Waislam msiende liliondo- redio kheir

ELCT wana hospitali nyingi tu kwanini wakubali Babu afanye Tiba "walioibariki" sehemu ambayo kuna mapungufu mengi tu ya Kiafya? ..!!!

Hapa mnaibisha bisheni lkn kuna "ushirikina" ndani yake...!!!! Huyu Babu hana tofauti na Washirikina wengine.

Ila hawa Jamaa wanaoshangilia baadae wakianza kufa kama Njugu wataanza kusema Serikali haijawasaidia...?

Tusubiri tuone ukweli kadri siku zinavyoendelea....!!!
 
Nadhani ungejibu kwanza swali lake vizuri tu bila hasira na kumwelimisha na kisha na wewe kumwuliza ili akuelimishe kuhusu Hiter na Mussolini. Lakini ulivyojibu, unaonesha kama Hitler na Mussolini walikuwa wauaji na walikuwa Wakristo (kama unavyodai), basi hata Alqaida kujilipua ni ruksa kwa vile ni Waislamu. Pili did Hitler and Mussolini kill in the name of their religious belief or political motives as Alqaida claim they are doing it in the name of Allah? Do, you get the point?
Majibu ya kuuwa ni halali au si halali soma juu nimeweka km mara 3. Sina haja ya kufafanua zaid. kwa faida yako, uislamu hauruhusu mauaji yeyote either awe non-muslim au muslim kutoa roho ya mwingine pasipo huyo mtu kuuwa kwa kusudi. Alqaida has nothing to our Glory Qur-an. Km unataka kujudge iSlam judge thru Qur-an na sio blah blah cjui Alqaida cjui nani. Kipindi cha Crusade for christianity mbn siongelei apa wkt mauaji yalifanyika makubwa kwa jina la dini? Na ndo watumiaji wa neno Holywar. Yes Hitler was Christian. Kajipange tena uje hapa na usikurupuke.
 
Ulichokifanya ni kusoma biblia na kukariri (memorise) vifungu fulanifulani. Lakini Biblia haisomwi hivyo. Lazima usome kwa kutafakari na ukisoma kwa kutafakari utapata fundisho fulani na siyo kuishia kukariri maneno au mpangilio wa sentenso. Kuna msemo ambao huwa napenda kuutumia kuonesha tofauti na kukariri. Nao ni huu: "The camel is the ship of the desert". Kwa mtu anayesoma na kukariri maneno atasema: Ngamia ni meli inayopita jangwani, ambako kuna bahari. Anayesoma kwa kutafakari atasema: kama meli ilivyo chombo cha usafiri baharini/ziwani, vivyo hivyo na ngamia jangwani. Kwa hiyo, ngamia siyo meli bali inafaninishwa tu na meli kutokana na ustahimilivu wake jangwani kama ilivyo meli baharini. Biblia nayo inabidi isomwe hivyo. Kwa hiyo, kama umasoma narrative fulani lazima ujiulize narrative hiyo inafundisha nini? Context yake ni nini? Primary addressees wake ni akina nani? Secondary addressees wake ni akina nani? Na pia fundisho lake ni nini? Ukifanya hivyo, ndipo huwa umesoma biblia kwa namna inayotakiwa! Kwa upande mwingine, kama umesoma na hupati fundisho lolote (hujaguswa kutafakari zaidi ulichokisoma) ni sawa na mtu, ambaye hajwahi kuisoma kabisa!
Jibu kwa vifungu sio siasa kny dini. Mfano mie nimekuambia soma Mathayo 5: 30-47 na Mathayo 5 :17-20. Nataka ubishe hayo maandiko kwa vifungu. Usilete story ya nursery ya Camel unajaza page tu!
 
