KERO Maji ya DAWASA yana harufu na ladha ya Dawa kali sana, ni salama kweli?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
DAWASA tunawashukuru sana kwa kuanza kurejesha huduma ya Maji baada ya kukatika kwa muda mrefu huku mkieleza chanzo ilikuwa kurekebisha mitambo ya machujio ya tope. Lakini sasa kuna jipya, maji yenu yanakuja harufu kali sana ya Dawa za kutibu maji kiasi kwamba hata ladha ya maji imepotea.

Sasa swali langu hizo dawa ni salama kiasi gani kwa watumiaji? msije kutusababishia Kansa za matumbo jamani.

Pia soma:
- KERO - Wakazi wa Mbezi Beach tunapata maji ya bomba machafu, na yana harufu mbaya. Mlipuko wa magonjwa unakuja
 
Dar es salaam ni kuchafu sana

Sio kwenye maji tu, ila hata vyakula vya mtaani vingi vinaandaliwa katika mazingira machafu na hata mazingira kwa ujumla wake yaani compound na hali ya hewa ni chafu sana.
 
Maji ya DAWASA kila siku yana ladha mpya.
Mpaka unashindwa kuelewa haya maji vipi!!!

Kuna siku unakuta kama Chumvi, Tope tope n.k.

Watujulishe shida ni nini?
 
"WHOLE HOUSE SEDIMENT FILTER au CHUJIO" kama inavyoonekana kwenye picha. Inatumika kuchuja maji nyumbani, hotelini, na ofisini, inachuja vumbi, tope, uchafu na kukusaidia upate maji kwa matumizi ya kila siku.

Zinapatikana katika rangi tofauti:
⚪ RANGI NYEUPE: Hii inadumu kwa muda mrefu hata ikipigwa na jua. Lakini pia inaonyesha vizuri kama filter yako imechafuka na ni muda wwa kubadilisha.

🔵 RANGI YA BLUE: Hii inaficha uchafu kwa nje huwezi kuona kama ndani imechafuka na inahitaji kubadilisha, imara na inadumu.
Bei ni tshs 70000

Kwa msaada, ushauri na manunuzi,
Wasiliana nasi: 📞 +255 758 404 554
KARIBU SANA.
 

Attachments

  • IMG-20240418-WA0001.jpg
    IMG-20240418-WA0001.jpg
    64.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom