Mkasa wa Kweli: Nilivyookoa maisha ya Watalii toka Finland

leadermoe

R I P
Feb 15, 2017
1,392
4,573
Wakuu heshima kwenu!
Napenda kushea nanyi simulizi ya maisha yangu . Hii sio hadithi ya kutunga, nimelazimika kutumia majina ya kutunga ili kuleta maana. Pia nimetumia codes nyingi sana hapa ili kuepusha watu wanaonifahamu ku connect matukio. Kuna baadhi ya matukio nimeyabadili kidogo ili kujaribu kuleta ugumu wa watu kujaribu ku connect.

Tuanze sasa.......

Sehemu ya 1:
Naitwa leadermoe, nimelelewa na mama tu. Baba alikuwa anafanya kazi mkoa wa Iringa sehemu moja inaitwa 'kitete' na alikuwa anafanya kazi TAZARA (Tanzanian and Zambia Railway) way back.

Baada ya kumaliza form 4, nikawa niko mtaani tu nikisikilizia matokeo. Mzee alikuwa anamiliki nyumba za wapangaji sehemu moja inaitwa 'sakina' so mimi nikawa ndio bosi wao by that time. Maisha home yalikuwa safi kiaina sio ile saana, ila michuzi ya kutesea mtaani ilikuwa haikauki.

Nilikiwa na tabia ya kufanya jogging asubuhi saa 11 kila siku, natoka hapo home sakina mpaka pale habari maalum ngara. Kama kawaida sikuwa na kampani kubwa ila ni wanangi wanne tu ndio nilikuwa najiachia nao. Ila jogging wawili walikuwa wavivu so nilikiwa nakutana na mwenzangu pale sakina super market tunaliunga mdogo mdogo mpaka ngara.

Siku moja nimetoka zangu home saa 11:00 nashuka mdogo mdogo, kuna semehu kuna shamba kubwa la migomba so huwa panakuwa na giza sana. Nilipokaribia hilo eneo nikaona gari nyeusi imesimamishwa kwenye hilo shamba la migomba. Kipindi hicho Arusha ujambazi uko juu sana ila sikuwa na hofu maana mida hiyo kuna watu wanaokwenda kufata nyama pale Arusha meat wanakuwa njiani.

Nikapunguza mwendo ili nijue lile gari ni la nani na kwa nini liko migombani kama limefichwa vile. Honestly i was curious to know what was going on kwa vile lile shamba lilikuwa linapakana na nyumba zetu (kwa wapangaji wetu). Sikufanikiwa kulikaribia gari maana nilihisi kama limeibiwa naweza pata matatizo na vyombo vya dola, au kama kuna mpuuzi kajificha pale ili wanyanduane. Ilikiwa kawaida sana kukuta mtu amepaki anakula mzigo maana njia yenyewe haikuwa busy sana na migomba ilikiwa mingi that area so nikang'oa kwendelea na hamsini zangu.

Nilikutana na mwangu (yeye alikuwa anakaa mianzini) pale point yetu tukaunga mpaka kwa idd akasema hayuko poa so tukarudia hapo. The idea was twende home maana ni karibu zaidi kuliko kwao ili akapumzike kwanza. Wakati napandisha na mwana tukalikuta lile gari pale pale, nikamtonya mwana ila tukashauliana tusisogee maana tulihisi tu limeibiwa so hatukutaka kujitafutia matatizo. Ilikuwa 12:30 wakati tunarudi, mwana alioga then akanywa paracetamol akalala. Mimi nikatoka ili nikaangalie kama ile gari bado lipo surprisingly ikawa iko pale pale, this time nikaisogelea maana tayari kulikuwa kumeshapambazuka so watu wako njiani wengi tu.

Nilipokaribia nikachungulia mbele nikaona mtu amekaa ananiangalia ila amefungwa kitambaa mdomoni. Alipo niona akawa anatikisa kichwa tu mwili umekaza so nilitulia pale huku najiuliza nifanyeje. Nikapata ujasiri wa kusogea karibu, nikamuona vizuri alikuwa ni ngozi nyeupe ila amekuwa mwekundu kutokana na kamba alizofungwa. Akanipa ishara nikafungua mlango wa mbele, nilimkuta amefungwa kwenye siti ya dereva, miguu imefungwa kamba, amekalishwa kwenye siti na mikono imefungwa nyuma ya siti. Kamba zilipita karibu na mabega so alishindwa hata kujitikisa kwa jinsi manila zilivyokuwa zimebana.

