pro-chadema jf wanajadili mambo ya ccm kwa umakini mkubwa halafu hawa hawa watakuja kuipigia kula ccm.
Hizo ni husika tu! Pitia taarifa kwa umma hapa: Faustine's Baraza
Acha dharau kwa Wasiisra wewe....Wassira ni kichwa, huoni alivyofanikiwa kutengeneza mgogoro wa kidini Mwanza ili wapate sababu ya kusema kuwa vurugu hizo zinatokana na 'Ukristo' wa CHADEMA...
kambi ya legwagwaniJerry Silaa. Kweli dogo moto chini...
Wanaolalamika imbalance ya dini hawatakuwa na cha kusema...
Mkuu ukiimba hako kawimbo ganja lisikae mbali!!kwa hali ya mambo ilivyo CCM walitakiwa kuweka watu ambao wanakubalika na kambi zao na wananchi ili kuupa wakati mgumu upinzani wakati wa kunadi sera.Siasa ya tz hivi sasa inaamuliwa sana na sifa za watu husika mbele ya jamii.CCM inakabiliwa na upinzani wa aina tatu,mosi vyama vya siasa na mataifa wafadhili,pili kambi zenye mitazamo tofauti ndani ya chama chenyewe,tatu ni wananchi.niitazamapo list hii inaonyesha dhahiri kuwa imechaguliwa kwa ajili ya kusolve case ya kwanza tu na kuacha case mbili zilizobaki ambazo ni tishio zaidi kwa chama.kwa mara nyingine naona CCM ikifanya maamuzi huku vichwani wakiiwaza Chadema,NCCR,CUF,marekani,ujerumani,iran,china,malkia n.k na kusahau kambi zao ndani ya chama na wananchi na hapo ndipo wanapoingizwa shimoni bila kujijua!hizi sura ni sura za kupambana na Chadema lkn si sura za kuleta utulivu ndani ya CCM na pia si sura za wananchi.najiuliza kulitokea nini 2010 hadi upinzani uwakoseshe usingizi CCM namna hii?naona mtego wa wapinzani kwa CCM 2015 ulitegwa 2010 na unafanya kazi very successful!huu mtego mie nauita AUTOMATIC DIVERSION!Ndg zangu wa Chadema nina kawimbo ka kuwaimbia hapa,I WAKE UP THIS MORNING,SMILE WITH THE RISING SUN,THREE LITTLE BIRDS,BESIDE MY DOOR STEPS,SINGING SWEET SONGS,THE MELODY IS PURE AND TRUE,SAYING,THIS IS A MESSAGE TO U UH UH!SINGING..........!
Eventually, hawa hawaamui kitu, everything has to go NEC.
Tibajuka mwenyewe kaanza kupoteza dira aliyotoka nayo UN!
ifuatayo ni orodha ya wajumbe wa kamati kuu kikao kimemalizika muda si mrefu.
1. WASIRA
2.PINDI Chana
3.Tibaijuka
4. Jerry Slaa
5. Kimbisa
6. Nchimbi
8. Lukuvi
9. Fenela Mkangara
Zanzibar:
1. Nahodha
2. Hussein Mwinyi
3. Prof Makame Mbalawa
4. Dr Salm
5. Maua daftari
6. lL. Abuu
7. Samia
Wadau naomba kuwasIlisha
Mwigulu asingeachwa. Au dogo ana matusi kuliko mwigulu?amekuwa akiitukana sana CDM kwa siku za hivi karibuni. Nadhani hiki ni kigezo kikuu cha mtu kuteuliwa kama ilivyo kwa Wasira
Last week nilikuja na mada kusema majina yako na hakuna cha kura watu wakabeza wakidhani tunatania .Sasa hao hapo juu ulizia wamepata kura ngapi .Hawakupigiwa kura ni chaguo la Mwenyekiti .Nilisema kijana mmoja kichaa akasema naleta udaku .Naomba nionyeshwe idadi ya kura zao basi .
Mkuu Ritz kuipigia Kula CCM ndiyo nini?
Bado naona kamati kuu ya Mkapa angalau ilikuwa na watu strong kiasi fulani, lakini hii ya akina Maua Dafutari, Samia Suluhu? Hivi Kikwete amewachagua kutokana na uwezo wa kureason mambo au mwonekano wao? Kwamba akina wasira wana sura za kuogofya kidogo basi wajumbe wote watawatetemekea au akina Lukuvi wazee wa kutetea maslahi ya mwenyekiti hata yale ya kijinga? Akina Jerry Slaa sijui Kimbisa, no please! Sijaona mtu hapo, labda Dr Salim ambaye hatahivyo na yeye keshachoka, anaweza asiwe critical sana.Alichofanya mhe naona ni kuteua watu ambao hawatampinga kwenye maamuzi yake,karibia wote hao ni ndiyo mzee,naona wakati wengine wanafikiria chama mhe amefocus 2015!kwa ajili ya kumpitisha mtu amtakaye,ila anasahau kuwa nidhamu ya hao wajumbe kuelekea 2015 itashuka,akumbuke mkapa alikuwa anaogopwa lakini 2005 watu walimwona wa kawaida tu wakati wa kutafuta mgombea.
Kutokuchaguliwa kwa Lowasa hakumzuii kuukwaa urais 2015.
Watu walioumizwa hapo ni Membe na Sita.