Wajumbe Kamati Kuu CHADEMA wamuonya Zitto.

Wajumbe Kamati Kuu CHADEMA wamuonya Zitto.

Sielewi kwanini watu hawaoni hivi vitendo vya Zitto ni tatizo!!

Sidhani kama kuna mbunge wa CCM anaweza kwenda kufanya mikutano kwenye majimbo mengine tu nje ya utaratibu wa CCM.

Sawa endeleeni kumuonea aibu kumwambia ukweli.
 
Kaa kimya wewe , usisahau kuwa slaa ni katibu mkuu wa chama... Sasa huyo mnafiki wenu vipi? Afu kwanini msimshauri akaanzishe chama chake jamani?

Wivu na roho mbaya zitawaua. Subirini maamuzi ya chama acheni kuropoka roppka hovyo!
 
Hivi Mtei alijisikiaje pale alipopata taarifa kuwa Mbowe kamsaliti binti yake?!
 
Last edited by a moderator:
hizo tulishazizoea, mnakumbuka Nazir Karamagi, Chenge, Rostam na Lowassa wote walipokelewa kwa mbwembwe za hali ya juu!!lakini leo wako wapi zaidi ya Lowassa kukimbilia makanisani na misikitini kuomba pa kusemea!!Huyo ZZK na yeye ndo muda wake unaisha hivyo na yy anafahamu hasafishiki tena CDM!!
 
Tatizo lako molemo wewe una Zittoforbia,ndio maana siku hizi unashindwa hata kula ukashiba kisa Zitto kufanya mikutano na mapikezi kuwa makubwa kuliko ya madikteta wako?
Zitto ni mtetezi wa kigoma nzima,ndio maana alidai kwa nguvu zote kigoma na wilaya zake kupatiwa umeme,alidai Daraja la maragarasi ambalo halipo jimboni kwake,alidai kigoma kuunganishwa na mikoa mingine kwa kujengewa barabara za lami. Zitto pia ni mwakilishi wa watanzania wote,najua mnatamani mumzuie asiende mikoa mingine lkn wananchi tumejitolea kuchangia mabadiliko,tutamchangia mh.Zitto ili afanye mikutano nchi nzima na watanzania wanaojitambua watamiminika kumsikiliza.
Mmezoea kujifanya makaburu lkn tatizo kubwa linalowasibu hamna strategies,mmebaki kutumia peda kama wafanyavyi ccm ili mpate watu mikutanoni,mwusho wa ubaya ni aibu,huyo ndio Zitto kabwe tumaini pekee la watanzania,nakushauri ujitambue na uache kutumiwa na nakaburu wa chadema, ungana na kijana mwenzako kama mungu kakuandikia mafanikio kamwe hayawezi zuiliwa na Mbowe na Slaa,walimkomoa Kafulila wakijua wamemmaliza kisiasa lakini ndio wakamuongezea umaarufu na sasa yupo mjengoni na Mbowe unae muabudu
Zitto anatarajia kufanya mikutano nchi nzima kwa gharama za wananchi wapenda mabadiliko na utazimia siku atakapopokelewa Arusha kama mfalme ndipo utatambua nguvu za Shujaa huyu aliejitoa kusimamia haki na uwajibikaji ndani ya chama chake na nje ya chama chake.go Zitto go watanzania tunakuamini.
 
Laiti angeishia Jimbo lake la Kigoma Kaskazini ingeeleweka kwa kuwa yeye ni mbunge wa Jimbo hilo.Lakini Kasulu wapi na wapi huku akiwa hana madaraka yoyote ndani ya chama?

Hapa kuna Tofauti gani na Shibuda aliyekuwa anajiamulia kuhutubia majukwaa ya CCM?

Jambo lingine ni kwanini akiwa kama Mbunge asiungane na Katibu Mkuu wa chama chake aliyeko ziarani Kanda ya Magharibi huko Tabora??

Poor thing!Naona mmeishiwa hoja mpaka mnahuzunisha siku hizi,Halafu na hii Kamati Kuu ya Chama inazidi kunitia hofu kama kweli inaundwa na watu wenye weledi wa kutosha au wenye mawazo huru,Nahisi kama vile wamegeuka kuwa mateka wa kisiasa wa Mbowe kiasi kwamba hata hawaeleweki wanaongea nini.Hivi hii CC ya Chadema haijui kuwa Zitto bado ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa Magharibi?Na akitoka Kigoma ataenda Shinyanga,Tabora kwasababu Mikoa yote hii ipo chini yake.Chadema punguzeni Udikteta na kujiona kwamba nyinyi ndio pekee wenye haki miliki ya kufanya mikutano ya kisiasa hapa Tanzania.
 
Zitto afukuzwe tu chadema akawe mbunge wa mahakama
 
Sielewi kwanini watu hawaoni hivi vitendo vya Zitto ni tatizo!!

Sidhani kama kuna mbunge wa CCM anaweza kwenda kufanya mikutano kwenye majimbo mengine tu nje ya utaratibu wa CCM.

Sawa endeleeni kumuonea aibu kumwambia ukweli.