DUUU KWELI KAZI KWELI KWELI YAANI WATU HAWAPIMI NA HAWATUMII ALIKI ZAO ..BADO BONGO...TUKO KWENYE GIZA ZITO KWELI WATU WANAAMINI UCHAWI ? ATI WA DINI YETU ? MIMI NILIFIKIRI NI NIGERIA TU WANALIWA KAMA WANAVOONESHWA TV YA EMMANUEL KUMBE NA WABONGO SO BONGO KWELI NI NAZI KOROMA....
UKWELI HII DAWA NI MPANGO WA KIINI MACHO WHITE MAGIC..YAANI KIINI MACHO. WAKO WANATUMIA KIINI MACHO KUCHEKESHA NA KUFURAHISHA KAMA MICHEZO...NA WAKO WANAOTUMIA WHITE MAGIC KUTAPELI KAMA MFANO WAPO WALIO LIWA KUUZIWA DHAHABU FEKI...AMA WAKO WAMEBADILISHIWA DOLLA KWA MAKARATASI AMA WAKO WAFANYABISHARA WAMEUZA MALI ZAO NA KUPOKEA MAKARATASI BADALA YA NOTI HALISI ..JAPO ALIPOZIPOKEA ALIZIONA HALISI.
SASA MAGONJWA YA BINAADAMU MENGI YANASABABISHWA NA BACTERIA NA VIRUS ...PIA KUNA MARADHI YANAYOSABABISHWA WEKNESS YA MWILI WA BINADAMU KAMA KISUKARI KINACHOSABABISHWA NA MWILI KUTOKUWA NA UWEZO WA KUBALANCE SUKARI INAYOHITAJIWA NA MWILI NA PRESHA,MOYO, HAYA NI MATATIZO YATOKANAYO NA UDHAIFU WA MWILI. NA MARADHI YOTE YAPO KATIKA THE BODY SYSTEM ...MFANO NGOZI..NA MARADHI YAKE...INI NA MARADHI YAKE..UTUMBO NA MARADHI YAKE...NERVES NA MARADHI YAKE...FIGO NA MARADHI YAKE....MIFUPA TA MARADHI YAKE...DAMU NA MARADHI YAKE... PIA KUNA MATIBABU YAKE NI KUPATA DAWA ZINAZOTIBU AINA ZA MARADHI KUTEGEMEA MARADHI AINA GANI NA YA SEHEMU GANI YA MWILI WA BINADAMU..INAWEZA KUWA NI DAWA ZA KISASA AMBAZO NI ZA HOSPITALI NA PIA INAWEZA KUWA DAWA MBADALA YAAANI DAWA ZA MITI SHAMBA..LAKINI DAWA ZOTE SI DAWA TU..YA KILA KITU..NDIO MAANA HUWEZI KUPONA KIPINDUPINDU KWA KULA ASPIRIN !!!!!
KUTOKANA NA RULE HII DAWA YA HUYU PADRI INA WALAKINI....KILA MARADHI YANA DAWA YAKE HAIJAWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA MATIBABU DAWA MOJA IKAWA DAWA YA MARADHI YOTE.
LAKINI WATU WANAENDA KWA PADRI LOLIONDO JEE WAMEPATA USHAHIDI YA MGONJWA TUSEME WA AIDS...ANAEJULIKANA WAZI KWAMBA HUYU ALIKUA KARIBU ANAKUFA NA AKAENDA KWA PADRI LOLIONDO AKAPONA TUNAMHITAJI AJITOKEZE KWA USHAHIDI.
LAKINI KAMA WATU BAADA YA KUSIKIA TU KUNA DAWA NA MTU HAJAWAHI KUJIPIMA KAMA ANA HIV ANAJISHIKU TU LABDA KATEMBEA NA MWANAMKE AMBAYE AMEKUFA KWA AIDS...
TUNATAKA USHAHIDI FULANI AMEPONA...SASA HII NI PROPAGANDA NA KWA SABABU YA UJINGA WETU BASI BILA YA KUFIKIRI WATUU HAOOOO KWA PADRI...
SASA TUJE SEHEMU ILE INAYOHUSU WHITE MAGIC .....HAPA WHITE MAGIC AMA KIINI MACHO KINAWEZA KUTUMIKA KATIKA HILI ,,UKINYWA ILE DAWA UNAPATA GANZI FULANI MAUMIVI ULIYOKUWA NAYO YANAONDOKA LAKINI KAMA NI KISUKARI KIPO ILA HAKIONEKANI KUTOKANA NA YALE MAZINGAUMBWE HUWEZI KUONA LILE TATIZO....NI KAMA YULE ALIPOKEA NOTI ..ANAZIONA NOTI SAWASAWA......LAKINI BAADA YA MUDA BASI YALE MARADHI YAKO YATAONEKANA TENA KWASI YA AJABU KWANI YALIKUA HOLD KUTOKANA NA GANZI YA MAZINGAOMBWE...U
HUU NI UCHAWI SI MAMBO YA MIUJIZA.......HATA YESU ALIMUOMBA mWENYEZI MUNGU KUPONESHA WAGONJWA...YEYE ALIKUA NI MTUME..DUA ZAO ZINAKUBALIWA...NA HAKUNA HATA KATIKA WALE WANAFUNZI WAKE WALOBOBEA KATIKA MAFUNZO YAKE AMBAE ALIKUA NA UWEZO WA KUPONESHA MAGONJWA KAMA ALIVOFANYA MWALIMU WAO YESSU. HUU NDIO UKWELI..LAKINI LEO WAPO MANABII WA UONGO MATAPELI WANAKUJA NA KUSEMA WANAPONESHA WALEMAVU KUTEMBEA...NA VIPOFU KUONA..UTAPELI HUU KILA MWAKA UNATOKEA PALE JANGWANI....NA TANGU UTAPELI WA AINA HII UANZE KUJA HAPA TANZANIA NI KARIBU MIAKA 20 HIVI.(.KABLA YA HAPO HAKUNA MADHEHEBU YA KIKRISTO YALIOKUA YAKIPONYA MAGONJWA ......) NA HAKUNA ISHARA KAMA WALEMAVU WAMEPUNGUA ILA NAONA NI SERIKALI NA WHO KUFANYA KAMPENI YA HALI YA JUU KUHUSU ULEMAVU ...NAYO NI KAMPENI YA CHANJO YA POLIO....HAWA WA JANGWANI NI MATAPELI WALEMAVU WENGI TUNAWAJUA TUNAO MITAANI WENGINE WAKRISTO NA HAKUNA KATI TUWAJUA MITAANI ALIEPONYWA PALE JANGWANI.....HAKUNA KATI NDUGU ZETU VIPOFU AMBAYE AMEPONA HUU NDIO UKWELI..LAKINI UTAONA WATU NA SUTI ZAO WAMEJAZANA KUANGALIA VIPOFU WANAVOPONESHWA KWA MIUJIZA...

