Wajibu wa mtoto kuwafanyia wazazi wake mambo 10

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
594
1,827
Assalamualaikum
Mambo 10 unatakiwa kuwafanyia wazazi wako wakiwa hai.

1-Ikiwa umeshafikia balekhe na una jitegemea kimaisha, ni wajibu wako kuhakikisha wazazi wako hawalali njaa. (BABA na MAMA kula yao ni wajibu wako mtoto): Utawahudumia chakula kama wao walivyokuwa wakikuhudumia wakati wa utoto

2-Kuwavisha, mavazi ya wazazi ni jukumu la mtoto

3-Wakikutuma unatakiwa kutumika, nasio unafanya kwa muda unaoutaka wewe.

4-Wakikuita uwaitike, mzazi anapokuhitaji kufika alipo basi hakikisha unafika kwa wakati unaotakiwa kama hakuna kikwazo chochote.

5-Zungumza nao kwa kauli laini na kauli nzuri, (uisilamu umeharamisha kupaza sauti mbele ya mzazi na wala usifoke mbele ya mzazi wala kumkoromea sauti ya base na yenye kiburi)

6-Usiwaite wazazi wako kwa majina yao: Usimwite Baba yako kwa jina lake (mfn: Mzee Fulani) au Bimkubwa au Bibi fulani au mama fulani): Usiwaite wazazi kwa majina yao wala usiwaite kwa majina ya watoto wao: Mwite mzazi kwa heshima yake kama BABA au MAMA. Bila kujali umri wako.

7-Waombee dua wazazi wako kila unaposhiriki ibada au maombi: MUNGU awahurumie kama walivyo kuhurumia wewe wakati wa utoto wako.

8-Usiwatangulie mbele wakati wa kutembea, hadi pale mzazi atapokutaka wewe utangulie mbele

9-Wapatie wazazi wako yale unayo yapenda katika nafsi yako: Na usiwape vile ambavyo umevichoka na usivyo vipenda

10-Jitahidi kuwafanyia wema wazazi wako hata kama walikuacha wakati wa utoto wako.

Baba-akiwa-amembeba-mwanawe.jpg
 
Uzi ni mzuri, ila umeharibu kuweka neno uislam kana kwamba watu wa dini nyingine hawapaswi kupita hapa
 
Wafanyie wema wazazi wako hata kama walikuacha, kima cha mapenzi na upendo vitapungua au visiwepo kabisa lakini wema unatakiwa kubakia palepale
Hasiye ubeba msalaba wake hata Yesu alisema hamfai, timiza wajibu wako kama mzazi ili mtoto wako aje kukutunza kama ulivyo mtunza wewe. Upendo wa mtoto na mzazi unajengwa kwa mzazi kuwajibika.
 
Back
Top Bottom