nina eka 2 nikapata shida katokea mkenya nisimuuzie? Na hakuna atakae kosa ardhi kama sisi wenyewe waTz kila mmoja atakuwa makini kuangalia na kutouza ardh hadi ya wajukuu zake lakin kama tutaendelea na hii system ya kuuza ovyo kila tukipata shida mwisho hata tukiwatoa wakenya wote ardh itabaki kwa waTz wachache wanaonunua ardhi sasa.
 
Back
Top Bottom