Tatizo la CHADEMA ni kulea matatizo, angalia issue ya Kafulila NCCR Mbatia alimvua uanachama Mara moja ahadi kamwaga jozi, CCM hivyo hivyo yule Masoud wa Zanzibar walimvua uwanachama Mara moja.
 
Hizi taratibu, kanuni na itifaki hazina vipengele?.

Viwekeni hivyo vipengele hapa kwenye jukwaa ili mkate mzizi wa fitina na pia muwasaidie ambao hawazijui kuliko kung'ang'ania kusema ANATENDA MAKOSA. Wekeni hapa ili wataalamu wa siasa wavichambue na wao watoe angalizo.

Halafu hawa wajumbe wa Kamati Kuu hawana majina?. Au ndiyo siasa zilezile za kuvidhiana chini ya meza.

CHADEMA walipoanzisha hii kitu hawakufahamu kuna infallible law of karma
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepitisha mpango mkakati wake wa kuelekea kushika dola mwaka 2015 kwa kumega madaraka ya makao makuu katika kanda kumi. Maazimio hayo yalipitishwa na Kamati Kuu (CC) juzi kwa agenda moja kubwa ambayo ni kupitisha mpango mkakati wa mwaka 2013 ili kushinda chaguzi zote kuanzia serikali za vitongoji, vijiji na mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015.
 
Kamati kuu inamuunga mkono,baraza kuu lina muunga mkono na hata mkutano mkuu unamkubi zitto kama Icon of transformation,hizo molemo unazosema ni hekaya za Mbowe na Vibaraka wake,chadema inaamini ktk nguvu ya umma,acheni nguvu ya umma iamue na si vikao vya chumbani vyenye maslahi ya wachache tu. Mwache Zitto atimize wajibu wake ,ninyi endeleeni na majungu pamoja na mikakati haramu ya kumhujumu kisiasa kwa kisingizio cha usaliti lkn hata mwana kijiji amewaonya ktk makala zake hapa JF.
 
Zitto na hao wanaomdhamini wanapoteza mda wao. CDM Kigoma ina mbunge na diwani 1. Hivyo CDM haina/haikuwa na nguvu ya kiivyo Kigoma. Watu wa kigoma kwa maksudi au kutokujua wametumika na Zitto,kwa kisingizio cha Ukigoma,mtoto wa nyumbani!.
 
Eti kamati kuu,teh teh teh,unamaanisha mtei na mbowe? itisheni baraza kuu muone nguvu za Zitto,mbona mnakimbia kivuli chenu wenyewe? baraza kuu mliunda ninyi halafu kiliitisha mwaona kigugumizi,hayo ndio matunda ya unafiki na uzandiki,mwacheni zitto atupe elimu na tupo tayari kuchangia harakati.
 
Huyu mtu sijuin kwanini chama kinamlea kwa kiwango hiki. Huko Kigoma Kaskazini angalau inaweza kueleweka kwamba alikwenda kuongea na wapiga kura wake lakini maeneo mengine anakwenda kama nani? Kama anakwenda kama mwananchi huru au mwanachama wa CCM na ieleweke hivyo na sio kwenda kwa mwamvuli wa chama huku akifanya yaliyo kinyume na kanuni za chama anachojifanya kukipigania.

CDM wamchomoe tuu ,ili akiandaa mikutano atafute chama cha kupewa kibali.
 
Kamati kuu inamuunga mkono,baraza kuu lina muunga mkono na hata mkutano mkuu unamkubi zitto kama Icon of transformation,hizo molemo unazosema ni hekaya za Mbowe na Vibaraka wake,chadema inaamini ktk nguvu ya umma,acheni nguvu ya umma iamue na si vikao vya chumbani vyenye maslahi ya wachache tu. Mwache Zitto atimize wajibu wake ,ninyi endeleeni na majungu pamoja na mikakati haramu ya kumhujumu kisiasa kwa kisingizio cha usaliti lkn hata mwana kijiji amewaonya ktk makala zake hapa JF.

Maajabu ya Mussa..!!
 
CC ya cdm ijilaumu yenyewe! wangemtimua haya mambo tungeyazungumza kwa lugha nyingine kabisa!
 
Hivyo vibali vya mikutano na maandamano anaombea kwa kibali kipi? Anaomba kama kiongozi gani ndani ya chama?

Kuna sheria inayoruhusu mtu yeyote kwenda popote kuomba vibali vya mikutano na maandamano bila kushirikisha chama??

mbona wakati ameshuka airport alipita ofisi za Chadema mkoa ofisi za mkoa nazo hamzitambui¿
 
Sielewi kwanini watu hawaoni hivi vitendo vya Zitto ni tatizo!!

Sidhani kama kuna mbunge wa CCM anaweza kwenda kufanya mikutano kwenye majimbo mengine tu nje ya utaratibu wa CCM.

Sawa endeleeni kumuonea aibu kumwambia ukweli.
Utaratibu wa chama ndiyo upi huo?.

Please, Naomba unisaidie kunieleza na kunifafanulie hivyo vipengele ili na mimi nifahamu vizuri.
 
Back
Top Bottom