Mbinu mpya za wizi na utapeli

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
story fupi, tamu na yenye kufundisha soma hadi mwisho

Ni Kawaida Sana kupita sehemu ukasikia tangazo la mtu kununua pesa za kigeni pesa mbovu au pesa za zamani yes pesa hizi zinanunuliwa kulingana na thamani mfano elfu 10 mbovu atakupatia elfu 8 yeye akipeleka bank anapata elfu 10 Ile Ile na yeye anakuwa kapata faida ya shilingi elfu 2 maana bank hawakatai pesa eti Kisa mbovu

Je umewahi kusikia kuwa pesa hizo (Mia tano) za zamani kuna watu wananunua na kuna wengine wanatangaza kuwa wananunua mpaka shilingi milioni Moja kwa noti Moja ?

Ngoja kwanza nikupe darasa kidogo

Ukweli ni kwamba hizo hela hazina Kazi yoyote na hakuna anaezinunua Ila wajanja wenzangu watoto wa town kila kukicha wanaamka na akili ya kupata pesa maana Ajira zenyewe hakuna na kama unavyojua wajinga wa kuibiwa mjini huwa hawaishi

Wanachofanya anatokea mtu mmoja anatangaza ananunua hizo noti kwa shilingi elfu 2 kila Moja

Yoyote aliekuwa nazo atajitokeza tuu Kisha watakuja kununua kwako Kwa labda watasema wanataka noti 20 jumla watakupatia shilingi elfu 40 Kisha watakuacha unachelelea na wao watajifanya wajinga wanaondoka na hizo noti Kisha watachukua namba zako na kukuomba ukipata noti nyingine uwapigie

Baada ya siku 3 utapigiwa simu na mtu yoyote (kumbuka walichukua namba zako ) kisha atajitambulisha kuwa ni wale wanaonunua za zamani za Shilingi Mia 5 na wanaomba kama ukipata nyingine uwaambie maana kwa sasa wamepata soko kubwa zaidi na watanunua kila noti kwa shilingi elfu 50 badala ya shilingi elfu 2 ya mwanzo

Kwanza ukiskia Hivi utawaamini maana walishakuja kwako kununua na hawana longo longo so kisaikorojia watakuwa wakekupa Kazi mbili

Kwanza kutafta hizo noti kwa udi na uvumba pili utakuwa tayari ata kwenda kukopa pesa ili ununue hizo noti mtaani Kisha uje kuwauzia hao matajiri

Baada ya kukata tuu simu Jioni ya siku hiyo eidha kuna kijana atakuja kwenu au pale mlipokutana na wateja wako wa mwanzo akiwa na noti za Mia 5 za kutosha tuu Kisha atakuulizia umsaidie kutafta soko kama unajua zinaponunuliwa ( kumbuka wateja wa mwanzo ulikutana nao kwako au kijiweni kwako so wanajua pa kukupata) na kama mlikutana tuu mtaani basi utapokea simu toka Kwa mtu atasema anazo noti za Mia 5 za zamani na anaomba umtafutie soko ila yeye anataka elfu 20 tuu kwa kila noti

Wewe ukipiga hesabu wateja wako pendwa mwanzo walinunua kwa elfu 2 yaani Katika noti 20 zenye thamani ya shilingi elfu 10 wao walikupa elfu 40 na Kwa sasa wanataka kila noti kwa shilingi elfu 50 yaani kwa noti 20 za Mia 5 ya zamani zenye thamani ya shilingi elfu 10 wao watalipa jumla ya shilingi milioni Moja

Hapo ndio unaamua kukopa pesa unanunua hizi noti za huyu aliekuja kukuomba umtafutie soko maana zake anauza kwa elfu 20 kila noti tena unanunua zote ili ukauze kwa elfu 50 kwa kila noti maana wateja wako nao wanapiga simu kila mala kuulizia ila usichofahamu ni kwamba wote Lao Moja na ukishatoa hela ukanunua hizi noti za huyu jamaa kwa Lengo la kuja kuwauzia wateja zako basi ishakula kwako yaani wakipata taarifa ushanunua tuu maana yake hela yao imerudi na faida juu na kuanzia hopo unakula block adi kwenye komwe lako kwakuwa walikupatia elfu 40 mwanzo ukajiona mjanja ila wao wamekuuzia tena zote kwa shilingi laki 8.

Credit New Katoto
View attachment 2705321
 
Mimi kwa ujinga huu unitapeli, yani asubuhi muitaji apige, jioni aje muuzaji, anayeibiwa kwa hivi ni fala fala fala kabisa.
 
Ahsante kwa somo zuri, agiza soda popote ulipo nakuja kulipa! 🙏
 
Dah, saa kumi kapita dada mitaa karibu na napofanya kana PA inasema ananunua hela mbovu na hela za kigeni.
 
Back
Top Bottom