Wakaka, Waume..

Tank you so much ...

one more question ..
Je we unadhani inapendeza zaidi kwa sisi kuwaambia tunataka nini au nyie mfanye lolote..?

My dear I miss you too..
Nafurahi kukutana nawe hapa tena ..
Dah hapo ni pagumu kidogo ila naturally wanawake wengi duniani wanapenda kuwa submissive na wengine wanafantasize hali hii kabisa (hii inathibitishwa na kitendo cha kufanya mapenzi ambapo wanaume huwa sterling kwa 80%. Hali hii ndio inaendelea hata kwenye mambo mengine ya kawaida. Ila kwa mtazamo wangu mi naona kwamba,
  • Ni vizuri kumwambia mtu wako what u feel and what you want ingawa usilazimishe unachokitaka kitokee kila wakati.
  • Kuna baadhi ya wanaume wanataka kifanyike kile tu wanachotaka wao ingawa ukweli ni kwamba ukimwambia hata kama hatafanya wakati huo na no matta how much hard he is next time atafanya.
  • So for me simply be free to say what you feel and what u want your mtu akufanyie
 
306085_2686294608816_1599953016_1798474_556756354_n.jpg

Ooh poor me.Thanks smile for that,ni vizuri kupeana matumaini na tukumbuke ....we only lives once but if we live right once is enough......vinginevyo unaweza kuja kukata rufaa kwa baba mungu wetu kwamba nilisahau kuishi ile mara ya kwanza naombaa nafasi nyingine tena,kwa sababu ya haya mauzauza ya dunia.Just be happy smile regardless
 
ni juzi mama alinipigia simu na kuniambia ''leo ni siku yako ya kuzaliwa'' hbday mwanangu....nikamwambia asante mama likini ukweli ni kwamba katika kichwa changu hili halikuwepo kabisa na sijawahi kulikumbuka ....

Mkuu Edson swali langu ndo linakuja hapo..
Je ni kwanini huwa hamkumbuki vitu hivyo ?
 
Dah hapo ni pagumu kidogo ila naturally wanawake wengi duniani wanapenda kuwa submissive na wengine wanafantasize hali hii kabisa (hii inathibitishwa na kitendo cha kufanya mapenzi ambapo wanaume huwa sterling kwa 80%. Hali hii ndio inaendelea hata kwenye mambo mengine ya kawaida. Ila kwa mtazamo wangu mi naona kwamba,
  • Ni vizuri kumwambia mtu wako what u feel and what you want ingawa usilazimishe unachokitaka kitokee kila wakati.
  • Kuna baadhi ya wanaume wanataka kifanyike kile tu wanachotaka wao ingawa ukweli ni kwamba ukimwambia hata kama hatafanya wakati huo na no matta how much hard he is next time atafanya.
  • So for me simply be free to say what you feel and what u want your mtu akufanyie

Nimependezwa sana na majibu yako yote..
ila vitu kama hivi mi naona ujitahidi sana kukumbuka mwenyewe.
jiwekee reminder kwenye calender kazini au kwenye cellphone or laptop.
inapendeza zaidi kwa nyie kutokuambiwa na kufanya tu. maana saa nyigine
kuna wanawake wenye "short temper" ambao wanatarajia high standard kutoka
kwa wenza au watu wao wa karibu ."mi mmoja wapo" watu kama sisi huwa kuwakumbusha
kila mara au kila mwaka inaleta hasira fulani hivi na inaonyesha you don't care. maana huwa
sisi tunatimiza kipengele chetu..

sasa utawapa ujuzi gani wanaume wenzako ili waweze kukumbuka?
au nini kiwasaidie kukumbuka?
 
Mimi wala sikumbuki huwa wife ndo ananikumbusha, imagine hata birthday yangu wife anaikumbuka kuliko mimi.

Mungu ambariki sana mke wangu, kweli wanaume wengine tuna bahati kupata wanawake wanao tupenda, na wanao tuheshimu, asante sana mungu kwa kunipa mke mwema :cool2:
 
Mahakama kuu na kesi yenyewe ni ya kudanganya matukio. Ulipaswa uwe somewhere ila ukaenda kwingine na hukuonekana.
Je huwa unakumbuka birthday ya mchumba au mpaka ukumbushwe kwa kengele

Rocky, Rocky TF ka kimbia wapi tena??
 
Mimi huwa nakumbuka. Lakini kwa kweli kwangu personally birthday haina uzito sana. Yaani hata ikitokea akasahau im ok.

Thats me. Honestly. Ila anniversary za ndoa zina uzito wake. . . . .
 
wedding anniversary, Birthdays, etc..