NDO MAANA HAYA LOLIONDO SI AJABU....
 
Nawapenda sana waislam, hawa ni ndugu zetu wakristo kabisaaaa!!! Mitume walipiga injili sana Mashariki ya Kati Uislam ulikoanzia. Sasa ili kuumaliza Ukristo Uislam ukaanzishwa, ikawa ni chuki, kuna masacre kubwa ilitokea wakristo walichinjwa kama kuku. Ndo Uislam ukaenea sana na ukristo kufutiliwa mbali mashariki ya kati.

Nina waalika kupata kikombe, si mda mrefu mtarudi home. Kwani sikitambo mambo yanakwenda kuwekwa wazi.

Sio ukristo kurudisha jino kwa jino. Akikupiga kushoto mgeuzie kuli.
 
Wakati wa DECI mlikusanyana pale Sabasaba Kilwa Road mkasema maneno haya haya. Oooh Yesu anagawa utajiri, kwa Mungu yanawezekana! mwisho ukweli ukajulikana kuwa ilikuwa ni SCAM! Nashangaa wale maaskofu walioshadidia hili hawakuwaomba radhi!

Leo unakuja ushetani mwingine watu mnaleta stori zilezile! Soon ukweli utajulikana msije mkabadilisha kauli hapa!

La msingi, nani aliyepimwa na kuthibitika ana HIV antumia ARV akaenda huko kwa babu akapona? Apimwe tuthibitishe kuwa kapona! Msitulee stori za imani imani hapa!

wewe huna kumbukumbu,DECI haikufilisika ila serikali ilipora hela za deci,..acha uzushi fuatilia mambo kabla hujaropoka...deci ilikuwa inaendelea vizuri tu ila njama za jk ndo ziliiua deci
 
Hilo ni tatizo la imani bila elimu dunia....KAZI KWELI KWELI
Hizi dini tulizorithi au kupokea zinatupeleka pabaya sasa!


Watu wanajitafutia tiba mbadala, wengine wako busy na vipaaza sauti wakiwakataza! tuone itakavyokuwa.

HUU UDINI UNATUFUNDISHA NINI HAPA TANZANIA?
 
