Wakenya wanajua kuitumia ardhi kwa manufaa zaidi kuwazidi Watanzania?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Siku chache zilizopita, nilimtembelea mkulima mmoja wa matunda nchini Kenya. Taswira ya shambani kwake ilinipa ujumbe kuwa ni mkulima mwenye mafanikio mazuri.

Japo hana na eneo kubwa sana, analitumia kikamilifu eneo lililopo. Sidhani kama shamba lake lote linazidi ekari tano!

Aliniambia kuwa kwa kawaida, robo ekari humwingizia shilingi milioni moja hela ya Kenya kwa mwaka

Milioni moja ya Kenya ni kama milioni kumi na sita hela ya Tanzania.

Sitilii mashaka maelezo yake, ila najiuliza kama kuna Watanzania wanaopata mafanikio kama hayo kupitia kazi za shamba.

Na kwa kuwa bado sijamsikia Mtanzania mwenye mafanikio kama hayo, nimebaki najiuliza: Wakenya wenye uhaba wa ardhi wanajua namna bora ya kutumia ardhi kwa kilimo chenye tija kuwazidi Watanzania wenye ardhi bwerere?
 
Mkenya ana masoko ya uhakika baada ya kuvuna tukianzia nchini kwao pamoja na nchi za nje. Wabongo wanategemea dalali.
 
Kenya kuwa na kiwango kikubwa cha elimu kimewasaidia sana kupunguza kuwa na tabia za kiswahili ambazo ni very common among the people of Tanzania.

Na hii kwa kiasi kikubwa ndio inasababisha Tanzania kuwa na uchumi mdogo tofauti na Kenya pamoja na kuwa na rasilimali nyingi zaidi kuishinda Kenya.
 
Nini kinachomkwamisha Mbongo kutafuta soko la nje? Kwa sababu utakuta hata huyo dalali naye ni Mtanzania pia.

Wakenya wamewazaje kupata soko la nje ilhali Watanzania wanakosa?
Kikubwa ni urasimu ila pia Tanzania kupata soko nje ni ishu maana wakulima wetu wengi hawana exposure. Ni kundi dogo mno linaloweza kuzalisha kwa quality na capacity inayotakiwa nje na ndio sababu wa Kenya wengine wamezamia humu humu nchini kulima na kununua mazao kupeleka nchini kwao for exports.
 
Kenya kuwa na kiwango kikubwa cha elimu kimewasaidia sana kupunguza kuwa na tabia za kiswahili ambazo ni very common among the people of Tanzania.

Na hii kwa kiasi kikubwa ndio inasababisha Tanzania kuwa na uchumi mdogo tofauti na Kenya pamoja na kuwa na rasilimali nyingi zaidi kuishinda Kenya.
Hata Tanzania walioelimika ni wengi mno ila system imeshikiliwa na waswahili. Siku mfumo ukishikiliwa na mtu alienyooka mabadiliko ni ndani ya miaka michache mno.
 
Kenya kuwa na kiwango kikubwa cha elimu kimewasaidia sana kupunguza kuwa na tabia za kiswahili ambazo ni very common among the people of Tanzania.

Na hii kwa kiasi kikubwa ndio inasababisha Tanzania kuwa na uchumi mdogo tofauti na Kenya pamoja na kuwa na rasilimali nyingi zaidi kuishinda Kenya.
Mkuu, unamaanisha nini kusema "kiwango kikubwa cha Elimu?"

~ Elimu yao ni bora?

~ Watu wengi wameelimika?
 
Kikubwa ni urasimu ila pia Tanzania kupata soko nje ni ishu maana wakulima wetu wengi hawana exposure. Ni kundi dogo mno linaloweza kuzalisha kwa quality na capacity inayotakiwa nje na ndio sababu wa Kenya wengine wamezamia humu humu nchini kulima na kununua mazao kupeleka nchini kwao for exports.
🙏🙏🙏
 
Nini kifanyike ili wakulima wa Kitanzania nao wapate exposure kama wenzao wa Kenya?
 
Mkuu, unamaanisha nini kusema "kiwango kikubwa cha Elimu?"

~ Elimu yao ni bora?

~ Watu wengi wameelimika?
Elimu yao ni bora kwa sababu medium of instruction inayotumika kwa ngazi zote za elimu wote wanaielewa vizuri tofauti na Tanzania.

Karibu kila mkenya ana elimu ya sekondari na zaidi ya asilima 60 wana elimu ya chuo ndio maana huwezi ukawaambia eti wakimbize mwenge wakakubali maanake wanafahamu ni mbinu nyingine tu ya ufisadi kwani wanafahamu mwenge haina uhusiano wowote na mikakati ya kimaendeleo.
 
Mambo ya kufananisha nchi jirani na sisi huku Bongo.. hayasaidii...

Kila nchi ina mfumo wake wa uendeshaji..

You can't paste it katika uhalisia wa maisha yetu..
 
Back
Top Bottom