Naomba kuwa uliza wakaka na waume wa hapa Je ni kwamba
hamkumbuki siku kama hizo au hazina umuhimu sana kwenu..?

Na Je mnataka tuwe tunawakumbusha siku hizo zikikaribia au??

Samahani kwa thread fupi I hope mmenielewa..
Asanteni.

Hallo AD.Hujambo mami wangu? Nafurahi kukuona tena hapa MMU baada ya kusoma thread moja kwamba ulikutana na Ban Ki Moon. Kama ni kweli pole sana na karibu 'home' yetu ya JF.Turudi kwenye thread yako.

Saikolojia ya wanaume inatofautiana sana na ile ya wanawake.Mtazamo, mwelekeo na mawazo ya mwanaume ni je, napambana na maisha ipasavyo? Ni wapi kuna deal safi zaidi kuliko hili la sasa? Mawazo haya yanamzamisha kwenye dunia yake peke yake na ni vigumu kwake kutoka huko na kuzingatia jambo tofauti. Mwanamke yeye mawazo yake ni kutunza, kupendezesha na kuratibu. Ndo maana ni rahisi sana kwa mwanamke kukumbuka sikukuu ipi inakuja tarehe ipi na kama amejiandaa ipasavyo: mavazi, mlo nk. Wanaume wengi hawapo kabisa kwenye hii dunia ya ceremonies/festivals. Kwa hiyo AD usiwashangae sana wakaka na wababa kwa kushindwa kwenda sambamba na mabirthday nk. Halafu kumbuka tunaishi Tanzania ya mwaka 2012 ambayo sh 10,000 huwezi kwenda nayo sokoni kariakoo kutafuta mahitaji ya mlo wa jioni na kutoka ukiwa na furaha! Wanaume wana msongo wa mawazo, na mapressure makali.Hiyo birthday yako itakaa kwenye kichwa kipi? Hapa nazungumzia kwa ujumla tu jinsi hali ilivyo.Wengine hata ukimkumbusha inakuwa ugomvi.

Kwa hiyo AD ni vitu viwili ndivyo vinawakorofisha akina kaka na wababa: jinsi walivyoumbwa na hali mbaya ya uchumi.
Birthday yako lini nikutumie mkungu wa ndizi toka Moshi.
 
Mimi wala sikumbuki huwa wife ndo ananikumbusha, imagine hata birthday yangu wife anaikumbuka kuliko mimi.

Mungu ambariki sana mke wangu, kweli wanaume wengine tuna bahati kupata wanawake wanao tupenda, na wanao tuheshimu, asante sana mungu kwa kunipa mke mwema :cool2:

Ukipata mke mwema umejipatia kilicho chema sana, maisha yako yote yatajawa na amani! Ila nawe sasa uendelee kumtunza, kumheshimu na kumpenda. . . .
 
Hongera sana mkuu..

Unaonaje mwaka huu we ufanye suprise ??
si kukumbuka tu siku tamu kati yenu bali kumshukuru
kwa yeye kukumbuka kila mwaka?
 
Nimependezwa sana na majibu yako yote..
ila vitu kama hivi mi naona ujitahidi sana kukumbuka mwenyewe.
jiwekee reminder kwenye calender kazini au kwenye cellphone or laptop.
inapendeza zaidi kwa nyie kutokuambiwa na kufanya tu. maana saa nyigine
kuna wanawake wenye "short temper" ambao wanatarajia high standard kutoka
kwa wenza au watu wao wa karibu ."mi mmoja wapo" watu kama sisi huwa kuwakumbusha
kila mara au kila mwaka inaleta hasira fulani hivi na inaonyesha you don't care. maana huwa
sisi tunatimiza kipengele chetu..

sasa utawapa ujuzi gani wanaume wenzako ili waweze kukumbuka?
au nini kiwasaidie kukumbuka?
I will be honesty here, if you love someone you will never forget anything important for him or her yaani you dont even have to write it anywhere. Ntakuwa mkweli hapa mi nimewahi kupenda just once na huyo mtu niliyekuwa nampenda nakumbuka everything about her tena without writing it anywhere, i even remember the first day she said yes to me, the first day we kiss na kila kitu tena kwa tarehe, saa na mwaka ijekuwa birthday!

Kuna kupitiwa nakubali hasa mtu anapokuwa na shughuli nyingi but believe me kama anakupenda kwa dhati hatasahau kitu chochote muhimu kwako. Ila sasa wanaume wanakwepa sana gharama so wakati mwingine wanajitahidi kadri iwezekanavyo kuzikwepa halafu cha ajabu ni kwamba hukwepa gharama kwa watu wao wa kudumu acha vile vi one night stand huko wataspend balaa.

