Wakazi wa DAR wenye uhitaji wa Internet katika kazi zenu kuanzia Ofisini mpaka Nyumbani, suluhisho hili hapa

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,989
Najua watu wengi sana hutumia internet katika mishe za hapa na pale,binafsi ni wale watu wanaoishi mjini kwa kutegemea internet kwa sana, pamoja na mengine ninayofanya ila nina mengi makubwa nayafanya kupitia internet.

Nimeshatumia internet mbali mbali za makampuni makubwa na madogo, na baadhi ya kampuni nilizowahi tumia nilishazitoleaga ufafanuzi kwenye thread yangu 1👇


Kama ilivyo kawaida yangu huwa sipendi kukaa na kitu au kutumia kitu kizuri peke yangu huwa napenda shirikisha watu yale mazuri ambayo naona yatawavusha kutoka sehemu 1 kwenda sehemu nyingine.

Makampuni makubwa mengi niliyotumia hayaunganishi hii huduma kwa watu walio majumbani,ila hata majumbani kuna wahitaji wengi sana wa internet.

Nimepata solution kwa wakazi wa DAR baada ya sakanya sakanya nimepata utatuzi,kwa yeyote anaehitaji internet (UNLIMITED) akaribie PM tuelekezane namna ya kupata hiyo huduma.

Survey ni bure kuja kutembelea eneo ulipo ili kuona na kujua mahitaji gani yatahitajika ili upate huduma,huduma hii ni popote kwa wakazi wa DAR.

Gharama sio kubwa inategemea tu na mahitaji ya vifaa vitakavyohitajika kufikisha mtandao eneo lako. Ndio mana survey ni muhimu (na ni bure).

Malipo ya mwezi ni 150,000 (hizi ni daily monthly cost) tofauti na zile cost za material za mwanzo,hizi 150k ndio gharama ya net kila mwezi.

Kwa maulizo yote tuulizane kwenye comment PM akaribie anae hitaji huduma,Hela ni mwisho wa mwezi,Ukiungwa internet Leo utatumia mpk mwisho wa mwezi ndio utalipia 150k.

Haina janja janja wala unga unga hela yako baki nayo mfukoni kula maisha ikifika mwisho wa mwezi unalipa,Simple and Easy.

Speed ni uhakika unapata Above 5Mbps,zilizo nyooka zisizo na longo longo,streaming ndio kbsa,wale wazee wa movie downloading kama bwana Movies Store wanaelewa nini namaanisha.

d.png


Karibuni wote.

OFA

Kwa atakaeweza niletea wateja wa 5, sio lazima wewe uwe mteja ukiweza nitafutia wateja wa 5 Nakupa Offer ya kuku unganisha na internet Free popote utakapokua ndani ya DAR, hutochajiwa gharama za instalation wala vifaaa,itakua free. PLUS 1 month Free na sio lazima wateja wa 5 at a time,hata ukileta kila baada ya miezi mteja m1 nakuhesabia,wakifika wa 5 Unapata OFA yako (kwa wahitaji tu lakini).
 
Kama ni biashara legit ungeweka kila kitu wazi.

Sio kila mtu anapendelea kufuatana PM.

Unaweza kosa wateja wengi potential kisa unakimbizia watu PM.
 
Mzee unafanya ghali sana mimi naishi Posta na Home tumefunga hiyo Internet ya UNLIMITED Kwa Mwezi Tunalipa Elfu 70 tu Na Tunapewa 30Mbps per second mkuu
 
Mzee unafanya ghali sana mimi naishi Posta na Home tumefunga hiyo Internet ya UNLIMITED Kwa Mwezi Tunalipa Elfu 70 tu Na Tunapewa 30Mbps per second mkuu
Usipojali weka jina la kampuni tu. Turkey nao hewani
 
Mzee unafanya ghali sana mimi naishi Posta na Home tumefunga hiyo Internet ya UNLIMITED Kwa Mwezi Tunalipa Elfu 70 tu Na Tunapewa 30Mbps per second mkuu
gharama inategemea na eneo mkuu na nani kampuni inayokufungia hiyo huduma.

gharama halisi za hii kitu hazipo costant,hii ni biashara kama huduma ya umeme tanesco

sio kila mteja atapata umeme kwa gharama wanazotangaza,kuna vitu vingi vinavyoleta TOTAL ya nini ulipie ili upate huduma.
 
5Mbps per second ni ndogo sana tena kwa 150k

Samahani Lakini
Bila samahani boss,hii biashara sio tu ya kuangalia number mkuu kuna vitu vingi vinavyoleta gharama husika unayotakiwa kulipia kwa speed tajwa.
 
Kama ni biashara legit ungeweka kila kitu wazi.

Sio kila mtu anapendelea kufuatana PM.

Unaweza kosa wateja wengi potential kisa unakimbizia watu PM.
ni kweli ila hamna mtu anapenda namba yake personal iwekwe hadharani kisa tu eti n mteja

na si kila mtu ni mteja mkuu,kuna wale watest mitambo,unapowambia watu waje PM kuna namna

unawachuja watu walio serious na wale changamsha ubongo,sio kwa ubaya PM n muhimu mkuuu
 
Back
Top Bottom