Wajumbe Kamati Kuu CHADEMA wamuonya Zitto.

Wajumbe Kamati Kuu CHADEMA wamuonya Zitto.

Laiti angeishia Jimbo lake la Kigoma Kaskazini ingeeleweka kwa kuwa yeye ni mbunge wa Jimbo hilo.Lakini Kasulu wapi na wapi huku akiwa hana madaraka yoyote ndani ya chama?

Hapa kuna Tofauti gani na Shibuda aliyekuwa anajiamulia kuhutubia majukwaa ya CCM?

Jambo lingine ni kwanini akiwa kama Mbunge asiungane na Katibu Mkuu wa chama chake aliyeko ziarani Kanda ya Magharibi huko Tabora??

Kwanini katibu mkuu hasiungane na zitto wakati anaenda kigoma....jaribu kujiuliza swali lako upande wa pili
 
Hao wajumbe ni kina nani,wapo wangapi na wamesema wapi? Mbona sugu anakujaga huku songea kufanya mikutano na hana cheo chochote zaidi ya ubunge wa mbeya? Wapi zitto kakashifu viongozi wa chama,kama wafuasi wake mbona yeye anatukanwa pia?

Unauhakika kwamba huwa hatoi taarifa Taifa makao makuu?

wanaomlalamikia Zito ndo hao wa huko makao makuu, je umeshawahi wasikia wakilalama kuhusu Sugu?
 
Hongera sana zitto kwa kazi nzuri uayofanya ya kuwaeleza ukweli wananchi
 
Mbona mnachelewa, hebu mfukuzeni muone halafu tukutane 2015 hapahapa JF
 
Kutokana Na Yaloandikwa Katika Uzi Huu Nimebaini Makosa Matatu Tu, Na Ndiyo Yaliyopo 1.kufanya Mikutano Nje Ya Jimbo Lake Pasipo Idhini Ya Chama, Ziala Ambayoa Lengo Lake La Kweli Ni Kuimarisha Chama. Kwahili Apongezwe Tu Kama Walivyo Mpongeza Katika Kampeni Za 2010, Alizoendesha Nje Ya Jimbo Lake. 2. Kutukanwa Kwa Viongozi Wa Juu Ya Chama Chetu Cha Demokrasia Na Maendeleo. Kwa Mujibu Wa Muandika Uzi Hapa Na Ndivyo Ilivyo, Kosahili Limefanywa Na Mashabiki Wa Zitto. Zitto Hajatukana Mtu Ila Ametukanwa Na Viongozi Wa Chama Chetu. Zitto Amekwenda Kuwapatanisha Wananchi Na Viongozi Wa Chama Hi Ni Wazi Kutokana Na Hotuba Zake. Jambo La Mashabiki Wa Chama Kutukana Si Kosa La Kabwe, Wanalifanya Hata Huko Mitaani, Tena Mumshukuru Kabwe Anawaita Na Kubadilisha Mawazo Yao Ovu. 3. Kosa La Tatu Ni Kumaliza Chadema, Zitto Hajafanya Hivyo . Anahukumiwa Kwakuwa Suala Hili Limeripotiwa Na Gazeti La Chama Gamba. Hii Ndio Nature Ya Magamba, Wakizalisha Mgongano Ndani Ya Upinzani Wanatafuta Upande Waegemee.
 
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA wamemuonya aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kwa ukiukwaji wa waziwazi wa taratibu za chama hicho.

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wajumbe hao wameshangazwa na kitendo cha Zitto Kabwe kujiandalia ziara zenye mwelekeo hasi kwa chama hicho.

Ikumbukwe kwamba Zitto amefukuzwa nafasi zote za Uongozi ndani ya Chadema na yeye ni mbunge tu wa Kigoma Kaskazini huku akisubiri huruma ya Kamati Kuu kuhusu uanachama wake.

Kilichoshangaza zaidi ni kitendo cha Zitto Kabwe kufanya ziara Jimbo la Kasulu bila kutaarifu Chama huku mashabiki wake wakiutumia mkutano huo kukashifu chama na viongozi wake.

Kitendo kinachofanyika hakikubaliki na ni ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na taratibu za chama.

Katika hali ya kuonyesha kinachofanywa ni mkakati wa kuangamiza Chadema Gazeti la Jamboleo Toleo la Jumapili linalomilikiwa na Kada wa CCM katika habari kuu limeandika "Zitto aimaliza CHADEMA" likiripoti yanayotokea Kigoma.
Yeye amekwemda kwao. Kwani amesema amekwenda kama kiongozi wa cdm?
 
Hivi CDM mna akili kweli au zimeshamalizwa na mabomu? Mtu mdogo kama Zitto mmeshindwa kumfukuza eti kwa kuogopa chama kugawanyika? Propaganda za baadhi ya wana CCM wanaotaka kuturudisha miaka ya 1995 ndo zinawaogopesha? Endapo hamtamfukuza Zitto kweli taamini hiki chama kipo kwa ajili ya maandamano tu. Hivi umfume mke wako akipigwa front na back km walivyokuwa wanafanya wale askari wa tokomenza ujangiri kwa hiari yake utamsamehe kwamba kapitiwa na shetani? Chama kimejaa wasomi kumbe hata bongo hawana wamejaza makamasi tu. Mnampa kiburi nyie wenyewe ingeni North Korea kwani mnatuchosha sana sisi wapenda mabadiliko. Kuwepo kwa CCM IMARA NI PALE PATAKUWA NA UPINZANI IMARA lakni si huyu mhubiri ukabila Zitto.
 
Aisee, sijui hata kwanini bado hawajamfukuza mpaka leo.... Hakuna mnafiki kama zito, natamani aondoke chadema akaanzishe chama chake, anao wanachama wengi tu watamtosha kwenda kuanzisha chama... Aondoke cdm, tumechoka kumsikia na vituko vyake kila kukicha!...

Kamati kuu tafadhalini tuhurumieni wanachama wenye mapenzi mema na cdm... Hili la zito lifikisheni mwisho jamani
tatizo wasiomtaka zito hawafiki hata 100 tena wengi ni hawa akina molemo,ben,yerico,mungi,mnyika,mungi,arushamoja na nani mwingine...mh slaa,mtei,mbowe,lema,nasari, basi.
 
Zitto na hao wanaomdhamini wanapoteza mda wao. CDM Kigoma ina mbunge na diwani 1. Hivyo CDM haina/haikuwa na nguvu ya kiivyo Kigoma. Watu wa kigoma kwa maksudi au kutokujua wametumika na Zitto,kwa kisingizio cha Ukigoma,mtoto wa nyumbani!.

Slaa kura za uraisi alipata nyingi kushinda Kilimanjaro.
 
Namshangaa sana zitto, kwanini asifanye maamuzi magumu?
 
Hao wajumbe ni kina nani,wapo wangapi na wamesema wapi? Mbona sugu anakujaga huku songea kufanya mikutano na hana cheo chochote zaidi ya ubunge wa mbeya? Wapi zitto kakashifu viongozi wa chama,kama wafuasi wake mbona yeye anatukanwa pia?

taarifa ndugu ndo tatizo,sidhani sugu anaweza kwenda songea bila chama kuwa na taarifa.
 
tatizo wasiomtaka zito hawafiki hata 100 tena wengi ni hawa akina molemo,ben,yerico,mungi,mnyika,mungi,arushamoja na nani mwingine...mh slaa,mtei,mbowe,lema,nasari, basi.

wewe ni matokeo ya athari za shule za kata.
 
naamini washauri wa Zitto ---------- na cdm.hii sio akili ya kawaida aisee
 
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA wamemuonya aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kwa ukiukwaji wa waziwazi wa taratibu za chama hicho.

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wajumbe hao wameshangazwa na kitendo cha Zitto Kabwe kujiandalia ziara zenye mwelekeo hasi kwa chama hicho.

Ikumbukwe kwamba Zitto amefukuzwa nafasi zote za Uongozi ndani ya Chadema na yeye ni mbunge tu wa Kigoma Kaskazini huku akisubiri huruma ya Kamati Kuu kuhusu uanachama wake.

Kilichoshangaza zaidi ni kitendo cha Zitto Kabwe kufanya ziara Jimbo la Kasulu bila kutaarifu Chama huku mashabiki wake wakiutumia mkutano huo kukashifu chama na viongozi wake.

Kitendo kinachofanyika hakikubaliki na ni ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na taratibu za chama.

Katika hali ya kuonyesha kinachofanywa ni mkakati wa kuangamiza Chadema Gazeti la Jamboleo Toleo la Jumapili linalomilikiwa na Kada wa CCM katika habari kuu limeandika "Zitto aimaliza CHADEMA" likiripoti yanayotokea Kigoma.
Kamati kuu ya wabaguzi
 
Back
Top Bottom