Just remind him kama unaona kweli kabanwa na kasahau kuna kupitiwa pia u know we are not psychics tujue this year kwenye birthday yako unataka nikufanyie nini!Tell me what you want me to do and no real man will say no.

Kwa wanaume wenzangu, najua sisi kama wanaume huwa hatujali sana vitu vidogo kama anniversary na birthdays but women do na hapo ndipo hujua kama unawajali ama la na believe me women love men who care for them, watch out kama akitokea mtu aka fake ku care umekwisha
 
Ukipata mke mwema umejipatia kilicho chema sana, maisha yako yote yatajawa na amani! Ila nawe sasa uendelee kumtunza, kumheshimu na kumpenda. . . .
Kabisa kabisa mungu anizidishie amani, yani niko happy sana na wife....Huwezi kuamini mara nyingi sana mimi ndo balaa, yani lazima nimchokoze wife napenda nimuone kakasirika, lakini wapi wala hakasiriki ananiombea dua kwa mungu, anasema naomba mungu akutulize :cool2:
 
Hallo AD.Hujambo mami wangu? Nafurahi kukuona tena hapa MMU baada ya kusoma thread moja kwamba ulikutana na Ban Ki Moon. Kama ni kweli pole sana na karibu 'home' yetu ya JF.Turudi kwenye thread yako.

Saikolojia ya wanaume inatofautiana sana na ile ya wanawake.Mtazamo, mwelekeo na mawazo ya mwanaume ni je, napambana na maisha ipasavyo? Ni wapi kuna deal safi zaidi kuliko hili la sasa? Mawazo haya yanamzamisha kwenye dunia yake peke yake na ni vigumu kwake kutoka huko na kuzingatia jambo tofauti. Mwanamke yeye mawazo yake ni kutunza, kupendezesha na kuratibu. Ndo maana ni rahisi sana kwa mwanamke kukumbuka sikukuu ipi inakuja tarehe ipi na kama amejiandaa ipasavyo: mavazi, mlo nk. Wanaume wengi hawapo kabisa kwenye hii dunia ya ceremonies/festivals. Kwa hiyo AD usiwashangae sana wakaka na wababa kwa kushindwa kwenda sambamba na mabirthday nk. Halafu kumbuka tunaishi Tanzania ya mwaka 2012 ambayo sh 10,000 huwezi kwenda nayo sokoni kariakoo kutafuta mahitaji ya mlo wa jioni na kutoka ukiwa na furaha! Wanaume wana msongo wa mawazo, na mapressure makali.Hiyo birthday yako itakaa kwenye kichwa kipi? Hapa nazungumzia kwa ujumla tu jinsi hali ilivyo.Wengine hata ukimkumbusha inakuwa ugomvi.

Kwa hiyo AD ni vitu viwili ndivyo vinawakorofisha akina kaka na wababa: jinsi walivyoumbwa na hali mbaya ya uchumi.
Birthday yako lini nikutumie mkungu wa ndizi toka Moshi.

hahahahahahaahah lohhh
Kwanza asante sana kwa majibu yako ambayo yaani
umeyaeleza kwa kina sana tena sana. Na niimecheka
kupita kiasi sante my dear HYGEIA..

Pili ni kweli nilikuwa Lupango kwa muda kidogo lakini sasa
nimerudi. asante tena kwa kunikaribisha..

Anyway ..
umesema na kuongea mengi sana..
kwa kiasi fulani na kubaliana nawe na kwa kiasi fulani
naona mna make "excuses" kwa dunia hii ya sasa unakuta
baba doctor mama lawyer wote ni mkumku wa kutafuta ridhiki
kujenga maisha yao.. lakini ikija kwenye vitu kama hivyo ni mama anaekumbuka
na wote mko busy .. we unaonaje hapo mkuu wangu Hygeia?

HAlafu naomba sana huo mkungu wa ndizi ndugu yangu
anwani yangu ni .

Afro mwana wa Denzi
Po.Box 8462
Sweethome
Jamii forum .
 
Mkuu Edson swali langu ndo linakuja hapo..
Je ni kwanini huwa hamkumbuki vitu hivyo ?

Tuko bussy kutafuta chapaaaaaa mama AD....na tamaduni ya mtanzania na mwanamume pia vitu kama hivyo ni nadra sana kukumbuka sana saaaana utakumbuka mtoto lini anaenda shule ngoja nianze kutafuta ada.
 
Back
Top Bottom