Wajumbe Kamati Kuu CHADEMA wamuonya Zitto.

Wajumbe Kamati Kuu CHADEMA wamuonya Zitto.

Unasema umaarufu wa zito unaishia mwandiga?, we umemjuaje?
 
Kajipigilia mwenyewe msumari wa mwisho wa jeneza lake. Nitashangaa kama ataachiwa kuendelea kuwa mwanachama wa CDM.
 
kama gazeti limeandika hivyo na yeye hajalikemea kwenye mkutano wake wa Kasulu au kw namna nyingine yoyote ,amejiongezea kosa.CDM hebu itisheni vikao vyenu mapema mkate mzizi wa fitina.

Kwan akilikemea hilo gazeti ndo maandishi yatafutika?
 
Hapo kwenye Red: Huruma ya nini, si mumfukuze? kwani siku 14 hazijaisha?
Hapo kwenye green: Slaa alienda Jimbo la Zitto bila mwenyeji wake kuwepo. Je hapo FAIR PLAY ikowapi? CHADEMA mmecheza Faulo na Zitto naye anacheza faulo.(Nakumbuka enzi za miaka ya 1970 mechi kati ya Uruguay & Paraguay kuanzi golikipa hadi namba 11 wote wanapiga buti)
Hapo mimi naona kama Ngoma imekuwa droo.

Duh? Ulizaliwa mwaka gani mkuu?
 
Kabwe hana kosa, Chadema wasipoangalia chama kitakatika vipande. Tusubiri tuone.
 
zzk anachofanya ni sawa na kutoboa meli aliyopanda, ili meli iwe salama nafikiri cc wanajua wanatakiwa kufanya nini
 
Kabwe hana kosa, Chadema wasipoangalia chama kitakatika vipande. Tusubiri tuone.
Platform anayoitumia yakuwa mwanachama wa chadema karibu itaisha I thnik ataingia chauma chama akipendacho
 
sasa kama anajimaliza we kinacho kuwa ni kipi? hata ye kaisha jua kwa chadema sio liziki hivyo hana haja ya kuremba na kaisha jipanga kuwa raia mwema wewe acha kuwashwawashwa.
 
Hapa kilichowaudhi ni kwamba watu wamejaa na wamempokea kwa heshima kubwa katika maeneo ambayo Slaa alipigwa mawe.

Ni wivu tu wa kidhaifu, si kingine...
 
zitto washauri wake wa kisiasa watakuwa na upeo mdogo au dogo my be hashauriki...naona kaamua kujimaliza mwenyewe kwa kuonyesh true color yake katika kukiharibu chama...watu wakisema jamaa msaliti kuna watu wa cdm walikuwa wanamtetea,this guy anatumiwa na ccm kutekeleza utabiri wa wasira
Your are very right.

Iweje Wassira aliongea akiwa na overvonfidence,kuwa Chadema itakufa before 2015,wakati kada huyo wa CCM akielewa fika kuwa,Chadema ndiyo chama pekee kati ya vyama vya upinzani,ambacho mamilioni ya waTz,wanakiona ndiyo mkombozi wao wa wanyonge,wanaogandamizwa ndani ya nchi yao.

Sasa iweje makada wengi wa CCM,akiwemo Wassira na Nape wkitabirie kifo Chadema,badala ya kuvitabiria vifo vyama vingine B vya CCM,ambavyo vinaonekana dhahiri vinajifia natural death,kama sio.mchezo mchafu unaotumiwa na magamba,kwa kuwatumia "mamluki" waliomo CDM,wakishirikiana na UWT yao?!!
 
Huyo puppet ni bora tu akatolewa chamani,halafu tuone kwenye platform ya magamba kama ataweza kukusanya hao "wakereketwa" wake kama anavyofanya sasa akiwa CDM.

Awaulize waliokuwa "puppets" wenzie akina Shonza na Mwampanda huko magambani,kama wanaweza kukusanya angalau watu 20 kwenye mkutano mmoja,kama zisipofanyika juhudi za ziada za kuwaleta "wafuasi" wao hao 20 kwa lori,na kuwapa fulana,khanga na kofia za bure huku wakiwaandalia na pilau?!
 
Jambo lingine ambalo linalothibitisha pasipo shaka yoyote kuwa huyu ZZK,anatumiwa na magamba,ni kwa nini wanao sympathize sana kwa yaliyomkuta CDM na wanosihi sana abaki CDM,wawe ni viongozi na wakereketwa wa CCM,kuliko viongozi na wafuasi wa CDM?

Hivi tujiulize swali moja tu,hivi katika hali halisi inawezekana kweli kama ZZK angekuwa "mwiba" wa kikweli kweli kwa magamba,kama walivyo akina Tundu Lissu, Lema, Dr Slaa na Mbowe,kama list hiyo niliyoitaja kama ingesikika fununu tu kuwa wanataka kutimuliwa CDM, viongozi na easterlies wa CCM wangeombea usiku na mchana, viongozi hao nguzo ya CDM watimuliwe haraka,tofauti na hivi sasa kuhusu ZZK,ambapo kutwa kucha, magamba "wanasali" mtu wao abaki CDM,ili awakamilishie,mission yao ya "kuinyonga" CDM!!
 
Kuwatembelea wapiga kura wake, hakuna shida yoyote ile.Lakini kumbuka alisimama kwa tiketi ya chama.

Point ya msingi ni kuwa Zitto amesimamishwa kuwa kiongozi wa chama,still bado ni mwanachama wa chadema na ni mbunge na ana haki ya kutembelea wananchi waliomchagua
 
Kama Slaa na mbowe wanazunguuka kummaliza Zitto, yeye kwanini asifanye counter attack. ZZK ameshafanya hesabu imefika mwisho anajua kilichopita, kilichopo na kijacho na ana options za kutosha na hatimae atakuwa bado ni mshindi.
 
Kabwe hawezi kuondoka mwenyewe kwenye chama. Raha ya kuondoka kwenye chama ufukuzwe. Ukifukuzwa huo ndio mtaji mkubwa wa kisiasa lkn kuondoka mwenyewe ni ishara ya woga. ZZK sio wa calibre hiyo. Jamaa anakokotoa to the simplest form.
 
Back
Top Bottom