Mdomoni alifungwa kitambaa ili asipige kelele. Mpaka wakati huo akili ilisimama nisijue la kufanya, ghafla nikapata ujasiri wa kumfungua kitambaa cha mdomoni ndipo akaanza kuongea ila kinyonge sana. Baada ya kumfungua kamba zote, na yeye akajaribu kushuka kwenye gari ila akashindwa kusimama akajimwaga chini. Nilisaidia mkumkalisha akaegemea gari, akawa ananiambia 'my wife and my daughter ' mwanzo nikajua ni wenge tu ila nilipomwangalia kwa makini nikajua kuna kitu anamanisha so nikachungulia tena nyuma ya gari (ilikuwa ni prado zile za milango 5). Siti za kati hakukuwa na watu nilipochungulia kwenye buti nikakuta viumbe wawili mwamefungwa kitaalam na wamekunjwa na kulala chini.

Hapo ikanibidi niwashtue jamaa flani walikuwa wanapita, wakaja ila wakaniambia dogo umeshanunua kesi, tena watu wenyewe wazungu. Basi mzee mmoja akashauri kwa kuwa wahusika wako hai, tuwasaidie tu hata wao wataeleza polisi kuwa tumewapa msaada tu. So tukawafungua na kuwashusha. Alikuwa mama wa miaka kama 32 hivi na binti alikuwa na around 16 yrs. So ukafanyika utaratibu wa kumtafuta balozi, akaenda kutoa taarifa polisi so ikaja difenda ikawapeleka mount meru.

Kimbembe kikaja tulipotakiwa kwenda kutoa maelezo polisi, watu wote wakanipoint mimi kua ndie mtu wa kwanza kuwaona, na yule mzee alietoa ushauri akajitolea kuungana na mimi so tukapelekwa central pale. Tumechukuliwa maelezo yetu pale ila tukazuiliwa hakuna kutoka mpaka wale victims watoe maelezo yao. So tukawekwa chumba flani hapo na ulinzi ukawepo ila chai na chakula mchana tuliletewa fresh kabisa. Tatizo tu hakuna uhuru wa kutoka hapo. Baada ya kama dakika 20, yule mzee akaitwa nikabaki mwenyewe. Alitumia kama nusu saa kule then akarudishwa ila this time alikuja na mkuu wa kituo. Akawa amekaa pembeni yangu wakati mkuu wa kituo ananihoji. So baada ya maswali mengi, tukaambiwa tusiwe na wasiwasi, wakishapata maelezo ya wale wageni watajua nini cha kufanya so tuvute subira. (ila wakati huo wote yule mzee alikuwa ananihoji vimaswali vya kunipima anacheka nikajua tu ananitoa uoga ili nione ni jambo la kawaida).

Ilipofika saa 8 tukaitwa ofisi ya RPC, yule mzee akapewa kiti kwa heshima tu na pole juu toka kwa RPC mwenyewe, (baadae nilikuja kufahamu, yule mzee alikuwa ni Kanali wa JW alikuwa amestafu mwaka moja nyuma. Kumbe hata wakati ule ameitwa na mkuu wa kituo alijitambulisha wakaridhia yeye aende ila nibaki mimi kusubiri maelezo ya wale wageni ila mzee alikataa kwa kuwaambia akiniacha watanisumbua so hata yeye atasubiri). Wakati tunaongea yule mzungu akaletwa na askari mle ofisini, so tukawa watu watano. (RPC, Mzee Kanali, Leadermoe, mzungu na mkuu wa upelelezi wa mkoa).

Yule mzungu walikuwa wameshamhoji na amenyoosha maelezo. Maana aliwaambia mimi ndie nimewaokoa maisha yao so sikupaswa hata kukalishwa pale kituoni. Ripoti ya Dr. Ilisema wako salama, hakuna alieumia sana ila ni maumivu tu ya kamba na vibao walovyopigwa tu basi, wakati huo simu ya upepo ilishapigwa makao makuu ya polisi, wamewataarifu ubalozi husika so ikabidi wapelekwe Hotelini kusubiri taratibu zingine.