Wanaakili za kitoto kabisa hawa wao ni waislamu gani?wamekunywa dawa waislamu wanaojiita waislam toka oman,Watu wamekwisha kujitangaza hawasikilizi wala hawafuatilii habari hawa jamaa wanaojiita waislam,kwenye vyombo vya habari mbona wamejitangaza,TV,Magazeti,Redio na mitaani pia mimi nisingekwenda kama kumuona mwenye kisukari cha kuchoma sindano kupona na mwenye Ukimwi kuacha kutumia ARV baada ya kurudi toka kwa mchungaji.
kilichopo hapa hawa jamaa na ubinafsi wao ndio unaowasukuma kusema hivyo,kwa kuwa ni mkristo anayetoa tiba ndio maana hawataki waislamu watibiwe na mkristo si waache hospitali za wakrito na waenda za waislamu?Walie tu serikali yenye mkono mrefu imeshindwa sembuse wao,waende na wao wakanywe kikombe bana wasijivunge.
Hivi ina maana JK (aka mzee wa kiduku) sio muislam? Maana babu alisema wakati anazungumzia foleni kuwa mtu pekee aliyemruhusu kutokaa foleni ni Raisi (pamoja na kwamba alikwenda kablafoleni haijawa kubwa) kwa kuwa Mungu anataka watu waheshimu kila mamlaka kwa hapa duniani ---lakini kwa wengine wasipokaa foleni hawatapona!!! Huo ni uthibitisho kuwa raisi alipata tiba pale na nijuavyo mimi ni muislam safi na muumini wa hata sheikh Yahya (ustaadhi)
 
Hili hawawezi kulizuia, watu wanashida nyingi wao wanasema wasiende? Ili iweje wakati mmeshindwa kuwatibu?

Huwezi kuzuia mtu kufanya anachofikiri Maana Kazi ya watu ni kukumbusha wenye akili watakumbuka waliopotea wataendelea kupotea.
Redio kheir wako sahihi wamekumbusha waislam wao kuwa suala hili halipo kwenye mafundisho ya Kiislam, Suala la waislam kwenda hilo ni la kila mtu. waislam hatupingi dawa kwa sababu ni ya mchungaji hata sheikh yahya anapingwa dawa zake ni za shirk haifai muislam kwenda kutibiwa kwake, mambo ya nyota ni haram katika uislam. Mbona waislam tunatibiwa Bugando KCMC n.k? Wanachosema Misingi ya dawa kidini haifai hivyo tu.
 
Kila mtu binafsi anajua anaumwaje, siamini kama mtu mwingine anaweza kukushawishi uende kwenye tiba au usiende.
 
Kuna watu wanaropoka tu bila kujua UISLAM unasemaje kuhusu unabii/utume.Waislam humkubali YESU ,yupo hai na hakuuwawa;Lakini mtume na nabii wa mwisho ni MOHAMMAD s.a.w so kama kuna mtu anaamka na kusema yeye ni nabii kama asemavyo Babu thatz Y waislam wanazuiwa.Hata huyo mnayemsema shekh yahya ni mzushi tu kama kakobe, babu ,lwakatare,mzee wa upako nk
 
Huwa mambo mengine yanashangaza sana,ubnafsi sio kitu cha maana hata kidogo,,Ok mnavokunywa panadol au dawa ya malaria mnajua ninani anayetengeneza!!!! Ni dini? Kuweni na mawazo chanya acheni mwanzo hafifu.Na in short km unaona hiyo dawa ya mchugaji haikufai na sio mwisilamu stop,kwanza mnavoenda kule mnasababisha hate cream ya dawa inapungua.
 
Kuna mtu anapanda mbegu ya kutugombanisha, mbona tunashirikia vizuri kwenye vijiwe vyetu?
1. Misiba tupo pamoja
2. Kwenye shida tupo pamoja Masuala ya Dowans, Maji na Bei ya vyakula na petrol
3. Kwenye viti virefu na K'moto'S tupo pamoja

Sasa wewe unayetufitini una ajenga gani ya siri? tumeshakujua jirekebishe na kundi lako - tukielewana utaumia
 
Anayewasihi waislam wasiende mweyewe keshawahi kikombe,au ni namna nyigine ya kuwaelezea kuwa waende nina wasiwasi na huyu mtu anaweza kuwa mchawi.:hatari:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom