Wajumbe wapya wa Kamati Kuu CCM hawa hapa...

Wajumbe wapya wa Kamati Kuu CCM hawa hapa...

bibikuku

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2011
Posts
832
Reaction score
496
Waliochaguliwa ni William Lukuvi, John Nchimbi, Pindi Chana, Jery Silaa, Anna Tibaijuka na Steven Masatu Wasira

Ifuatayo ni orodha ya wajumbe wa kamati kuu kikao kimemalizika muda si mrefu:

1. Wassira
2. Pindi Chana
3. Tibaijuka
4. Jerry Slaa
5. Kimbisa
6. Nchimbi
7. Lukuvi

Zanzibar:
1. Nahodha
2. Hussein Mwinyi
3. Prof Makame Mbalawa
4. Dr. Salim
5. Maua daftari
6. lL. Abuu
7. Samia Suluhu

Mwananchi Newspaper
Makada 14 wa CCM, saba kutoka kila upande wa muungano walipigiwa kura katika uchaguzi huo ambao matokeo yake yalitangazwa usiku wa manane.

Kutoka Tanzania Bara, waliochaguliwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira.

Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa na Mbunge wa Viti Maalum, Pindi Chana.

Kutoka Tanzania Zanzibar mbali na Dk Salim, wengine ni Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi.

Pia wamo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Maua Abeid Daftari pamoja na Khadija Aboud. Wajumbe hao wapya wanaunda Kamati Kuu pamoja na wengine wanaoingia kwa nyadhifa zao.
 
ifuatayo ni orodha ya wajumbe wa kamati kuu kikao kimemalizika muda si mrefu.
1. WASIRA
2.PINDI Chana
3.Tibaijuka
4. Jerry Slaa
5. Kimbisa
6. Nchimbi
8. Lukuvi
9. Fenela Mkangara

Zanzibar:
1. Nahodha
2. Hussein Mwinyi
3. Prof Makame Mbalawa
4. Dr Salm
5. Maua daftari
6. lL. Abuu
7. Samia

Wadau naomba kuwasIlisha
 
Eventually, hawa hawaamui kitu, everything has to go NEC.
 
Mbona wajumbe ni 16 tu, wamepatikanaje. Je akinanani wataingia ata kwa vyeo vyao?

Ya kweli Au ndio masihara haya. Kama ni kweli
CCM IMEKAMATWA VIBAYA. Ni mali ya mwenyekiti
 
By Andrew Lameck, Duuuh kazi kweli kweli! white hair hayupo?
 
Kutokuchaguliwa kwa Lowasa hakumzuii kuukwaa urais 2015.
Watu walioumizwa hapo ni Membe na Sita.
 
Waliochaguliwa ni William Lukuvi, John Nchimbi, Pindi Chana, Jery Silaa, Anna Tibaijuka na Steven Masatu Wasira 'Tyson'

These demons from hell, so heartless! civil war zinaendelea sehemu mbali mbali, watu wanauana, wao kimyaaa, wanaendelea tu kugawana madaraka
 
bibikuku; + nkomelo;


Siyo shirika moja wajamen?

Ni hofu na ID hizi!

anyway! Chama cha majambazi hata ingemchagua nani awe wapi hakika nakwambia hawana tena sumu kwa Watanzania walio waelewa!

Wanatapatapata tu! Mbinu zao zote tunazo mifukoni!
 
Last edited by a moderator:
bibikuku; + nkomelo;


Siyo shirika moja wajamen?

Ni hofu na ID hizi!

anyway! Chama cha majambazi hata ingemchagua nani awe wapi hakika nakwambia hawana tena sumu kwa Watanzania walio waelewa!

Wanatapatapata tu! Mbinu zao zote tunazo mifukoni!

mkuu ondoa shaka, simfahamu nkomelo hata kidogo. ukiangalia vema, mie sina jina la Fenela lakini mwenzangu analo.
 
Last edited by a moderator:
Mbona wajumbe ni 16 tu, wamepatikanaje. Je akinanani wataingia ata kwa vyeo vyao?

Ya kweli Au ndio masihara haya. Kama ni kweli
CCM IMEKAMATWA VIBAYA. Ni mali ya mwenyekiti

Last week nilikuja na mada kusema majina yako na hakuna cha kura watu wakabeza wakidhani tunatania .Sasa hao hapo juu ulizia wamepata kura ngapi .Hawakupigiwa kura ni chaguo la Mwenyekiti .Nilisema kijana mmoja kichaa akasema naleta udaku .Naomba nionyeshwe idadi ya kura zao basi .
 
Back
Top Bottom