Wajumbe Kamati Kuu CHADEMA wamuonya Zitto.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA wamemuonya aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kwa ukiukwaji wa waziwazi wa taratibu za chama hicho.

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wajumbe hao wameshangazwa na kitendo cha Zitto Kabwe kujiandalia ziara zenye mwelekeo hasi kwa chama hicho.

Ikumbukwe kwamba Zitto amefukuzwa nafasi zote za Uongozi ndani ya Chadema na yeye ni mbunge tu wa Kigoma Kaskazini huku akisubiri huruma ya Kamati Kuu kuhusu uanachama wake.

Kilichoshangaza zaidi ni kitendo cha Zitto Kabwe kufanya ziara Jimbo la Kasulu bila kutaarifu Chama huku mashabiki wake wakiutumia mkutano huo kukashifu chama na viongozi wake.

Kitendo kinachofanyika hakikubaliki na ni ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na taratibu za chama.

Katika hali ya kuonyesha kinachofanywa ni mkakati wa kuangamiza Chadema Gazeti la Jamboleo Toleo la Jumapili linalomilikiwa na Kada wa CCM katika habari kuu limeandika "Zitto aimaliza CHADEMA" likiripoti yanayotokea Kigoma.
 
1800

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
2,215
1,195
Wala haina haja ya kuhangaika nae,sidhani kama ataweza kufanya mikutano nje ya Kigoma!anachofanya ni kuwalaghai baadhi ya watu wasiojitambua kwa minajiri ya UKIGOMA wake!hizi ni dalili za mfa maji,ni kumuacha ahangaike mwisho wa siku atakua amejimaliza naturaly!
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,030
2,000
Huyu mtu sijuin kwanini chama kinamlea kwa kiwango hiki. Huko Kigoma Kaskazini angalau inaweza kueleweka kwamba alikwenda kuongea na wapiga kura wake lakini maeneo mengine anakwenda kama nani? Kama anakwenda kama mwananchi huru au mwanachama wa CCM na ieleweke hivyo na sio kwenda kwa mwamvuli wa chama huku akifanya yaliyo kinyume na kanuni za chama anachojifanya kukipigania.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,030
2,000
Wala haina haja ya kuhangaika nae,sidhani kama ataweza kufanya mikutano nje ya Kigoma!anachofanya ni kuwalaghai baadhi ya watu wasiojitambua kwa minajiri ya UKIGOMA wake!hizi ni dalili za mfa maji,ni kumuacha ahangaike mwisho wa siku atakua amejimaliza naturaly!

Mkabila mkubwa sana huyu. Aende maeneo mengine ya nchi tumwone.
 
Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
15,722
2,000
Hao wajumbe ni kina nani,wapo wangapi na wamesema wapi? Mbona sugu anakujaga huku songea kufanya mikutano na hana cheo chochote zaidi ya ubunge wa mbeya? Wapi zitto kakashifu viongozi wa chama,kama wafuasi wake mbona yeye anatukanwa pia?
 
COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,473
2,000
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA wamemuonya aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kwa ukiukwaji wa waziwazi wa taratibu za chama hicho.

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wajumbe hao wameshangazwa na kitendo cha Zitto Kabwe kujiandalia ziara zenye mwelekeo hasi kwa chama hicho.

Ikumbukwe kwamba Zitto amefukuzwa nafasi zote za Uongozi ndani ya Chadema na yeye ni mbunge tu wa Kigoma Kaskazini huku akisubiri huruma ya Kamati Kuu kuhusu uanachama wake.

Kilichoshangaza zaidi ni kitendo cha Zitto Kabwe kufanya ziara Jimbo la Kasulu bila kutaarifu Chama huku mashabiki wake wakiutumia mkutano huo kukashifu chama na viongozi wake.

Kitendo kinachofanyika hakikubaliki na ni ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na taratibu za chama.

Katika hali ya kuonyesha kinachofanywa ni mkakati wa kuangamiza Chadema Gazeti la Jamboleo Toleo la Jumapili linalomilikiwa na Kada wa CCM katika habari kuu limeandika "Zitto aimaliza CHADEMA" likiripoti yanayotokea Kigoma.

