Wakazi wa Dar watadharishwa kukosa huduma ya Maji Septemba 23

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
TAARIFA KWA UMMA

KUZIMWA KWA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU CHINI

20.9.2022

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini kuwa Mtambo utazimwa siku ya ijumaa tarehe 23/9/2022 kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 2 usiku

Sababu: Kuruhusu matengenezo makubwa ya bomba kuu maeneo ya Mlalakuwa na Mwenge.

Maeneo yatakayo athirika ni pamoja na; Bagamoyo, Zinga, Kerege, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni,Kigamboni Vingunguti, Ilala na Katikati ya mji.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaotokea.

Tafadhali kumbuka kuhifadhi maji ya kutosha ili kuwa na hifadhi ya kutosha kipindi cha matengenezo
 
Hii dawasa hatuijui ni maji ya kisima tu kama tuko vijijini
 
Hiki ni kichekesho au dhihaka kutoka kwa DAWASA?😂😂

Yaani wanatoa notisi ya maji kukatika wakati yanakatika kila siku? Tena yanakatika hata wiki nzima baadhi ya vipindi
 
Mie Jana nimepiga simu halmashauri wakaniunganisha na engineer wa wilaya niliopo engineer wa maji akasema nipe muda kidogo maji yataanza kutoka hapo mpaka sasa hakuna maji siku ya tatu hii daaaah Tanzania yangu hii
 
Mbezi Louis ni kawaida sana na hakuna taarifa kutoka Mamlaka husika.

Kuna sehemu nyingine watu hukata mabomba, lakini DAWASA imejitahidi sana kuhakikisha Dar ina maji...

Ungeishi Dar ya zamani, kwenye suala la maji kwa sasa Dar walau ni nusu pepo...
 
Mie Jana nimepiga simu halmashauri wakaniunganisha na engineer wa wilaya niliopo engineer wa maji akasema nipe muda kidogo maji yataanza kutoka hapo mpaka sasa hakuna maji siku ya tatu hii daaaah Tanzania yangu hii
Hamieni masaki na ndoo zenu huko hakuna maji kukatika.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom