Wajumbe Kamati Kuu CHADEMA wamuonya Zitto.

Ndio maana hua nasema kuwa Baadhi ya Waandishi WA Habari WA Tanzania ni zaidi ya Ibilisi, sasa hapo Jambo Leo wameandika utumbo gani? Je wakati wanaandika walifikiria impact ya utumbo kwa Jamiii maskini?????

Na ndiyo maana wanachama wanashangazwa na hali hii.Ina maana kama Zitto ameenda kwa niaba ya Chama magazeti yanayojulikana kumpamba yataandikaje Zitto Aimaliza Chadema??
 
Hapo kwenye Red: Huruma ya nini, si mumfukuze? kwani siku 14 hazijaisha?
Hapo kwenye green: Slaa alienda Jimbo la Zitto bila mwenyeji wake kuwepo. Je hapo FAIR PLAY ikowapi? CHADEMA mmecheza Faulo na Zitto naye anacheza faulo.(Nakumbuka enzi za miaka ya 1970 mechi kati ya Uruguay & Paraguay kuanzi golikipa hadi namba 11 wote wanapiga buti)
Hapo mimi naona kama Ngoma imekuwa droo.

Acha kujifanya kipofu wa siasa na taratibu.

Dr Slaa ana mamlaka ya kwenda popote yeye ni Katibu Mkuu wa chama.Pili Ziara ya Dr Slaa imepangwa na Sekretariati Makao Makuu.
 
Labda kama amevunja katiba ya CDM, lakini Katiba ya JMT, sheria mama inasema kila raia ana uhuru wa kwenda popote, kukutana na mtu au kikundi cha watu ili mradi havunji sheria. Huyu mtu lazima CDM muwe na shukurani Ziara yake za hatuba zake zmepunguza kumeguka chama, ameeasa wanachama wawe wavumilivu wakati huu suala lake likishughulikiwa.
 
Labda kama amevunja katiba ya CDM, lakini Katiba ya JMT, sheria msma inasema kila raia ana uhuru wa kwenda popote, kukutana na mtu au kikundi cha watu ili mradi havunji sheria

Hivyo vibali vya mikutano na maandamano anaombea kwa kibali kipi? Anaomba kama kiongozi gani ndani ya chama?

Kuna sheria inayoruhusu mtu yeyote kwenda popote kuomba vibali vya mikutano na maandamano bila kushirikisha chama??
 
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA wamemuonya aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kwa ukiukwaji wa waziwazi wa taratibu za chama hicho.

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wajumbe hao wameshangazwa na kitendo cha Zitto Kabwe kujiandalia ziara zenye mwelekeo hasi kwa chama hicho.
Ikumbukwe kwamba Zitto amefukuzwa nafasi zote za Uongozi ndani ya Chadema na yeye ni mbunge tu wa Kigoma Kaskazini huku akisubiri huruma ya Kamati Kuu kuhusu uanachama wake.

Kilichoshangaza zaidi ni kitendo cha Zitto Kabwe kufanya ziara Jimbo la Kasulu bila kutaarifu Chama huku mashabiki wake wakiutumia mkutano huo kukashifu chama na viongozi wake.

Kitendo kinachofanyika hakikubaliki na ni ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na taratibu za chama.

Katika hali ya kuonyesha kinachofanywa ni mkakati wa kuangamiza Chadema Gazeti la Jamboleo Toleo la Jumapili linalomilikiwa na Kada wa CCM katika habari kuu limeandika "Zitto aimaliza CHADEMA" likiripoti yanayotokea Kigoma.

Hivi siku hizi mtu aruhusiwi kufanya mikutano jimboni kwake au hata nje ya jimbo lake bila ruhusa ya Chama chake? Inakuwaje viongozi wengine wa CHADEMA wafanye mikutano wakiongelea masuala haya ya zitto lakini yeye hasiruhusiwe!
 
Labda kama amevunja katiba ya CDM, lakini Katiba ya JMT, sheria msma inasema kila raia ana uhuru wa kwenda popote, kukutana na mtu au kikundi cha watu ili mradi havunji sheria

Hicho kibali akiomba anaomba kuwa yeye ni mchungaji wa kanisa hivyo anaenda kuwahubiria watu au anaomba kwa jina la chama gani?
 
Haikubaliki kuandaa mikutano bila ridhaa ya chama.
Zitto amekiuka chama kichukue hatua stahiki.

Laiti angeishia Jimbo lake la Kigoma Kaskazini ingeeleweka kwa kuwa yeye ni mbunge wa Jimbo hilo.Lakini Kasulu wapi na wapi huku akiwa hana madaraka yoyote ndani ya chama?

Hapa kuna Tofauti gani na Shibuda aliyekuwa anajiamulia kuhutubia majukwaa ya CCM?

Jambo lingine ni kwanini akiwa kama Mbunge asiungane na Katibu Mkuu wa chama chake aliyeko ziarani Kanda ya Magharibi huko Tabora??
 
Hivi siku hizi mtu aruhusiwi kufanya mikutano jimboni kwake au hata nje ya jimbo lake bila ruhusa ya Chama chake? Inakuwaje viongozi wengine wa CHADEMA wafanye mikutano wakiongelea masuala haya ya zitto lakini yeye hasiruhusiwe!


Zito sasahivi ni mbunge wa kigoma tu, hivyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za chama haruhusiwi ndio
 
Hivi siku hizi mtu aruhusiwi kufanya mikutano jimboni kwake au hata nje ya jimbo lake bila ruhusa ya Chama chake? Inakuwaje viongozi wengine wa CHADEMA wafanye mikutano wakiongelea masuala haya ya zitto lakini yeye hasiruhusiwe!

Ziara zote za viongozi na wabunge wa Chadema ni lazima ziruhusiwe na zipate baraka ya chama!
 
Back
Top Bottom