Hapo kwenye Red: Huruma ya nini, si mumfukuze? kwani siku 14 hazijaisha?
Hapo kwenye green: Slaa alienda Jimbo la Zitto bila mwenyeji wake kuwepo. Je hapo FAIR PLAY ikowapi? CHADEMA mmecheza Faulo na Zitto naye anacheza faulo.(Nakumbuka enzi za miaka ya 1970 mechi kati ya Uruguay & Paraguay kuanzi golikipa hadi namba 11 wote wanapiga buti)
Hapo mimi naona kama Ngoma imekuwa droo.
 
damcon

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
214
195
zitto washauri wake wa kisiasa watakuwa na upeo mdogo au dogo my be hashauriki...naona kaamua kujimaliza mwenyewe kwa kuonyesh true color yake katika kukiharibu chama...watu wakisema jamaa msaliti kuna watu wa cdm walikuwa wanamtetea,this guy anatumiwa na ccm kutekeleza utabiri wa wasira
 
sweetlady

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
16,962
1,250
Huyu mtu sijuin kwanini chama kinamlea kwa kiwango hiki. Huko Kigoma Kaskazini angalau inaweza kueleweka kwamba alikwenda kuongea na wapiga kura wake lakini maeneo mengine anakwenda kama nani? Kama anakwenda kama mwananchi huru na ieleweke hivyo na sio kwenda kwa mwamvuli wa chama huku akifanya yaliyo kinyume na kanuni za chama anachojifanya kukipigania.

Aisee, sijui hata kwanini bado hawajamfukuza mpaka leo.... Hakuna mnafiki kama zito, natamani aondoke chadema akaanzishe chama chake, anao wanachama wengi tu watamtosha kwenda kuanzisha chama... Aondoke cdm, tumechoka kumsikia na vituko vyake kila kukicha!...

Kamati kuu tafadhalini tuhurumieni wanachama wenye mapenzi mema na cdm... Hili la zito lifikisheni mwisho jamani
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Hao wajumbe ni kina nani,wapo wangapi na wamesema wapi? Mbona sugu anakujaga huku songea kufanya mikutano na hana cheo chochote zaidi ya ubunge wa mbeya? Wapi zitto kakashifu viongozi wa chama,kama wafuasi wake mbona yeye anatukanwa pia?

Kwa kifupi tu ziko taratibu za chama kwa kiongozi au mbunge kwenda kufanya mikutano.Siyo kujiamulia mtu yeyote na kwenda kuhutubia popote.Vinginevyo chama kisicho na utaratibu siyo chama bali ni genge la wahuni.
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,067
2,000
Kwani hizo taratibu au kanuni zinatakaje? Ni kwa vipu huho ZZK amekiuka au kuvunja kanuni hizo?
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,113
2,000
Ndio maana hua nasema kuwa Baadhi ya Waandishi WA Habari WA Tanzania ni zaidi ya Ibilisi, sasa hapo Jambo Leo wameandika utumbo gani? Je wakati wanaandika walifikiria impact ya utumbo kwa Jamiii maskini?????
 
Bilal bin Rabah

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
254
0
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA wamemuonya aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kwa ukiukwaji wa waziwazi wa taratibu za chama hicho.

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wajumbe hao wameshangazwa na kitendo cha Zitto Kabwe kujiandalia ziara zenye mwelekeo hasi kwa chama hicho.

Ikumbukwe kwamba Zitto amefukuzwa nafasi zote za Uongozi ndani ya Chadema na yeye ni mbunge tu wa Kigoma Kaskazini huku akisubiri huruma ya Kamati Kuu kuhusu uanachama wake.

Kilichoshangaza zaidi ni kitendo cha Zitto Kabwe kufanya ziara Jimbo la Kasulu bila kutaarifu Chama huku mashabiki wake wakiutumia mkutano huo kukashifu chama na viongozi wake.

Kitendo kinachofanyika hakikubaliki na ni ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na taratibu za chama.

Katika hali ya kuonyesha kinachofanywa ni mkakati wa kuangamiza Chadema Gazeti la Jamboleo Toleo la Jumapili linalomilikiwa na Kada wa CCM katika habari kuu limeandika "Zitto aimaliza CHADEMA" likiripoti yanayotokea Kigoma.
Kwahiyo sisi tufanyaje?
 
sweetlady

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
16,962
1,250
Hapo kwenye Red: Huruma ya nini, si mumfukuze? kwani siku 14 hazijaisha?
Hapo kwenye green: Slaa alienda Jimbo la Zitto bila mwenyeji wake kuwepo. Je hapo FAIR PLAY ikowapi? CHADEMA mmecheza Faulo na Zitto naye anacheza faulo.(Nakumbuka enzi za miaka ya 1970 mechi kati ya Uruguay & Paraguay kuanzi golikipa hadi namba 11 wote wanapiga buti)
Hapo mimi naona kama Ngoma imekuwa droo.

Kaa kimya wewe , usisahau kuwa slaa ni katibu mkuu wa chama... Sasa huyo mnafiki wenu vipi? Afu kwanini msimshauri akaanzishe chama chake jamani?
 
COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,473
2,000
Hao wajumbe ni kina nani,wapo wangapi na wamesema wapi? Mbona sugu anakujaga huku songea kufanya mikutano na hana cheo chochote zaidi ya ubunge wa mbeya? Wapi zitto kakashifu viongozi wa chama,kama wafuasi wake mbona yeye anatukanwa pia?

Mkuu pokea big like :peace: . Hiyo inaitwa mkuki kwa nguruwe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom