Wakati JPM alijenga uwanja mkubwa wa kimataifa wa ndege Chato, ambao hakuna ndege inayotua zaidi ya kunguru, shule ya wanafunzi 1500 haina choo

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,003
20,681
Ni hapo hapo Chato. Aliwajengea uwanja wa ndege ambazo hata nauli hawana, bado wanatumia punda. Pia baada ya kuwajengea uwanja huo, watoto wa wana chato wanaknya vichakani.

Kalemani atupishe, tangu JPM aondoke,hakuna alilofanya
Screenshot_20240214-155718.jpg
 
Ni hapo hapo Chato. Aliwajengea uwanja wa ndege ambazo hata nauli hawana, bado wanatumia punda. Pia baada ya kuwajengea uwanja huo, watoto wa wana chato wanaknya vichakani.

Kalemani atupishe, tangu JPM aondoke,hakuna alilofanya
View attachment 2903903
JPM ukurasa wake umeshafungwa, naona bado mzimu uñakutembelea na kukufanya uweweseke.

Pambana na akina Makonda ili pesa wanazotumia kwenye maigizo wajengee vyoo.
 
SIR- 100 alikuwa Makamu wa Rais, Philip Mpango alikuwa waziri wa fedha, Naibu waziri mkuu alikuwa Waziri wa Madini, Majaliwa alikuwa waziri mkuu.

Tusidandanyane sio Kila mwanaccm hana akili
 
JPM ameshakufa...; Vipi hio shule ina vyoo kwa sasa ?!!!!

Bora mapesa kutupwa Chato kuliko sasa hivi zinatupiwa kwenye akaunti za watu pasipojulikana....

Ni kama zimwi ambalo halikuli likakwisha sasa hivi hili zimwi linatumaliza.....
 
Hiyo shule haina kamati ya shule? haina uongozi wa kata? Hao watoto/wanafunzi hawana wazazi?
Kuna vitu vingine ni kujidekeza tu havina haja eti kuililia serikali
 
Back
Top Bottom