Baada ya maongezi mengi tulirudishwa na difenda nikakabidhiwa kwa mama then wakampeleka mzee kanali kwake. Nilikmkuta mama ametulia tu hana furaha kabisa, baada ya polisi kumweleza kilochotokea kisha wakaondoka. (Lengo la kunirudisha mpaka home ni ili wapajue endapo kutakuwa na taarifa tofauti waweze kuniibukia fasta). Ile gari iliyohusika iliikodiwa na wale watalii toka Dar na walikuwa na safari ya kwenda serengeti.(Mwanaume alikuwa amekuja mara kadhaa Tz so hakuwa mgeni sana). Kesho yake wale wazungu walipelekwa na polisi pale KiA wakasepa Dar.

Kumbe walijichanganya katika maongezi wakiwa moshi wakatoa codes kadhaa, kumbe kuna jamaa walizifungua codes then wakawawekea radar. Walitoka moshi saa 9 Alasili ili wakalale Arusha then kesho waingie Ngoro ngoro, wale jamaa wakaunga tela. Kufika Arusha akalengeshwa jamaa mmoja ili awe nao karibu, so wakaenda hotel moja pale sakina wakachukia room. Mida ya saa 1:30 jamaa akatoka na familia yake kwenda kushangaa mji kidogo, wakati anarudi kama saa 3 hivi jamaa wakam tight pale round about ya frolida.

Mchezo ukawa hivi, jamaa wakajidai corola yao imezima barabarani so wakawa wamemblock jamaa. Kutokana na ugeni akawa amesimama ili atafute namna ya kupita(hapa nimesema kutokana na ugeni kwa kuwa hakuwa anajua njia zingine za kutokea. So alikuwa anafata njia aliyoshuka nayo ile ya mianzini to stand kubwa) kosa alilofanya ni kushusha kioo, kumbe jamaa mmoja alikuwa nyuma ya gari yake, hakumuona maana mawazo yalikuwa mbele kwa ile corola, so akanyoshewa chuma usoni aka unlock milango jamaa moja akatoka kwenye corola akafungua mlango wa dereva akamshusha mzungu then mzungu kakaa nyuma na familia yake wakiwa guarded na yule gun man.

Ngoma ikala moto mpaka pale migombani nilipowakuta. Jamaa walichukua mali zao zote ziliachwa passport tu. Pesa, cameras, laptops, nguo, viatu na zaga zao zote wakasepa nazo. Polisi wali fanya kazi yao, baada ya siku 5 wakamdaka yule 'gun man' alitaka ku push camera na laptop kwa boss mmoja kumbe jamaa wako radar wakamdandia. Baada ya kuhojiwa akanyosha maelezo kesho yake wale wengine wa2 wakadakwa so wakawa wa3. Kumbe hawakuwa hata na cha moto ni akili tu alitumika kwa yule 'gun man' kushika toy.

NB: Wakuu huu mkasa nimeshauandika kwa 75%. Hakuna arosto, nipatapo mda Nashua episode.

Niambieni muda mzuri wa kuiweka ili tuisome ikiwa ya moto bado. Unaruhusiwa kuuliza swali lenye staha.

JBourne59 Antonnia Bantu Lady National Anthem Intelligent businessman Dahan Analyse sophy27 sumbai Kapachino reymage Numbisa Karibuni na wengine pia
Antonnia Bantu Lady Kalpana Gily kaburungu Kibunango Lastmost wao ni wao Mpetde Santos06 To yeye niachiemimi JBourne59 harakati za siri Aaliyyah Lovelovie Semere92 mludego mwonge Smart AJ Mwana Mwanga Mkali sumbai @Zeus1 Rashidi Jololo barakalyimo Iceberg9 ERoni Dahan Mwananchi B Watu8 liwaya Ushimen madindigwa The email Gamaha IBRA wa PILI Kaka yake shetaniKoffi Annan macho_mdiliko
premji canoonhamachoachila ceez
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom