Naishi Dar huu mwaka wa 15 sasa kiufupi sio mgeni na huu mji,lakini nimeona mara nyingi sana yanapotokea matukio ya uporaji hadharani watu hawatoi msaada,iwe unaibiwa,unashambuliwa na vibaka au vp huwezi kuona watu wakisaidia ktk hilo,hili limekua tofauti na mikoa niliyowahi kuishi,nikija ktk tukio la huyu mwanafunzi wa diploma wa chuo cha Kampala (KIU) aliyeuwawa kwa kuchomwa na visu inasemekana watu walikuwepo na wakati huyo binti anahangaika kupata msaada kutokana na majeraha aliyosababishiwa ambayo yamepelekea mauti yake hakuna aliyesogea hii inaumiza sana,huku maeneo ya gongo la mboto kiufupi vibaka ni wengi kupita maelezo lakini huwezi sikia wameshikwa,Mimi binafsi waliwahi kujaribu kunipora bahati nzuri niliwazidi nguvu na mmoja wapo nilimfahamu nikamtafuta kwa muda wangu na kumtia adabu,hizi tabia zinakera wengi mtasema hamtaki ushahidi polisi wa kumsaidia mtu ila ni bora uokoe maisha ya mtu kwanza,damu ya huyo binti wa KIU itawalilia waliohusika ila hizi za kushindwa kutoa msaada zinakera kupita maelezo.