Wajumbe wa CWT wapata hekaheka kufanya kikao, Polisi waingilia kati

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Wajumbe wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), leo Septemba 25, 2023 wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzuiliwa kufanya kikao chao cha dharura cha Baraza la Taifa la CWT

Wakizungumza nje ya geti la makao makuu ya chama hicho Jijini Dodoma wamesema wameshangazwa na kitendo hicho kwani wao walikuwa na kikao cha kawaida cha kujadili mambo yao na pia ni vyema wangewaambia mapema kama hakuna kikao hicho kwani wengine wamesafiri kutoka mikoa ya mbali

Hata hivyo Mkuu wa kituo cha polisi Dodoma Mjini Joram Samson ambaye alisimamia zuio hilo kwa wanachama wa CWT alitoa zuio hilo na kuwaruhusu kufanya kikao chao ndani ya ofisi hizo kwa kuwaambia kuwa walichokuwa wanasubiri wao ni ruhusa kutoka kwa msajili wa vyama vya wafanyakazi ambapo pia amewataka kufanya kikao chao kwa amani.

Chanzo: Wasafi FM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom